Imekuwa kama kawaida malipo ya pensheni ya kila mwezi kwa mfuko wa PSSSF yanakuwa tayari kila tarehe 24 ya mwezi. Mfuko pia unatuma ujumbe(sms) unaompa taarifa mstaafu kuwa malipo hayo yameshatumwa benki.
Hii ni tofauti na mwezi huu wa Agosti ambapo malipo hayafanyika na taarifa iliyozoeleka pia haijatumwa. Je, kuna tatizo au ndiyo fedha za wastaafu zilizopigwa kama ilivyoripotiwa kwenye vyombo vya habari hivi karibuni? Au je, kuna uhusiano na tozo mpya za mabenki?
Idadi kubwa ya wastaafu wana marejesho ya mikopo ya benki yanayokatwa moja kwa moja kupitia mafao yao ya kila mwezi. Kama ni kweli kuna tatizo je, mabenki yatalichukuliaje jambo hili ukizingatia kuwa tatizo halijasababishwa na wateja wao?