Mali za Said Lugumi zakamatwa na TRA kwa kudaiwa Kodi ya Sh. Bilioni 14

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,137
2,000
Mkuu, Kwani hapo ndipo kashfa ya Lugumi imeshughulikiwa? kwani kashfa ilikuw ani kutolipa kodi??? hii kwanza wengine ndo tunaisikia leo.
Ameanzwa kushughulikiwa from all angles, vertically, perpendicularly, diagonally, side to side, head to toes and so forth.

Sasa wewe ulitaka waanzie wapi. Tumeanza kwa kumfilisi kwanza kupitia TRA immediately na mengine yatafuata baadaye akiwa tayari hoi bin tabani. Kesi yake ya ku supply electronic devices kwenye jeshi la polisi itakapofika mahakamani hatakuwa na nguvu ya fedha ya kuvuruga kesi hiyo kama ambavyo mafisadi wengi hufanya. So we started with the right step.
 

mharakati

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,273
1,225
Habari wadau!
Nimesoma vichwa vya habari kwenye magazeti kuwa mali za Lugunm zakamatwa akidaiwa kodi ya zaidi ya bil 14 na TRA.

Mie naona tunapiga sarakasi huku tukiwa tumevaa taulo.

Nijuavyo mimi anapoomba tenda kaiwaida lazima awe na tax clearence toka TRA ndo upewe tenda kuashiria hudaiwi kodi ili usije tumie pesa ya mradi kulupia madeni hasa kodi na tozo mbalimbali.

Iweje leo ndani ya miaka 3 awe anadaiwa zaidi ya bilioni 14 kwa biashara ipi anayofanya huyu Lugumi.

Kumshitaki kwa kosa la ufidlsadi inaonekana kuna watu serikalini wataguswa hasa toka chama kileeee. Ili ionekane anakufa nayo kama Lugumi wamekuja na njia nyingine kuwapumbaza wananchi

Hili jipu naona liko kwenye paji la uso inamaana mtumbuaji halioni? Au kwakuwa ni kampuni toka kanda maalum

Hata nchi zilizoendelea kodi utumika kama fimbo ya mwisho ya kuwanasa wahalifu au maadui wa sera na serikali wowote wanaonekana watakua wagumu Kuwatia hatiani na kesi nyingine yeyote.
Kitu muhimu ni kuchukua Mali zilizopatikana kwa wizi wa Mali ya umma kwa kudai kodi. Wateme walichotuibia na hii itafundisha walafi wengine kutumika na wanasiasa kutuibia
 

mharakati

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,273
1,225
Watanzania tunataka suala la kulipwa mabilioni bila kufanya Kazi sio TRA kumdai kodi

Akienda mahakamani na kesi ikaendeshwa akashinda kwa sababu kesi za vifaa vya kiusalama zinaweza kua limited kwa sababu ya sensitive info. Tutasemaje? Si bora afilisiwe liwe fundisho kwa wezi wengine wanaotuibia kupitia tenderprenuership na wanasiasa wao...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom