malezi ya watoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

malezi ya watoto

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by gfsonwin, Apr 15, 2012.

 1. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Hodi wana jf nakuja kwenu kwa mara ya kwanza nikiwa nimetingwa na lillonisibu mchana huu juu ya malezi ya wanetu.
  naomba mnisaidie majibu hasa ya kunielewesha manake kama shule basi basi nimeshafeli.

  niko nyumbani hapa na wanangu wawili mmoja ana miaka 6 na mwingine miaka 3 wote ni wa kiume. sasa walikuwa wanacheza na toys hapa, huyu mkubwa akawa anamsumbua mdogo wake mara kwa kumtuma tuma. mara amwambie chukua gari hili weka hapa mara leta treni ieke hapa, mara leta ufagio mimi kama mama nikakwazika. ndipo nilipomwambia mwanangu mkubwa usimchoshe mwanangu. nakiri kwamba nilisema maneno haya kwa lugha ya ukali kidogo napia huyu mdogo hakuwa amechukia japo ndiye aliyekuwa anatumwa.

  sikujua kama kaka mtu kakasirika kwa maneno niliyo mwambia ghafla alikaa kimya na mimi sikumzingatia, ndipo aliponiuliza hivi mama kwani mimi siyo mwanao? nikashtuka nikamjibu ni wanangu tena mkubwa akasema kwanini sasa unasema nisimchoshe mwanao? inamaana wewe unampendelea tu HUYO MWANAO KULIKO mimi.

  jamani nimeumizwa sana na haya maneno. hebu nisaidieni wana jf na wajuzi wa malezi, nataka niwalee wote kwa usawa. kwani wote nime wazaa mimi na kwa baba mmoja.
   
 2. N

  NZURI PESA JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 4,034
  Likes Received: 1,246
  Trophy Points: 280
  Ninapenda kukuelimisha kuhusu malezi sahihi ila ningependa kujua km wewe ni mfanyakaz au mama wa nyumbani ili nikupe vitu kulingana na nafasi yako
   
Loading...