Malipo ya Tiba Muhimbili sasa ni kupitia NMB

Malipo ya Tiba Muhimbili sasa ni kupitia NMB

Tutafia kwenye foleni!
Upange foleni weeeeh, umuone dr.
Upangwe weeeeh ukalipie vipimo.
Upangwe weeeeh, uingie maabara.
Unangojea majibu.
Unapangwa weeeh, unamuona dr.
Anakuandikia dawa.
Upangwe weeeeh, ukalipie dawa bank.
Ukifika dirisha la dawa unaambiwa hakuna hiyo dawa yako.
Unarudi bank.
Sijui ukijipanga wanakurudishia kahela kako?

Kwani kuinstal system kama ile ya agha khan kuwa ukifika unapewa docket for the day na kila mhusika anaupload itakuwaje?

Kila kunapokucha Tanzania utakosa kioja,Eee Mwenyezi Mungu angalia waja wako wanavyoteseka.
 
Duuh, njia mpya hii itatumika kwenye matibabu ya dharula pia?

Ni bora NMB waeke branch yao hapo hapo muhimbili.
 
Mwe!!!!!!!!!!!!!!!!!!ssa wale wakutoka tumbi inabidi waanzie NMB au? kweri mbuzi yake kamba,ukimuona na nyororo uyo simbuzi tena bali nimbuzi wa IRINGA.
 
Na nikilipia halafu bahati mbaya daktari niliyepangiwa kumuona apate dharura na asinione inakuwaje? watarudisha pesa yangu ama?
 
kitu kimoja tu. Pawekwe dirisha la NMB kwenye ofisi ya cashier. Mgonjwa kwenda kulipia mbali na hapo (huku akitapika, au kugugumia kwa maumivu) haitawezekana.
Pia, mtu akipata ajali akaanzia kutafuta PF3, halafu aende kwenye foleni ya NMB likely atakufa njiani, mipango ya REFUND iwekwe wazi.
NMB waandae WODI ya kupumzisha wagonjwa wanaokwenda kulipia ...full manesi, dripu na mops.

Halafu vituo vya malipo vitafanya kazi kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni siku za wiki. Maana yake ni MARUFUKU kwenda kupata huduma Muhimbili kuanzia saa 10 jioni, na siku za weekend na sikukuu. Maana yake ni MARUFUKU kuugua nyakati hizo.
 
dah kwa hili la NMB na MNH kuna maswali mengi kuliko majibu, wadau wengi wana wasiwasi sana and they have legitimate reasons za kuhofu....

katika tamko la MNH wao wanazungumzia zaidi namna watakavyonufaika kimapato kama malipo yatapitia bank na kupunguza ufisadi, kwamba wataweza kuongeza uwezo wa sasa wa kujitegemea from 58% to 72% kwa kutegemea mapato ya ndani. Kwa taasisi yeyote ile popote pale this is greaaat news and mafanikio makubwa ya kupongzwa kwa CEO na team yake nzima and of course their dearest clients, I mean wagonjwa for God sake!

Na kumbuka tamko la MNH limesisitiza mapato zaidi. They never wanted kujali kuzungumzia wateja wao kwa maana ya wagonjwa amabao ndio hasa inafanya wao wawepo na waweze kuzungumzia habari hizi. Na wagonjwa wao wanahitaji huduma bora!

Watu wanahoji mambo ya msingi sana yenye kuhitaji majibu ya kina yasiyo na shaka yeyote:
1. Watu wanauliza hatua hii itaboresha vipi utoaji na upatikanaji wa huduma bora kwa urahisi na gharama nafuu kwa 'common' citizen?

2. Je, mpango huu ni shirikishwaji kwa kiasi gani kwa wadau wote (madaktari, manesi, wagonjwa, famasia, maabara etc etc) ili kumlinda client/mgonjwa na usivurugue bali iboreshe huduma?,

3. Je utanishawishi vipi kwamba huduma hii haitachelewesha upatikanaji wa huduma? Mathalani katika emergency kama ajali etc?

4. Je hakukuwepo na njia bora zaidi ya hii- kwa mfano docket system itumiwayo na Agha Khan? Au hata njia kama mpesa, tigopesa, airtel money kwanini zisingekuwa optional?

5. Je iwapo nimelipa pesa benk na sijapata huduma ntarudishiwaje pesa zangu bila usumbufu wowote?.

5. Je katika utaratibu wa kawaida wa utendaji kazi wa madaktari na kada zote za afya how practical is this?-kwa mfano mimi nina tatizo la presha na nahitaji kumuona spesholist wa moyo na hapo hapo nina tatizo la mkojo ambapo ninapaswa kupata uchungzuzi na ushauri kutoka kwa daktari wa mkojo sasa je huo utaratibu hautaniletea usumbufu?

6. Sasa hao NMB watakuwa na payment points kila wodi, maabara ama? Just to ease payment kwa wagonjwa.

7. Maswali ni meeeeeengi sana na yanahitaki majibu timilifu yenye kuonesha evidence based practise from somewhere else. Otherwise no need to re-invert the wheel unaweza copy kutoka kwa taasisi zingine utaratibu wao.

