Maliasili na utalii Kuna nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maliasili na utalii Kuna nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by gollocko, Apr 29, 2012.

 1. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,830
  Likes Received: 1,544
  Trophy Points: 280
  Hivi wanaJF hebu mnijuze, pale wizara ya maliasili na utalii kuna nini? Maana kila kiongozi anaeteuliwa huwa hafai na mwishowe huondoka kwa kashfa; kwa kuthibitisha hili hebu tujikimbushe hawa wafuatao:

  1. Zhakia Megji – Huyu alituhumiwa kwa kjimilikisha vitalu vya uwindaji isivyo halali
  2. Prof. Jumanne Maghembe – Yeye alituhumiwa kufanya mabadiliko makubwa ya wakurugenzi na makamishna pale wizarani kwa utashi wake pia alipandisha bei ya vitalu na wanyama isivyo kawaida.

  3. Antony Dialo na Saleh Pamba- Hawa walituhumiwa kwa kufanya biashara ya magogo nje ya nchi ilihali ikiwa imepigwa marufuku na serikali.
  4. Shamsa Mwangunga - Yeye na katibu wake Blandina Nyoni walikuwa hawaelewani kabisa kiasi cha kila mmoja kufanyia kazi za serikali nyumbani kisa ni Mwangunga kutuhumiwa kutorosha magogo nje ya nchi bila vibali.

  5. Ezekiel Maige- Huyu ndio balaa, licha ya kutuhumiwa kugawa vitalu kwa rushwa na kuwa na ukwasi wa kutisha bado katika kipindi chake wanyama wametoroshwa nje ya nchi huku yeye akijifanya hajui kinachoendelea.

  Hapa ndo najiuliza hapa maliasili na utalii kuna nini? Mbona kila anayepelekwa mambo huaribika?
   
 2. tembaisdor

  tembaisdor Member

  #2
  Apr 29, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  mkuu omba nawe nafasi ya uwaziri tuone utendaji wako. maliasili ndio kila kitu
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Usicheze na maliasili. Majaribu ya kila aina ya rushwa. napendekeza ateuliwe kisha apewe shehe mtopea tumpime ucha mungu wake uone kitakachotokea!
   
 4. T

  Tujumwiche Member

  #4
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hata kaa mtu hapo, interest za wakubwa ni nyingi. Bilieve me kama hujui mambo ya vitalu na magogo maana yake nini ni basi hapa ndipo utamu ulipo.
   
 5. T

  Tiger One JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 569
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Khamran & other temptations!!!
   
 6. M

  Moony JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Na wakurugenzi wao je?
  Nenda kurugenzi ya misitu, hata mataipisti wanamiliki NOAH
   
 7. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,830
  Likes Received: 1,544
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona wajibu kwa hasira? nauliza nipate kujua inakuwaje wote waboronge?
   
 8. i

  iMind JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,908
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Mweeee
   
 9. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #9
  Nov 13, 2014
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,830
  Likes Received: 1,544
  Trophy Points: 280
  W​adau Naombeni kuuliza, hapo wizara ya maliasili na utalii kulikoni! Toka kipindi cha awamu ya pili , hii wizara haishi kashfa. Kipindi cha Mwinyi ilikuwa ni kasfa ya Loliondo, kipindi cha Mkapa, yaliyomkuta Abubakar Mgumia na Zakia Megji hayakuwa madogo. Sasa ni kipindi cha Kikwete mambo ndo mabaya zaidi.

  Katika kipindi cha miaka sita (ikiwa nia wastani wa mwaka na miezi sita kwa kila waziri) ya Serikali ya Awamu ya Nne, Wizara hiyo imeongozwa na mawaziri sita mpaka sasa. Alianza Anthony Diallo, akaja Profesa Jumanne Magembe, Shamsa Mwangunga, Ezekiel Maige, na Balozi Khamis Kagasheki na sasa Ni Lazaro Nyalandu.

  Wote wale waliomtangulia Nyalandu hawakuondoka kwa mema. Diallo ni kashfa ya magogo ndio ilimwondoa, Magembe ni vitalu- hasa alipopandisha bei ya kuvipata, Shamsa ni vitalu na magendo kiasi cha kufikia yeye na katibu wake Blandina Nyoni kufanyia kazi mahotelini wakiogopana, Maige naye rushwa ya vitalu haikumbakiza, Kagasheki – kupambana kwake na ujangili ndio ikawa safari yake. Huyu Nyalandu nahisi ndio kama hajielewi vile, kila siku kashfa zinamuibukia huku yeye akiwa hajitengi nazo!

  Nyalandu toka aingie ni kiguu na njia kutangaza vivutio vyetu ingawa naona hata mafanikio hamna!

