Malipo ya hundi za kimataifa

Clemford

Member
Nov 26, 2011
63
91
Naleta kwenu wadau.

Kuna rafiki yangu mmoja mfanyabishara. Alilipwa fedha zake kwa hundi (cheques). Drawers' Bank ni za Marekani na mlipwaji ni Mtanzania. Aliwasilisha hundi zake kwa ajili ya malipo kwenye Benki moja hapa mjini.

Hundi zikawa deposited. Amesubiri kwa muda wa siku zaidi ya sabini lakini bado akaunti yake haijawekewa fedha. Wala hajarudishiwa feedback yoyote kama cheque zina shida yoyote. Watu waliomlipa wamemweleza kwamba accounts zao kwenye benki zao kule marekani ziko debited. Lakini account ya huyu jamaa huku bongo haiko credited.

Naomba wenye ufahamu zaidi wa masuala ya Benki wanijuze kwamba hali hii inasababishwa na nini? Benki ya hapa Tanzania hawaonyeshi kuwa na ushirikiano mzuri, mara simu hazipokelewi, email hazijibiwi n.k. Je, kwa kawaida inachukuwa muda gani kwa international cheque clearance? Na kama muda wa ukomo umepita nini chaweza kufanyika?
 
Back
Top Bottom