Mali za Marehemu Bilionea Erasto Msuya, ndugu ngumi mkononi

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
757
Reaction score
1,822
Mgogoro wa Muda mrefu uliokuwa ukifukuta baina ya familia za Marehemu bilionea Erasto Msuya wa kugombea Mali umechukua sura mpya mara baada ya Serikali ya Mkoa kuingilia kati kwa lengo la kupata suluhu ya kudumu nje ya Mahakama.

Mgogoro huo ambao umedumu kwa takribani miaka 7 tangia kifo cha Marehemu mwaka 2013, upande wa wazazi wa marehemu Erasto Msuya unadai kwamba Mke wa marehemu amekuwa akiuza mali kinyume na utaratibu .

Upande wa Mke wa marehemu Erasto aitwaye Miriam Erasto ambaye kwa sasa yupo mahabusu Gerezani kwa tuhuma ya mauaji ya wifi yake. Mtoto mkubwa wa marehemu aitwaye Kelvin Erasto anadai wazazi wa marehemu baba yake wanataka kumpokonya mali.

Akiongea na familia hizo katika nyumba aliyokuwa akiishi Marehemu Erasto iliyopo Kwa Iddy wilayani Arumeru,Mkuu wa wilaya hiyo Jerry Muro amewataka watoto wa marehemu waliokuwa wameikimbia nyumba ya marehemu baba yao wakihofia kuuawa kurejea katika nyumba hiyo kuanzia leo wakati wakiendelea na utatuzi wa mtafaruku uliopo.

Aidha Muro amezitaka pande hizo mbili kufika ofisini kwake siku ya Jumatatu saa 4 asubuhi wakiwa wameambatana na vielelezo mbalimbali ili kufikia mwafaka wa mgogoro huo nje ya Mahakama.

"Si nia ya Serikali kuingilia jambo lililopo Mahakamani ila kama Serikali tuna mamlaka ya kusuluhisha jambo iwapo pande zote zipi tayari kuketi kwani suala la kutafuta mshindi mahakamani si suluhu ya kuleta amani" Amesema Muro

Akiongea mgogoro huo mtoto mkubwa wa marehemu , aitwaye Kelvin Erasto alimweleza mkuu huyo wa Wilaya kuwa wazazi wa marehemu baba yake( bibi) aitwaye Ndeshu Msuya na babu yake aitwaye Elisaria Elia Msuya pamoja na shangazi zake wanataka kumpokonya Mali za Marehemu baba yake .

Akijibu tuhuma hizo,Mama wa marehemu Erasto,Ndeshu Msuya amesema kuwa wao kama wazazi wa marehemu Erasto hawana nia ya kutaka urithi wa mali yoyote ya marehemu mtoto wao ila wanasikia uchungu kuona Mke wa Erasto akiuza Mali ovyo za Marehemu mtoto wao ili kumaliza suala la kesi ya mauaji inayomhusu wakati ugawanyo wa Mali bado haujafikiwa.

Mama huyo amedai kuhofika watoto wa marehemu kupoteza rasilimali hizo kutokana na Mali hizo ndugu wa Mke kujimilikisha ambao wamejipa kipaumbele kusimamia jambo ambalo linawapa mashaka kwamba huenda watoto hao wakadhulumiwa.

Naye baba wa marehemu aitwaye Elisaria Msuya amesema madai yanayotolewa kuwa amejimilikisha mgodi wa marehemu Erasto hayana msingi wowote kwani wakati anamzaa Erasto alikuwa anamiliki migodi huko Mererani na ubilionea wa Msuya umetokana na yeye kumpa mgodi wa kuchimba madini ya Tanzanite.

Marehemu Erasto alifariki agosti,7mwaka 2013 kwa kupigwa risasi zaidi ya 20 eneo la Mijohoroni,wilaya ya Hai ,mkoani Kilimanjaro na watu ambao baadae walikamatwa na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela Mara baada ya Mahakama kuwatia hatiani.

Ends.....

IMG_20191017_131917.jpeg
IMG_20191017_131205.jpeg
IMG_20191017_131230.jpeg
 
Hii familia mauzauza tupu,huyo mtoto anajazwa ujinga na ndgu wa mama yake ambao ndio wanasimamia mali hizo utafikiria hata wanajua zimetoka wapi.erasto hakuwahi kumiliki mgodi yote ni mali ya mzee kikaango kazaliwa kamkuta baba yake anamiliki hivyo vitalu
 
Nakukubali sana Kwenye Issues zinazohusu hii Familia.
 
