Mali za Said Lugumi zakamatwa na TRA kwa kudaiwa Kodi ya Sh. Bilioni 14

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
55,242
77,558
Umofia Kwenu Wana JF,

Kampuni ya Yono Kupitia TRA yamekamata majumba matatu ya Lugumi yaliyoko Ndege Beach Mbweni kwa kudaiwa kodi ya zaidi ya Bilioni 14.

Nawasilisha kutoka MINJINGU.

=======

Kampuni ya udalali ya Yono, imefanikiwa kukamata mali za wafanyabiashara wanaodaiwa kodi ya serikali inayofikia zaidi ya Sh bilioni 68.1. Operesheni ya kukamata mali hizo kwenye maeneo mbalimbali ndani na nje ya Jiji la Dar es Salaam imefanywa ndani ya wiki moja.

Katika operesheni hizo maofisa wa Yono wamekuwa wakishirikiana na maofisa wa Mamlaka ya Mapato(TRA), ambayo ndiyo imeipa kampuni hiyo kazi ya kukusanya kodi kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yono, Scholastica Kevela, Yono imepewa kazi na TRA kukusanya madeni yake ya kodi kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Pwani Njombe, Mbeya, Iringa na Zanzibar.

Aliwataka watanzania kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli za kuleta maendeleo kwa kulipa kodi bila shuruti ili zipatikane fedha za kujenga miundombinu kama barabara, reli, shule, madaraja, hospitali na zahanati.

Kuhusu taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba hata baadhi ya mali za Kampuni ya Lugumi zimeshikiliwa, Mkurugenzi huyo alithibitisha kuwa habari hizo ni za kweli ambapo wanashikilia nyumba za kifahari za mfanyabiashara huyo.

“Mmeniuliza kwamba mmesikia nyumba za Lugumi zimefungiwa ni kweli, amefungiwa nyumba zake za kifahari na anadaiwa Sh bilioni 14, yupo mtu anaitwa Gm Dewji naye anadaiwa Sh bilioni 1.8, Kampuni ya ujenzi ya Mutluhan Construction anadaiwa Sh bilioni 45,”alisema.

Alisema wanaodaiwa wanapaswa kulipa madeni yao TRA ndani ya siku 14 na kwamba muda huo ukipita watapewa maelekezo na serikali kama ni kuuza mali hizo ili kufidia madeni yao.

Ofisa Mwandamizi wa TRA, ambaye hakupenda jina lake litajwe alithibitisha kwamba nyumba ya Lugumi iliyoko Upanga mtaa wa Mazengo inashikiliwa na mamlaka hiyo na ghorofa la kifahari lililoko Mbweni JKT, Dar es Salaam.

“Hakuna siri maana mkienda kwenye hizo nyumba mtakuta alama ambazo huwa Yono wanaweka kwa nyumba inayoshikiliwa, nendeni Upanga na kule Mbweni JKT mtakuta hizo nyumba tunazoshikilia,” alisema


Chanzo: HabariLeo
 
Untouchable Said Lugumi
Hapo Serikali Ya Viwanda Ipunguze Maigizo Tumeshachoka Hilo Ni Kaburi Litamzika Mfukuaji Soon. Hapo Ukimwaga Sumu Ujue Umeiua Ccm Na Viongozi Wake Wote.

Wanadamu hatuna jema. Ni humu humu JF tumemkosoa Mkulu kwa kutowachukulia hatua akina Lugumi. Now, the man is trying and here we come....eti ni maigizo.

Aise mtu akikuchukia hata ufanye nini wallah! Mbele yake utakuwa ni ziro tuu.
 
Habari wadau!
Nimesoma vichwa vya habari kwenye magazeti kuwa mali za Lugunm zakamatwa akidaiwa kodi ya zaidi ya bil 14 na TRA.

Mie naona tunapiga sarakasi huku tukiwa tumevaa taulo.

Nijuavyo mimi anapoomba tenda kaiwaida lazima awe na tax clearence toka TRA ndo upewe tenda kuashiria hudaiwi kodi ili usije tumie pesa ya mradi kulupia madeni hasa kodi na tozo mbalimbali.

Iweje leo ndani ya miaka 3 awe anadaiwa zaidi ya bilioni 14 kwa biashara ipi anayofanya huyu Lugumi.

Kumshitaki kwa kosa la ufidlsadi inaonekana kuna watu serikalini wataguswa hasa toka chama kileeee. Ili ionekane anakufa nayo kama Lugumi wamekuja na njia nyingine kuwapumbaza wananchi

Hili jipu naona liko kwenye paji la uso inamaana mtumbuaji halioni? Au kwakuwa ni kampuni toka kanda maalum
 
Binadamu hatuna jema jamani. Ni humu humu JF tumeshikia bango JPM kwa kuwaogopa akina Lugumi na wenzake. Leo hii serikali inachukua hatua...kudai kodi.....wengine tunasema ni maigizo. Kiukweli sijui waTanganyika tunataka nini.

Hivi kweli TRA ni wajinga wakakamate mali zake bila sababu? kwamba hawajampelekea notice ya kulipa? Tunasahau kwamba hata hizo hela zenyewe zimetoka serikalini. Mara kibao tumeambiwa miradi fake fake ambayo Lugumi amedeal nayo..ni humu humu JF tumelia na ufisadi wa Lugumi kuliko ufisadi mwingine. Leo serikali inamdai tunasema ni maigizo? sasa tunataka hiyo serikali ifanye nini haswa? We need Governement of Jesus aiseeeee....

By the way hapa watakuja wenzangu watasema..ooohh..mbona hajakamata IPTL..MEREMETA..NK. Lakini ukweli ni kwamba huwezi peleka kila mtu mahakamani....kuna stages.....ukifanya hivyo..serikali most likely itashindwa hizo kesi....na ikishindwa tutakuja hapa hapa kusema kwamba wanasheria wa serikali walikula rushwa au ni fake! Ilmradi tuna sababu ya kuwaponda...

Of course, kama nilivyosema kwingineko mtu akikuchukia cannot see anything positive from you. Na hii ndo Changamoto ya critics wengi wa JPM. Hata angefanya nini..they will never see anything good of this Man from Chato!

JPM ana mapungufu mengi kama Kiongozi na kama binadamu. Lakini tujitahidi kuona hata yale mazuri kidogo anayoyafanya. Otherwise..tutakuwa tunalalamika tuu for the next ten years! and at the end of the day...we will have achieved one thing only. NOTHING!

Natamani JPM afanye improvement kwenye uongozi wake-and he should. Lakini kuwa critic kwa kila kitu anachofanya haisaidii kabisa.
 
Kwann usiende mahakamani kuweka zuio la mali zake iwapo hayo unayosema ni kweli? Make hata kwenye ubunge tumeona mwananchi akaenda mahakamani kupinga ubunge mfano ule wa Lema na yule mama Buriani.
 
Hivi hapa suala kuu na la msingi ni kutolipa kodi au ufisadi wa Lugumi kujipatia pesa bila ya kufanya kazi au kutoa huduma aliyotakiwa kuitoa kwa malipo aliyolipwa??? Naona tunapotezewa focus hapa. Tunaweza kudaiwa na TRA ss watanzania lakini kupiga dili ya mabilioni kama Lugumi ni wachache sana wenye connection na sirikali. Suala la msingi liwekwe mezani tena na ufumbuzi upatikane.
Huyu jamaa yupo kweli bongo!?? Nahisi alishapewa escort hadi Airport
 
Huyu Lugumi alipewa hii tenda kama zawadi; hakuwa na vigezo vya kupewa hii tenda kubwa na nyeti kwa mustakali wa usalama wa Taifa. Kwa mtaji huo, Lugumi atakuwa na Mali yenye gharama ya b 14 ukizingatia fedha za tenda waligawana wengi? Bado naona hatua ya TRA in maigizo matupu.
 
Hii Lugumi inamhusu pia Mkuu 1 hivi aliyekuwa balazi wetu China ( sijui kama bado yupo) alipitisha hadi tenda hewa za jeshi.
 
Hivi hapa suala kuu na la msingi ni kutolipa kodi au ufisadi wa Lugumi kujipatia pesa bila ya kufanya kazi au kutoa huduma aliyotakiwa kuitoa kwa malipo aliyolipwa??? Naona tunapotezewa focus hapa. Tunaweza kudaiwa na TRA ss watanzania lakini kupiga dili ya mabilioni kama Lugumi ni wachache sana wenye connection na sirikali. Suala la msingi liwekwe mezani tena na ufumbuzi upatikane.
Huyu jamaa yupo kweli bongo!?? Nahisi alishapewa escort hadi Airport

Huu ndio ukweli
 
Wanadamu hatuna jema. Ni humu humu JF tumemkosoa Mkulu kwa kutowachukulia hatua akina Lugumi. Now, the man is trying and here we come....eti ni maigizo.

Aise mtu akikuchukia hata ufanye nini wallah! Mbele yake utakuwa ni ziro tuu.
Kazi ya hapo ni kuamisha goli!
 
Ivi kweli TRA wanakuaga wapi mtu anadaiwa Kodi halipi inafika bilioni ya kwanza ya pili ya tatu nne mpaka zinafika 45 Wao wapo tuu wanaangalia au malengo yao Ni kuona watu wanafilisika maana sio rahisi iyo kampun kwa Sasa kulipa iyo 45b itakufa tuu yawezekana hata hawana mtaji Wa hivo TRA waache uzembe
 
Wanadamu hatuna jema. Ni humu humu JF tumemkosoa Mkulu kwa kutowachukulia hatua akina Lugumi. Now, the man is trying and here we come....eti ni maigizo. Aise mtu akikuchukia hata ufanye nini wallah! Mbele yake utakuwa ni ziro tuu.
Kabisa aise ni kama huyu mdau naye "Namchukia magufuli from bottom of my heart" Namchukia magufuli from bottom of my heart, sasa ebu nieleweshe unamchukia mtu bila sababu ili iweje, kwanini usitumie mitandao ya jamii kama yakina Mange Kimambi kukosoa na kutoa ushauri wajirekebishe?! Sababu wanasoma huko, watasikia tu...watabadilika..
 
Back
Top Bottom