Malimbikizo, vyeo na madai mbalimbali Julai

Malimbikizo, vyeo na madai mbalimbali Julai

nkisumuno

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2012
Posts
208
Reaction score
72
Nimeona kwenye taarifa TBC serikali imeahidi kumaliza kero za wafanyakazi mwezi Julai. Swali wanafanya hayo kwa ajili ya uchaguzi?

Sasa naamini serikali hii haina nia nzuri na watanzania. Maana ingekuwa na nia nzuri ingekuwa inalipa kwa wakati ili watanzania waendelee kupata huduma bora.

Basi kwa kutufanya wafanyakazi wajinga hiyo ni fursa nzuri kuonyesha hasira zetu kwa serikali kuwa sisi wafanyakazi tuna akili timamu.

Tafakari chukua hatua!
 
Badala ya elimu ya msingi na sekondari bure wangefanya elimu ya juu bure wangefanya la maana zaidi! Wasitupe danganya toto!
 
Serikali inataka kuwalaghai!!!! kwa nini wasilipe madai sasa hivi!!! watu wanafanya kazi mishahara inakata!!
 
serikali inataka kuwalaghai!!!! Kwa nini wasilipe madai sasa hivi!!! Watu wanafanya kazi mishahara inakata!!

kweli kabisa hii serikali inatuona kama wote hatuna akili, mimi niwaombe watanzania kwa ujumla tufike mahali tuseme imetosha kudanganywa walipe wasilipe wapigwe chini, utakuta sasa wanatandaza nguzo mara magreda barabarani wakati waliahidi kujenga barabara baada ya uchaguzi nguzo zinabaki hivyo na magreda yanarudishwa tuwakatae tu!
 
too much politics in administration will enevitably lead to evils!!!
 
Nani katoa tamko hilo? Kwanini walipwe july na sio january au february? Nia ya serikali ya ccm ni ipi zaidi ya kutoa haki za wananchi kama rushwa nyakati za uchaguzi? Yaani haki na stahiki ya mfanyakazi huumpi kwa wakati na ukimpa mnabadilishana na kura! This is too much. Haivumiliki hata kidogo na vyama vya wafanyakazi vianzie hapa kuitisha migomo na maandamano kupinga dhuluma hii ya wazi. Haviwezi, viache kuchukua michango ya wafanyakazi kwani nao wameshindwa kazi.
 
Nimeona kwenye taarifa TBC serikali imeahidi kumaliza kero za wafanyakazi mwezi Julai. Swali wanafanya hayo kwa ajili ya uchaguzi?

Sasa naamini serikali hii haina nia nzuri na watanzania. Maana ingekuwa na nia nzuri ingekuwa inalipa kwa wakati ili watanzania waendelee kupata huduma bora.

Basi kwa kutufanya wafanyakazi wajinga hiyo ni fursa nzuri kuonyesha hasira zetu kwa serikali kuwa sisi wafanyakazi tuna akili timamu.

Tafakari chukua hatua!
Ni kweli hata mimi nimewagundua wanafikiri sisi hatujui mimi nina madai yangu hatujalipwa hadi leo jamani niko kwenye cheo hichohicho miaka 5 sasa na hakuna dalili za kupandishwa, mwaka huu ni fursa nzuri kwetu kuchukua hatua.kuanzia Katiba hadi uchaguzi mkuu
 
ndio kawaida yetu, maneno mingiiiiii! afu utendaji, .............
 
Nani katoa tamko hilo? Kwanini walipwe july na sio january au february? Nia ya serikali ya ccm ni ipi zaidi ya kutoa haki za wananchi kama rushwa nyakati za uchaguzi? Yaani haki na stahiki ya mfanyakazi huumpi kwa wakati na ukimpa mnabadilishana na kura! This is too much. Haivumiliki hata kidogo na vyama vya wafanyakazi vianzie hapa kuitisha migomo na maandamano kupinga dhuluma hii ya wazi. Haviwezi, viache kuchukua michango ya wafanyakazi kwani nao wameshindwa kazi.
hata sisi wafanyakazi ni wajinga kama sio wapumbavu, kila siku tunachagua chama hicho cha watu wanaotudanganya, Hakuna kulalamika kwani ni ujinga wetu
 
Safari hii wafanyakazi tusiwe daraja la kuwabeba wanasiasa.Tufanye mbadiliko,tusidanganywe na ahadi za kutaka kura kisha wanatutelekeza.Tunataka haki zetu,na kura tutaamua tumpatie nani
 
Siyo serikali,ni kanjanja mmoja hivi ambaye ni Afisa utumishi halmashauri ya Iringa. Alikuwa anaongelea halmashauri yake.
 
Wanilipe tu ntashukuru ila kura yangu watasubiri sana yaani
 
Back
Top Bottom