Nilitaka kukutag mkuu...sector yako hii.
Hii familia mauzauza tupu,huyo mtoto anajazwa ujinga na ndgu wa mama yake ambao ndio wanasimamia mali hizo utafikiria hata wanajua zimetoka wapi.erasto hakuwahi kumiliki mgodi yote ni mali ya mzee kikaango kazaliwa kamkuta baba yake anamiliki hivyo vitalu
 
Hii familia mauzauza tupu,huyo mtoto anajazwa ujinga na ndgu wa mama yake ambao ndio wanasimamia mali hizo utafikiria hata wanajua zimetoka wapi.erasto hakuwahi kumiliki mgodi yote ni mali ya mzee kikaango kazaliwa kamkuta baba yake anamiliki hivyo vitalu
Erasto hakuacha wosia?
 
Mgogoro wa Muda mrefu uliokuwa ukifukuta baina ya familia za Marehemu bilionea Erasto Msuya wa kugombea Mali umechukua sura mpya mara baada ya Serikali ya Mkoa kuingilia kati kwa lengo la kupata suluhu ya kudumu nje ya Mahakama.

Mgogoro huo ambao umedumu kwa takribani miaka 7 tangia kifo cha Marehemu mwaka 2013, upande wa wazazi wa marehemu Erasto Msuya unadai kwamba Mke wa marehemu amekuwa akiuza mali kinyume na utaratibu .

Upande wa Mke wa marehemu Erasto aitwaye Miriam Erasto ambaye kwa sasa yupo mahabusu Gerezani kwa tuhuma ya mauaji ya wifi yake. Mtoto mkubwa wa marehemu aitwaye Kelvin Erasto anadai wazazi wa marehemu baba yake wanataka kumpokonya mali.

Akiongea na familia hizo katika nyumba aliyokuwa akiishi Marehemu Erasto iliyopo Kwa Iddy wilayani Arumeru,Mkuu wa wilaya hiyo Jerry Muro amewataka watoto wa marehemu waliokuwa wameikimbia nyumba ya marehemu baba yao wakihofia kuuawa kurejea katika nyumba hiyo kuanzia leo wakati wakiendelea na utatuzi wa mtafaruku uliopo.

Aidha Muro amezitaka pande hizo mbili kufika ofisini kwake siku ya Jumatatu saa 4 asubuhi wakiwa wameambatana na vielelezo mbalimbali ili kufikia mwafaka wa mgogoro huo nje ya Mahakama.

"Si nia ya Serikali kuingilia jambo lililopo Mahakamani ila kama Serikali tuna mamlaka ya kusuluhisha jambo iwapo pande zote zipi tayari kuketi kwani suala la kutafuta mshindi mahakamani si suluhu ya kuleta amani" Amesema Muro

Akiongea mgogoro huo mtoto mkubwa wa marehemu , aitwaye Kelvin Erasto alimweleza mkuu huyo wa Wilaya kuwa wazazi wa marehemu baba yake( bibi) aitwaye Ndeshu Msuya na babu yake aitwaye Elisaria Elia Msuya pamoja na shangazi zake wanataka kumpokonya Mali za Marehemu baba yake .

Akijibu tuhuma hizo,Mama wa marehemu Erasto,Ndeshu Msuya amesema kuwa wao kama wazazi wa marehemu Erasto hawana nia ya kutaka urithi wa mali yoyote ya marehemu mtoto wao ila wanasikia uchungu kuona Mke wa Erasto akiuza Mali ovyo za Marehemu mtoto wao ili kumaliza suala la kesi ya mauaji inayomhusu wakati ugawanyo wa Mali bado haujafikiwa.

Mama huyo amedai kuhofika watoto wa marehemu kupoteza rasilimali hizo kutokana na Mali hizo ndugu wa Mke kujimilikisha ambao wamejipa kipaumbele kusimamia jambo ambalo linawapa mashaka kwamba huenda watoto hao wakadhulumiwa.

Naye baba wa marehemu aitwaye Elisaria Msuya amesema madai yanayotolewa kuwa amejimilikisha mgodi wa marehemu Erasto hayana msingi wowote kwani wakati anamzaa Erasto alikuwa anamiliki migodi huko Mererani na ubilionea wa Msuya umetokana na yeye kumpa mgodi wa kuchimba madini ya Tanzanite.

Marehemu Erasto alifariki agosti,7mwaka 2013 kwa kupigwa risasi zaidi ya 20 eneo la Mijohoroni,wilaya ya Hai ,mkoani Kilimanjaro na watu ambao baadae walikamatwa na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela Mara baada ya Mahakama kuwatia hatiani.

Ends.....

View attachment 1236195View attachment 1236196View attachment 1236197
Nilivyosona Serikali imeingilia nikawa na uhakika wa kinachoendelea, kumbe ni Jerry Muro!!!
 
Back
Top Bottom