Dickson Ng'hily
JF-Expert Member
- Oct 22, 2010
- 473
- 508
Uongozi wa hospital ya Taifa yaMuhimbili (MNH), kuanzia tarehe 11 mwezi ujao itaanza kukusanya mapato yake kupitia benki ya NMB. Hii inatokana na makubaliano waliyoyaingia mwezi january mwaka huu.
Katika utaratibu huu mpya wa ukusanyaji mapato, mgonjwa atatakiwa kuwa na hati ya gharama ya malipo (bill note) itakayotolewa na wafanyakazi wa hisitali hiyo katika vituo vitakavyokuwa karibu na maeneo ya kutolea huduma.
Hati hiyo ya gharama itaonyeonyesha ni huduma ambazo mgonjwa anahitaji kulipia na kiasi cha fedha zinazopaswa kulipwa.
Baada ya kupata hati hiyo, mgonjwa ataelekezwa sehemu kilipo kituo cha benki ambako atafanya malipo na kisha kwenda sehemu ya kupata hudma inayohitajika.
Inasemekana kuwa, kufanikiwa kwa zoezi hili kutaiwezesha hospitali kuvuka lengo la kugharimia bajeti ya matumizi ya kawaida, kwa kutumia mapato ya ndani kwa asilimia arobaini (40%) kama sera ya mabadiliko ya taasisi za umma inavyoelekeza (public sector reforms).
Kwa sasa hospitali hiyo inagharimia bajeti yake ya matumizi ya kawaida kwa kutumia mapato ya ndani kwa asilimia 58 (58%).
Pia menejiment ya hospitali inasema kuwa mabadiliko haya ya mfumo wa ukusanyaji wa mapato kupitia benki, yataongeza makusanyo ya ndani kwa asilimia hamsini (50%) au zaid na hivyo kuongeza uwezo wa kifedha wa hospitali kugharamia bajeti ya matumizi ya kawaida kwa kutumia mapato ya ndani kutoka asilimia 58 hadi 72 katika mwaka wa fedha 2013/2014.
SOURCE: Taarifa kwa Umma toka Muhimbili iliyotolewa katika Ukumbi wa habari Maelezo.
Maelezo yangu:
Nashindwa kuelewa ni kwa namna gani wataondokana na foleni kwani katika huduma za kawaida NMB imekuwa ikiongoza kwa kuwan na foleni ndefu na hivyo kuwachuku wateja wake saa nyingi kabla ya kupata huduma.
Sasa kwa hili la wagonjwa itakuwaje! Ina maana Muhimbili wameshindwa kubuni njia nyingine ya kudhibiti mapato lakini wakihakikisha kuwa mteja wao (mgonjwa) hapati usumbufu wowote! Maana kwa hili naona kama wanalenga zaidi kukusanya mapato lakini sio kuboresha huduma za afaya ili mgonjwa asisumbuke.
Je ule mpango uliotangazwa juzi huko Mtwara na Mkurugenzi wa Bima ya Afya kuwa wanataka kuhakikisha watanzania wote bila kujali uwezo wao wa kiuchumi wanajiunga nayo na hivyo kupata huduma za afya kwa urahisi umefikia wapi? Na kwanini Muhimbili wasingeshauriana na NHIF ili kama suala ni kudhibiti mapato basi wangekuwa wanalipwa kupitia hundi za hao jamaa.
Kwa mfumo huu mpya, Muhimbili inakusudia kuvuruga urahisi wa huduma kwa wagonjwa kwani kwa utaratibu tu uliopo hali sio nzuri je huo wa malipo kupitia benki si ndo utaharibu kabisa!
Mwisho wadau wenye uzoefu na hili hebu mnisaidie kuwaelewa hawa Muhimbili…….