Muhimu kuliko yote tusisahau MNH ni taasisi ya umma and zaidi pia its a nationa referral and consultancy health provider in our country. It is an icon of health in this country.

Uongozi wa MNH na hata serikali kupitia wizara ya afya ina wajibu kwa umma wa kutoa maelezo yenye kutosheleza, short of that wananchi pengine kupitia Bunge au kamati ya huduma za jamii (hili sina uhakika nalo sana) hatuuingi mkono hatua hii

unless MNH PROVIDE majibu sahihi hapa naona kuna tabu na chaos mbele ya safari
 
kitu kimoja tu. Pawekwe dirisha la NMB kwenye ofisi ya cashier. Mgonjwa kwenda kulipia mbali na hapo (huku akitapika, au kugugumia kwa maumivu) haitawezekana.
Pia, mtu akipata ajali akaanzia kutafuta PF3, halafu aende kwenye foleni ya NMB likely atakufa njiani, mipango ya REFUND iwekwe wazi.
NMB waandae WODI ya kupumzisha wagonjwa wanaokwenda kulipia ...full manesi, dripu na mops.

Halafu vituo vya malipo vitafanya kazi kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni siku za wiki. Maana yake ni MARUFUKU kwenda kupata huduma Muhimbili kuanzia saa 10 jioni, na siku za weekend na sikukuu. Maana yake ni MARUFUKU kuugua nyakati hizo.


Hapa ndo nimeamini kauli ya CHADEMA kuwa kuna baadhj ya watu wanafikiria kwa kutumia masaburi...samahani msiombe mwongozo.
 
Yani badala ya Great thinkers kuhoji kwa nini huduma tlizozoea enzi na enzi zikiwa bure leo tunalipia, nyie mnajadili Namana ya kulipa.
Ushahuri wangu ni kuwa ni wajibu waserekali kutoa huduma ya afya buree namaanisha bure na hilo lina wezekama kabisa kwa kodi zetu.

Otherwise ni kuhakikisha nchi hii kila mtu ana bima ya afya.
 
kuna watu walikaa kwenye kikao wakajadiliana na kulipana posho kisha wakaja na uamuzi huu?????
 
NMB, yaani unamanisha NMB ninayoijua mimi, Duh naona sasa wameamua kutua kabisa, Kama kweli NMB ninayoijua ambayo nikienda kulipa ada ya shule wala sio shughuri za biashara natumia almost siku nzima nikiwa na afya tele nakuwa hoi bin taabani, je kama nitakwenda nikiwa naumwa/mgojwa si nafia huko kabisa, Hapana hebu uongozi watafakari zaidi, ila kama wameamua kutuua sawa waendelee na mpango vinginevyo nasema hapana.

USHAURI


Wafungue matawi yasiopunguwa matatu (3) around MNH na yasifanye kazi tofauti na hiyo na kuwe na Teller za kutosha.
 
BADILI TABIA hivi umejiuliza inakuwaje mtu anapewa fomu ya malipo yenye orodha ya huduma na ana kwenda kulipa kabla ya kujua ana tatizo gani?

Hii si huduma kama ya nyanya au sukari ambayo mtu unaweza kusema tu na hitaji huduma fulani na ukalipia na kupewa! Hapa tuna zungumzia huduma ya afya ni lazima nimuone daktari kwanza ndio nijue tatizo langu labda naumwa malaria au typhord!

Labda kama mtoa mada kokosea ku nukuu aelezo na labda kama kinacho lipiwa ni kumuona daktari au card!

Na kwa hili wana taka kutafuta posho tuu si kuboresha huduma japo wao wanasema wanataka kudhibiti wizi wa pesa!

kuna watu walikaa kwenye kikao wakajadiliana na kulipana posho kisha wakaja na uamuzi huu?????
 
Last edited by a moderator:
Uongozi wa hospital ya Taifa yaMuhimbili (MNH), kuanzia tarehe 11 mwezi ujao itaanza kukusanya mapato yake kupitia benki ya NMB. Hii inatokana na makubaliano waliyoyaingia mwezi january mwaka huu.

Katika utaratibu huu mpya wa ukusanyaji mapato, mgonjwa atatakiwa kuwa na hati ya gharama ya malipo (bill note) itakayotolewa na wafanyakazi wa hisitali hiyo katika vituo vitakavyokuwa karibu na maeneo ya kutolea huduma.

Hati hiyo ya gharama itaonyeonyesha ni huduma ambazo mgonjwa anahitaji kulipia na kiasi cha fedha zinazopaswa kulipwa.

Baada ya kupata hati hiyo, mgonjwa ataelekezwa sehemu kilipo kituo cha benki ambako atafanya malipo na kisha kwenda sehemu ya kupata hudma inayohitajika.

Inasemekana kuwa, kufanikiwa kwa zoezi hili kutaiwezesha hospitali kuvuka lengo la kugharimia bajeti ya matumizi ya kawaida, kwa kutumia mapato ya ndani kwa asilimia arobaini (40%) kama sera ya mabadiliko ya taasisi za umma inavyoelekeza (public sector reforms).

