Taured
JF-Expert Member
- Dec 12, 2010
- 805
- 679
Wasaalam naomba kujua nimekuwa nikinunua nafaka maduka ya jumla Mbagala rangi tatu kama vile maharagwe, mchele, mahindi nakadhalika jambo lililosababisha niletee mada hapa ni pale unapopimiwa mzigo halafu unadaiwa hela ya kupima mfano kilo10 utamkuta mpimaji sh 100, kilo 20 Utalipa sh 300 na kama uzito unaongezeka basi na hela itapngezeka! Sasa najiuliza hivi ni halali mambo haya au ni utaratibu upi kisheria unaomlazimu mteja kulipia gharama za vipimo? Je naweza kununua bidhaa bila kupimiwa? Na kama haiwezekani kwa nini nilipie hiyo huduma wakati ni jukumu la mpimaji kufanya hivi?