Heshima kwenu wanajamvi wote.
Naomba maoni yenu kuhusu malezi ya aina hii. Mke wangu ananitia mashaka kwa jinsi anavyowatreat wanangu wawili ambao ni wake pia, matunda ya ndoa yetu. Hana simile, hana upole. Mtoto akikosea yeye ni kufoka, kutukana na kupiga tu. Hana muda wa kuongea na watoto kwa upole na subira wanapokosea. Nikijaribu kumshauri awe na subira, si kufoka na kupiga tu, kukaa nao na kuwaelewesha kwa upole mambo ya nidhamu itasaidia, hunipinga na kusema mimi sijui kulea. (Yeye ana watoto wawili aliozaa na baba mwingine kabla sijamuoa). Nimekuwa nikiwakaripia watoto na kuwachapa kutegemea na ukubwa wa kosa lakini pia huwa naongea na watoto mbele yake kumpa mfano lakini wala hafati. Kwa malezi haya ya mke wangu ya namna hii naweza kupata watoto wenye balanced behaviour kweli? Au ni mimi nakosea? Nini faida au hasara za malezi ya aina hii?
NAWASILISHA!