Malezi ya manyanyaso yanavyoathiri watoto ki saikolojia.

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,720
215,778
Happy New Year wapendwa

Jana nilipata bahati ya kutoka kwetu Kwamtogole, nilialikwa Masaki kwenye New Year's Bash. Acheni kodi ya Masaki iwe juu, kule hata jirani akikaanga samaki si rahisi kufahamu, huku kwetu wale wa mboga saba wote tunawafahamu.

Nilipata shost mpya jana kwenye party, ni mdada wa ki-Tanzania anaeishi bondeni yaani South Africa, khee mwenyewe nilivyokuwa nimevunja kabati na pair yangu mpya ya clarks, kumkuta shost amepiga Louis Vuitton kuanzia viatu na handbag, nilijifanya kama kwangu ya kawaida, lakini aliposema "Sky I like your shoes" nikaona huku sasa kuchorana.

Shost anaitwa Rose, ingawa hakutaka nijue yeye ni kabila gani lakini hana mapenzi na Tanzania kabisa. Story ya Rose ni kuwa mama yake alipata ujauzito wake akiwa mwanafunzi, familia nzima ilimsakama mama kwa kutoendelea na shule akiwa kidato cha kwanza. Mama Rose alimlea mtoto wake akiwa kwa wazazi wake, mtoto alipofikisha miaka miwili, binamu anaeishi S/A alileta habari kuwa kuna kazi imepatikana mama Rose aende, si unajua wengi tunavyochangamkia mchongo wa kutoka nje ya nchi.

Rose aliachwa kwa mama mkubwa akiwa na umri wa miaka miwili kama alivyohadithiwa, mama mkubwa alikuwa na watoto nane kati ya hao sita wa kiume. Katika makuzi Rose alitambua kuwa yeye ni tofauti na wenzake, hakuwa anajaliwa sana, hata uniform zake zilikuwa mchoko kiaina. Mama mkubwa hakuwa na mapenzi na Rose, watoto wa kiume wa mama mkubwa walimfanya Rose kama jaribio la ngono, alilala na wanne kati yao, hii kwake yeye alifikiri ni njia itakayomfanya akubalike ndani ya nyumba.

Rose akiwa na umri wa miaka kumi na sita alipata ujauzito hata mwenyewe hafahamu kuwa ulikuwa wa nani kati ya wale vijana wanne wa mama mkubwa. Mama mkubwa alimpeleka hospitali na mimba ile ilitolewa.

Kule S/A mama Rose hakuweza kutoka nje ya nchi kwa kukosa vibali, baada ya mahangaiko ya muda mrefu alikutana na mwanaume wa Kizulu ambae alifunga nae ndoa na kumwezesha kupata vibali vya kuishi ki halali. Hii ilikuwa baada ya miaka 16 tangia ameondoka Tanzania, mama alipopata vibali tu, kitu cha kwanza alichofanya ni kurudi Tanzania na kumchukua Rose. Rose aliondoka na mama yake na kwenda kuendelea na masomo S/A. Rose akiwa mwanafunzi wa chuo kikuu mama yake aligundulika na cancer, miaka miwili baadae mama alifariki dunia.

Rose alimaliza shule na kukutana na kijana Robert ambae ni mixed race, baba yake Robert ni mzungu. Robert hakuwahi kumfahamu mama yake, lakini baadae aligundua kuwa alikuwa analelewa na mfanyakazi wa baba yake. Kutokana na siasa za ubaguzi wa rangi, baba yake Robert hakuweza kuwaambia ndugu jamaa na marafiki zake kuwa alizaa na mwanamke mweusi, hivyo alimuomba mpishi wake amlee Robert kama mtoto wake.

Robert hakukua kwa raha katika familia ile, kulikuwa na watoto wa kiume wakubwa wa baba yule ambao walimpa Robert kila aina ya mateso mengi Robert hapendi hata kuyaeleza. Mara moja kwa mwaka baba Robert aligharamia safari ya Robert na mama au baba wa ile familia kwenda Botswana, kule aliweza kupata muda wa kuwa karibu na Robert, walicheza kwenye mabembea, walikula pamoja migahawani na alimhusia sana Robert kupenda shule.

Robert akiwa kijana wa miaka 21 aligundua baba yake alimwachia mali nyingi, na hii ndiyo ilikuwa sababu ya chuki walioionyeshea watoto wa mpishi kwa Robert. Robert aliendelea na shule, pesa aliyopewa ilimsaidia kafanikikisha ndoto zake.

Rose na Robert wote wawili wameamua kutozaa watoto, kutokana na mateso waliyopitia kwenye maisha, wote hawataki kuleta kiumbe duniani ambacho kitateseka kama wao walivyoteseka. Rose alifanyiwa operation ya kutoa kizazi.
 
Rose kafanya kitu cha kijinga mnoo, wangezaa na wakawapa mapenzi ya kutosha watoto wao. Sio kila mtu ni mbaya kuna wema pia.
 
Mmh ningekua karibu na rose ningemsunta vya kutosha. Alichofanya sio uungwana kabisa.angekiacha tu kizazi,kuna watu wanatafuta yeye anakitoa jamani.
 
Sky unatakiwa urudi hapa kutoa maoni yako. Tusije tukamsema rafiki yako kumbe mwenyewe unampenda sana
 
Pole yao, dhambi moja tu kutokuzaa wamevunja maandiko.

Mateso pia ni sehemu ya maisha na mwangaza imara in the future.
 
Loo uamuzi wa kipuuzi,VP Rose hana mawasiliano na wale watoto wa mama mkubwa?,au potezea mbaya?.
 
Kitu cha kusitisha katika hii picha nzima ni kuwa wazazi hawakuwa na nia ya kuwatesa hawa watoto, mama Rose aliamini dada yake atamsaidia malezi ya motto, pia hakutegemea kukaa S/A miaka 16 bila ya kumuoana Rose. Baba Robert alimuamini mtu wake wa karibu ili amlelee mtoto wake, matokeo yake mtoto alitaabika na alisiyopenda kuyasimulia inawezekana sexual abuse.
 
Aiseee mmekutana jana jana na kashakupa story yoote hiyo. Ala-ah.

Upo vizuri kwa kuaminiwa.
 
Aiseee mmekutana jana jana na kashakupa story yoote hiyo. Ala-ah.

Upo vizuri kwa kuaminiwa.
Kwasababu Rose na Robert kutoka S/A walikuwa kama celebrity kwenye bash, sasa Rose kutokea kuunga urafiki na mdada wa Kwamtogole si unajua kulikua na hear say nyingi, niliyachukua ya Rose nikaunga na ya pembeni nikapata picha hii.
 
Back
Top Bottom