  Hapa naomba kuuliza wadu , hii wizara inaingizia taifa mapato kiasi gani kwa mwaka? Na kwa nini ni kama imeshindikana kutawalika? Hebu wataalam nijuzeni.
   
 10. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #10
  Nov 13, 2014
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,830
  Likes Received: 1,544
  Trophy Points: 280
  Hii wizara hakuna wanoijua?
   
 11. E

  Ezekiel Maige Verified User

  #11
  Nov 14, 2014
  Joined: Nov 10, 2013
  Messages: 11
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Ni Bahati Mbaya sana Watanzania wenzangu wengi mlizidiwa na upepo wa Lembeli ambaye sasa kidogo mmeanza kumjua. Wakati ule hamkunipa nafasi ya kunisikiliza. Mungefanya hivyo (kufanya utundu wa kutaka kujua "huyu bwana analalamika hajapata nafasi ya kusema, angepewa nafasi angesemaje?". Kwa kifupi sana, kwenye suala langu, RUSHWA SI KWAMBA MIMI NDIYE NILIPOKEA BALI WALIOKUWA WAKINISAKAMA NDIO WALIOPOKEA WAFANYE WALICHOKIFANYA. Nilisema kuna Mfanyabiashara mmoja aliwafanyia semina na kuwapa posho nono St Gasper Dodoma tar 16/4/2012. Mungejitahidi kufuatilia hiyo tip ingewasaidia sana kutenda haki.

  Kwa kuwa na mhimuko na ushabiki, mnajinyima nafasi ya kujua ukweli na hivyo kuishia usemi "UMDANIAYE NDIYE KUMBE SIYE".

  Naweza kuthibitisha hivi sasa lobying zinazofanywa (kwa wabunge) na wafanyabiadhara wanaoathirika na maamuzi ya watendaji serikalini ndiyo zinayumbisha na kuchafua Bunge. Anayejidanganya wabunge ni Mashekhe au Maaskofu (kwamba ni wasafi kihivyo) na hivyo kuamini kila wanachokisema basi pole zake.

  Rushwa WORKED AGAINST ME. Ningekuwa nimepokea rushwa na kufanya maamuzi yasiyo sahihi yangetokea yafuatayo:-

  1. Leo ningekuwa Mahakamani kama Idd Simba au Ekerege, na
  2. Maamuzi jiliyofanya yangekuwa yameshabatilishwa.

  Chunguzeni kwa nini hayo mawili hayajatokea.

  wanaJF hebu mnijuze, pale wizara ya maliasili na utalii kuna nini? Maana kila kiongozi anaeteuliwa huwa hafai na mwishowe huondoka kwa kashfa; kwa kuthibitisha hili hebu tujikimbushe hawa wafuatao:[/COLOR][/FONT][/SIZE]

  1. Zhakia Megji – Huyu alituhumiwa kwa kjimilikisha vitalu vya uwindaji isivyo halali
  2. Prof. Jumanne Maghembe – Yeye alituhumiwa kufanya mabadiliko makubwa ya wakurugenzi na makamishna pale wizarani kwa utashi wake pia alipandisha bei ya vitalu na wanyama isivyo kawaida.

  3. Antony Dialo na Saleh Pamba- Hawa walituhumiwa kwa kufanya biashara ya magogo nje ya nchi ilihali ikiwa imepigwa marufuku na serikali.
  4. Shamsa Mwangunga - Yeye na katibu wake Blandina Nyoni walikuwa hawaelewani kabisa kiasi cha kila mmoja kufanyia kazi za serikali nyumbani kisa ni Mwangunga kutuhumiwa kutorosha magogo nje ya nchi bila vibali.

  5. Ezekiel Maige- Huyu ndio balaa, licha ya kutuhumiwa kugawa vitalu kwa rushwa na kuwa na ukwasi wa kutisha bado katika kipindi chake wanyama wametoroshwa nje ya nchi huku yeye akijifanya hajui kinachoendelea.

  Hapa ndo najiuliza hapa maliasili na utalii kuna nini? Mbona kila anayepelekwa mambo huaribika?[/QUOTE]
   
 12. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #12
  Nov 14, 2014
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,830
  Likes Received: 1,544
  Trophy Points: 280
  [/QUOTE]

  Maige huu sasa ndio wakati wako wa kutupa hizo evidence za hapo maliasili ili tujue ni nini kinaendelea, Ni kweri siku hizi Lembeli ni mpole sana kwa Nyalandu, naona ni maswahiba sana. Na ripoti ya meno ya tembo naona wameikalia na hawataki kuitoa. Hebu waungwana tusaidieni maana naona kuna vita ya kufa mtu hapo wizarani, Nyalandu na Lembeli na katibu mkuu na watendaji wake!
   
Loading...