Malinzi jitumbue mwenyewe kwenye hili

SONGOKA

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
1,841
1,843
Nimesikitishwa kusoma katika magazeti ya leo eti TFF imepata hasara ya Tsh 500 milioni mwaka 2014, lakini kilichosababisha hasara hiyo ndo kimenifanya niruke mita 1000 kimanga kwa mshangao

Sababu zilizotajwa ni pamoja na "fedha za fidia za kukatiza mkataba wa Kim Poulsen" na malipo ya deni la Tsh 150 Milioni kwa mshkaji wake malinzi ambaye ni kiongozi hapo TFF eti kwa deni alilokopesha TFF, pamoja na kodi ya ofisi zaidi ya milioni 150
Ndugu Jamal Malinzi kumbuka tarehe 27 februari 2014, ulitutangazia kuwa wewe na rafiki zako mmejitolea kuchanga pesa za kulipia fidia ya kocha Kim Poulsen,. Nakumbuka kukuonya huo uamuzi wako kwa thread hii Malinzi acha kutudanganya , tena acha. , lakini ulipuuza na kesho yake tarehe 28 februari 2014 ukasisitiza eti mmejitolea. Sasa swali ni je inakuwaje katika hesabu za mkaguzi tunaona tena gharama za kusitisha mkataba wa kocha ambaye ulitwambia mnamlipa wewe na rafiki zako

Pili, nilikuuliza hizo pesa mna mpango wa kujilipaje, sasa leo nashangaa eti jamaa yako hapo TFF anapiga panga la Tsh 150 kwa kisingizio aliikopesha TFF, unaweza kutwambia aliikopesha TFF KWA SHUGHULI GANI, na toka lini taasisi za umma zikakopa kwa mtu binafsi tena mfanyakazi wa taasisi hiyohiyo, HUONI HUO NI MGONGANO WA MASLAHI (CONFLICT OF INTEREST)

tatu,hivi ni kweli eti msimu mzima unakusanya viingilio milionil 842?? seriously?? na hapo unajumlisha mechi za taifa stars??
alafu nani anakwambia unahama ofisi ya umma na ya shirikisho na kwenda kupanga, alafu mwisho wa mwaka unatwambia eti sababu za hasara ni pamoja na kodi ya ofisi zaidi ya mil 150, are u serious???

Ndugu malinzi jitumbue mwenyewe, kabla hatujakutumbua,

Natambua uwepo wako humu (ingawa nimejaribu kukutag sikukupata), naomba uje kujibu hizi hoja
cc. napenauye
 
Malinzi ni mpigaji mkubwa ndio maana mpaka sasa hataki kutumia mashine za electronic na anatumia pesa nyingi kuwaziba midomo wajumbe wa mkutano mkuu wa tff ndio maana hawawezi kuhoji wizi wake
 
Viongozi wa soka kuanzia ngazi ya vilabu na mashirikisho karibia wote Tanzania nzima wapo kwa ajili ya kupiga dili tu ndo maana hatusogei. Tatizo wengi wao wamezifanya zile nyazifa zao kama ajira rasmi na sehemu pekee ya kuondokana na ukali wa maisha.
 
Huyu Malinzi hata kuliona jina lake tu mahali popote pale naboreka na tifutifu yake kwa ujumla. Siku ambayo niligundua kuwa huyu mtu hatatufaa ni pale alipokapindisha sheria ya kadi tatu za njano eti mchezaji anaweza kuchagua game za kukosa ndio nilijua huyu Mhaya sio kabisa.
Kabla hilo halijafutika kichwani mwangu likaja lile la kuhamisha ofisi za tff, nalo hilo nawa kwann huyu Mhaya amefanya hivi!!!! Si akawaruhusu azam waenda Zambia kwenye bonanza huku ligi ikiwa katikati ya mashindano????
Hivi amebakiza muda gani pale tff maana nasikia anataka kupunguza idadi ya wajumbe pale tff, sijui hili nalo likoje?????
 
Umeone eeeeeeh!!!
 
