Malimbikizo ya mishahara yatalipwa lini?

Hute

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,537
6,463
Mke wangu anadai hela nyingi tu hakulipwa mishahara miezi kadhaa, anadai huu mwaka wa sita. Anafanya kazi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali. Hivi ninyi serikali mtawapa lini malimbikizo yao au hamtawalipa kabisa?
 
mke wangu anadai hela nyingi tu hakulipwa mishahara miezi kadhaa, anadai huu mwaka wa sita. ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali. hivi ninyi serikali mtawapa lini malimbikizo yao au hamtawalipa kabisa?

Watalipwa makusanyo yakifikia trillion 3 kwa mwezi
 
mke wangu anadai hela nyingi tu hakulipwa mishahara miezi kadhaa, anadai huu mwaka wa sita. ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali. hivi ninyi serikali mtawapa lini malimbikizo yao au hamtawalipa kabisa?
Mwambie aandike barua gazetini... huko atashughurikiwa
 
Ni muhimu serkali ikafikiria kulipa na riba kwa sababu si haki kumlipa mtu milioni moja aliyokuwa akiidai miaka 6 iliyopita wakati kipindi hicho milioni moja ingetosha kununua kiwanja na leo kiwanja hichohicho kinauzwa milioni 10.
 
watakwambia mlizoea kupiga na pia muwaache wanyooshe nchi... na mumuombe mtukufu malaika mkuu aliyejuu ya yote
 
Daah kiukweli watumishi wa umma wanateseka sana ,kipindi hiki.
Sana, na wana jambo la kufanya.
Ni kupandikiza chuki haswaa kuelekea 2020.
Pia kukwamisha sifa zote wanazojidai nazo.
Haiwezekani watu wadai malimbikizo yao kwa Muda mrefu kiasi hiki ni dharau.
#tumehuruyauchaguzi#
 
lakini nafikiri 2020 haipo mbali. mbio zoote zile ilikuwa nguvu ya soda tu. mbona makusanyo hayaeleweki, watu hawatumii efd machines ili kukusanya kodi, machinga ambao wangekuwa maeneo maalumu walipe kodi wanatandaza kila sehemu biashara hazitambuliki, kiufupi sasaivi hakuna uhamasishaji wa kukuza uchumi, ni kama nchi ipo kwenye majaribio tu. tulifanya makosa makubwa sana ambayo tunatakiwa kujilaumu kwa miaka yote hii mitano kwakweli. never to repeat it again.
 
Mimi mwenyewe huu mwaka wa sita nadai,malimbikizo 1780000 tu,mpaka leo kimyaaaa! Halafu wanasema tufanye kazi kwa morali,itoke wapi?
 
Kumbe serikali ni mdaiwa sugu wa wananchi halafu kutwa loan board kupigia kelele vijana walipe deni, pathetic!
Serikali lipeni madeni ya watu ndio na nyie muwadai wadeni wenu!
 
kusema kweli toka moyoni, mojawapo ya vitu ninavyovichukia hapa duniani, ni serikali ya sisiemu, hata hii ya awamu ya tano. nasema bila unafiki kabisa.
 
Poleni sana mnaoidai serikali iliyopita. Hii iliyopo haidaiwi na yeyote kwani retired rcs., deds na dcs wote walilipwa mafao yao na waliiteuliwa walilipwa kila kitu hadi nauki na pesa ya kujikimu.
Ninyi wa awamu zile mkamdai mstaafu kwani ndiye ajuaye pesa zenu ziliko.
Na rejea kauli ya waziri wa Elimu miezi miwili iliyopita juu ya madeni ya likizo za walimu alivyojibu kuwa wizara haidaiwi ilihali hats walimu waliokwenda likizo desemba hii hawajalipwa nauli zao.
Nchi ya matabaka hii isiyosimama kwenye nguzo zake za kisheria.
 
Back
Top Bottom