Malkia Elizabeth amtaja mrithi wake

Malkia Elizabeth amtaja mrithi wake

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,303
1523375699117.jpg


Malkia Elizabeth ametoa kauli hiyo leo alipokuwa kwenye mkutano wa nchi za Jumuiya ya Madola (commonwealth) uliofanyika nchini Uingereza, ambapo Tanzania pia imehudhuria.


Akisoma hotuba yake kama mkuu wa Jumuiya hiyo Malkia Elizabeth amesema “ni matumaini yangu kwamba Jumuiya ya Madola itaendelea kutoa utulivu kwa kizazi kijacho, na kuamua kuwa siku moja Mwana Mfalme wa Wales ataendelea kubeba kazi muhimu iliyoanzishwa na baba yangu mwaka 1949”.


Kwa kauli hiyo ya Malkia Elizabeth, ulimwengu unaamini kuwa mtoto wake wa kwanza wa kiume Charles, ndiye atakuwa mrithi wa kuongoza jumuiya hiyo kubwa duniani, ambayo ina nchi wanachama takriban 53.


Kwenye mkutano huo Tanzania imewasilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, huko jijini London nchini Uingereza.

Chanzo: EATV
 
Tumeona Faida za wenzetu kama Wakenya kupitia Rais Kenyatta alipohudhuria moja wapo ya Makongamano hayo na kama sikosei ni hili la madola, alitumia vizuri Fursa hiyo kuvutia wawekezaji Wajerumani kuja kuwekeza Kenya,
Nini kama watanzania tutarajie kukipata baada ya Makamu wa Rais na Waziri wake Augustino Mahiga kuhudhuri jumuiya hiyo ? Au tunaendelea kuchoma hela za watanzania tu kwa safari zilizozoeleka miaka nenda rudi bila ya kutunufaisha na lolote !
Ifikie mahala tuone Faida ya safari hizo , hela nyingi zinapotea.
Budget inayopitishwa na bunge kwa Wizara ya Mambo ya nje ina nia njema kabisa, lkn hatuoni Matunda haswa haswa ktk hili la safari hizo !, Viongozi wetu wawe wanaandaa agenda jenzi zingine pembeni zenye manufaa kwa Tz wakitaka kuhudhuria makongamano ya kimataifa kama hayo ,sio kuhudhuria tu kama wanaenda kusalimia Bibi na Babu zao kijijini, waende na agenda mbadala za kuwashirikisha wanaoenda kukutana nao kwa ajili ya manufaa ya Tz na Watz wote, sio kwenda kusikiliza tu na kutuletea Mrejesho kilichokuwa kinafanyika huko,tunataka tuone taifa likishiriki na sio wasikilizaji.
 
Back
Top Bottom