Huyu jamaa ni boya, kuna siku kaitisha mkutano na waandishi wahabari, akaanza kufoka kwa hasira kama anaongea na mke wake, au watoto wake nyumbani...!

Nilimuona fala kabisa, hajui hata uongozi...! Nadhani wale waliokuwa wanampigia debe, leo wanatamani ardhi ipasuke, waishilie huko...!
 
Mkuu mbona inaonekana ulikuwapo kwenye huo mkutano! Na kama ulikuwapo na ukashindwa kumtia vibao nitakulaumu sana. Watu kama hao ukichapa makofi umati wa watanzania watakupongeza sana
 
Huyu Malinzi hata kuliona jina lake tu mahali popote pale naboreka na tifutifu yake kwa ujumla. Siku ambayo niligundua kuwa huyu mtu hatatufaa ni pale alipokapindisha sheria ya kadi tatu za njano eti mchezaji anaweza kuchagua game za kukosa ndio nilijua huyu Mhaya sio kabisa.
Kabla hilo halijafutika kichwani mwangu likaja lile la kuhamisha ofisi za tff, nalo hilo nawa kwann huyu Mhaya amefanya hivi!!!! Si akawaruhusu azam waenda Zambia kwenye bonanza huku ligi ikiwa katikati ya mashindano????
Hivi amebakiza muda gani pale tff maana nasikia anataka kupunguza idadi ya wajumbe pale tff, sijui hili nalo likoje?????
kwani aliyeagiza upangaji Wa matokeo ya ligi daraja la kwanza naye ni Malinzi.halafu ndugu ukabila tuache mana kutanguliza ukabila ni ukaburuuu,hoja yako itakosa uhalalii,itakosa legitimacy.
 
Huyu jamaa ni boya, kuna siku kaitisha mkutano na waandishi wahabari, akaanza kufoka kwa hasira kama anaongea na mke wake, au watoto wake nyumbani...!

Nilimuona fala kabisa, hajui hata uongozi...! Nadhani wale waliokuwa wanampigia debe, leo wanatamani ardhi ipasuke, waishilie huko...!
mi mmoja wapo mkuu uyu bwana kanitoka kabisa sijui wale waganga njaa wenzangu wa CLOUDS wajisikiaje sasa looh punga kbs uyoo
 
kwani aliyeagiza upangaji Wa matokeo ya ligi daraja la kwanza naye ni Malinzi.halafu ndugu ukabila tuache mana kutanguliza ukabila ni ukaburuuu,hoja yako itakosa uhalalii,itakosa legitimacy.
Mkuu balibabambonahi hilo nalo ni jambo jingine linalonifanya nizidi kumuona Malinzi kama mtu hatari katika soka letu, hebu fikiria tangu siku ile habari ilipobainika kuwa zile timu zilipanga matokeo mpaka leo hajatolea ufafanuzi wowote, utashindwaje kuamini kuwa na yeye ni muhusika wa hilo jambo!!!!!
Unakumbuka kuwa issue kama hii ya kupanga matokeo iliwahi kutokea kule Nigeria lakini halikuchukua hata wiki kuzifungia zile timu ambazo zilipanga matokeo ili zipande daraja. Huyu Malinzi si mtu wa kukingiwa kifua hata kidogo.
 
Wadau wengi inaonekana mnamshambulia sana malinzi lakini ndo nyinyi mlimsifia sana Enzi zile anagombea Urais pale tifutifu. Tenga aliliona hili na ndo maana alijaribu kumzuia lakini wengi humu jf pamoja na vyombo vingi vya habari hasa clouds walimsifia sana malinzi. Mimi binafsi sikupenda kabisa malinzi awe presdaa wa soka letu. Kumbukeni Enzi akiwa sg pale yanga alileta nini? Wenye makosa ni sisi na tujilaum wenyewe maana tulimpa sifa asizo sitahili
 
alafu Jamal Malinzi anakiburi sana, kagoma kuja kujibu tuhuma zake hapa
 
Back
Top Bottom