Mali za viongozi 141 zahakikiwa

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
[h=2][/h]


Na Richard Makore



9th May 2o12













Viongozi wa umma 141 wamehakikiwa mali zao ili kubaini kama kulikuwa na udanganyifu wakati wakijaza fomu za mali wanazomiliki pamoja na madeni yao.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Afisa Habari wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Johanither Barongo.
“Mwaka jana tulikuwa na zoezi la kuhakiki mali za viongozi wa umma na tumefanya kazi hiyo kwa kanda sita,” alisema Barongo.
Alisema zoezi hilo lilikwenda vizuri na kwamba muda wowote watatoa kwa umma ripoti ya uhakiki huo.
Hata hivyo, Barongo hakutaka kuingia kwa undani juu ya matokea ya zoezi hilo na kusema kuwa kila kitu kitawekwa wazi kwa umma baada ya ripoti ya pamoja kukamilika.
Alifafanua kuwa katika zoezi hilo sio viongozi wote wa umma waliohakikiwa, bali walichagua baadhi na kwamba hawakupata kikwazo chochote wakati wa zoezi hilo.
“Hatukupata kikwazo, tulipata ushirikiano wa kutosha katika maeneo yote tuliyopita na watu wote tuliozungumza nao,’’ alisema.





CHANZO: NIPASHE


0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni




<a href='http://www.ripoti.com/openx/www/delivery/ck.php?n=a5793a20&cb=INSERT_RANDOM_NUMBER_HERE' target='_blank'><img src='http://www.ripoti.com/openx/www/delivery/avw.php?zoneid=267&cb=INSERT_RANDOM_NUMBER_HERE&n=a5793a20' border='0' alt='' /></a>









Habari Zaidi

[h=3]Articles[/h]Mawaziri watema cheche


Ripoti sakata la Blandina Nyoni yatua kwa JK


Waliofukuzwa watofautiana, wengine `bubu`


Mbowe akosoa uteuzi wa mawaziri


Aachwa na mume kwa kuzaa watoto wa ajabu
 
Huu ni ubabaishaji tu ,kubabaishwa Watanzania ili vigogo wapate nafuu, hii tume ya umadili ya viongozi kuchunguwa mali zao ni FAKE na haina Tafauti na Tume yetu ya taifa NEC, niwenyewe kwa wenyewe tu kiswahili chao kimoja baina ya vigogo na hio tume wote wana ccm na matapeli.

Ikiwa kweli tunataka kujuwa ukweli wa mali za vigogo basi tume ya uchunguzi wa hesabu ya Mh Zitto Kambwe ipewe fursa hio ndio hapo Watanzania tutakuwa na imani sio tume hii ya ubabaishaji.
 
Back
Top Bottom