Kwa sasa hospitali hiyo inagharimia bajeti yake ya matumizi ya kawaida kwa kutumia mapato ya ndani kwa asilimia 58 (58%).

Pia menejiment ya hospitali inasema kuwa mabadiliko haya ya mfumo wa ukusanyaji wa mapato kupitia benki, yataongeza makusanyo ya ndani kwa asilimia hamsini (50%) au zaid na hivyo kuongeza uwezo wa kifedha wa hospitali kugharamia bajeti ya matumizi ya kawaida kwa kutumia mapato ya ndani kutoka asilimia 58 hadi 72 katika mwaka wa fedha 2013/2014.

SOURCE: Taarifa kwa Umma toka Muhimbili iliyotolewa katika Ukumbi wa habari Maelezo.

Maelezo yangu:

Nashindwa kuelewa ni kwa namna gani wataondokana na foleni kwani katika huduma za kawaida NMB imekuwa ikiongoza kwa kuwan na foleni ndefu na hivyo kuwachuku wateja wake saa nyingi kabla ya kupata huduma.

Sasa kwa hili la wagonjwa itakuwaje! Ina maana Muhimbili wameshindwa kubuni njia nyingine ya kudhibiti mapato lakini wakihakikisha kuwa mteja wao (mgonjwa) hapati usumbufu wowote! Maana kwa hili naona kama wanalenga zaidi kukusanya mapato lakini sio kuboresha huduma za afaya ili mgonjwa asisumbuke.

Je ule mpango uliotangazwa juzi huko Mtwara na Mkurugenzi wa Bima ya Afya kuwa wanataka kuhakikisha watanzania wote bila kujali uwezo wao wa kiuchumi wanajiunga nayo na hivyo kupata huduma za afya kwa urahisi umefikia wapi? Na kwanini Muhimbili wasingeshauriana na NHIF ili kama suala ni kudhibiti mapato basi wangekuwa wanalipwa kupitia hundi za hao jamaa.

Kwa mfumo huu mpya, Muhimbili inakusudia kuvuruga urahisi wa huduma kwa wagonjwa kwani kwa utaratibu tu uliopo hali sio nzuri je huo wa malipo kupitia benki si ndo utaharibu kabisa!
Mwisho wadau wenye uzoefu na hili hebu mnisaidie kuwaelewa hawa Muhimbili…….


Hili nalo ni janga lingine tena
 
boooongo! only in tz malipo ya mgonjwa yanaanzia bank.
 
Itakuwa vema iwapo NMB watafungua tawi maalum/dirisha la makusanyo haya. Ni sawa na jinsi Citi Bank walivyo na dirisha pale TRA la kukusanya kodi.

Ndg! Siamini. Kweli unafananisha makusanyo ya TRA na huduma za Afya? Sitaki kuamini hivyo. Je umewahi kukutana na mwanamke mwenye uchungu wa KUZAA? Je atapitia NMB kwanza? Ukipata ajali wasamaria wema wakakuokota, je wakupitishie kwanza NMB? Are you serious.

Muhimbili walitakiwa kushirikiana na Bima ya Afya, if possible wahakikishe wananchi wengi wana bima ya Afya. Kuwe na mahali unatumia kadi ya dole gumba ili hata Kama uko unconscious basi wakiweka sahihi ioneshe uanachama wako na utibiwe mara moja.

Mwisho hili ni swali, kwani siku hizi MNH nayo imekuwa ni kampuni ambayo ni profit oriented?

Bless you.

Queen Esther
 
Ndg! Siamini. Kweli unafananisha makusanyo ya TRA na huduma za Afya? Sitaki kuamini hivyo. Je umewahi kukutana na mwanamke mwenye uchungu wa KUZAA? Je atapitia NMB kwanza? Ukipata ajali wasamaria wema wakakuokota, je wakupitishie kwanza NMB? Are you serious.

Muhimbili walitakiwa kushirikiana na Bima ya Afya, if possible wahakikishe wananchi wengi wana bima ya Afya. Kuwe na mahali unatumia kadi ya dole gumba ili hata Kama uko unconscious basi wakiweka sahihi ioneshe uanachama wako na utibiwe mara moja.

Mwisho hili ni swali, kwani siku hizi MNH nayo imekuwa ni kampuni ambayo ni profit oriented?

Bless you.

Queen Esther

Queen,
jinsi ulivyoniaddress ni kama vile mimi ndiye niliyeweka huo utaratibu!!!
Comment yangu nimeitoa in a sense kwamba kwa vile utaratibu huo umeshawekwa basi ni bora kuwe na tawi maalum au madirisha maalum ya kulipia hizo huduma ili wagonjwa wasikae foleni na watu wanaokuja kudeposit na kuwithdraw pesa za shopping.

Personally siwezi kuwa na kauli ya kuunga mkono au kupinga uwepo wa utaratibü huo kwa sababu sina taarifa za kutosha za sababu zilizopelekea kuanzishwa kwake.
 
Back
Top Bottom