Kama ilivyokuwa kwa familia nyingi za kikwetu inapoanza migogoro ya kindoa haijawahi waacha watoto salama.
Nikiwa kinda sana kwenye miaka ya 1995/96 wazee waliingia mtafaruku na kujikuta wameachana hivyo kusababisha mgawanyiko wa watoto kimalezi mana MAMA alibakia na baadhi ya watoto na BABA alichukua baadhi ya watoto nikiwemo mimi (Kwa kipindi hicho nilikuwa kama na miaka 5 a 6).
BABA alidhamiria kutulea watoto wake mwenyewe mpaka tulipofikisha umri flani ivi wa kujielewa kisha akaja kuowa mwanamke mwingine, hivyo asilimia kubwa ya malezi, tabia na mafunzo tumeyapata mikononi kwa BABA.
BABA alikuwa ni aina ya watu wenye IQ kubwa, majasiri, wenye misimamo na sio mwenye kutawaliwa na hisia. Alikuwa akitupa kazi/majukumu anawekea na deadline ya kutekeleza majukumu hayo, alipenda tufanye kazi kwa speed na ubora na si kulipua wala kulala lala. Hakuamini kwenye kumuonea mtu huruma ispokuwa kumpa stahiki yake, hakuamini kwenye kumuonesha mtoto mapenzi hivyo hakuna aliyejua kama anapendwa pia hakuwa na muda mwingi wa story na watu muda mwingi huwa mwenyewe na kazi zake kitu kilichopelekea kuogopwa na majirani na wanakijiji kwa ujumla na kusababisha hata sisi wanawe kuogopwa na watoto wenzetu na kukosa marafiki na hata walojitoa kuwa karibu na sisi walifokewa na wazazi wao pia hawakuwa wana enjoy urafiki coz mipaka ilikuwa mingi hivyo hawakuwa huru kuja home wala kucheza na sisi labda muda tukiwa shule pekee. Mzee alikuwa aina ya wale WAZEE ambao wakiingia nyumbani panakuwa kama kuna msiba yani panapoa na kila mtu anachukua position yake akisubiri kuitwa kuhojiwa kwa maendeleo ya shule au kama kuna mashtaka dhidi yake. Hakuamini kwenye kuombaomba, kukopeshwa wala kumuhadithia mtu changamoto zake hivyo alikuwa anakomaa nazo kisabuni.
Kupitia malezi hayo tulijikuta tuki Adapt baadhi ya tabia kila mmoja wetu pasi na sisi kujijua. Kwa upande wangu toka nikiwa shule nikawa mtu naependa vitu vilivyonyooka , sipendi ku reason wala kulalamika hovyo, nikawa nijukuta nina marafiki wachache mno na nisio dum nao. Nikawa muda mwingi napenda kuwa mwenyewe na kutafakari. Napenda tukikubariana kufanya jambo tulifanye kwa wakati na ubora na sipendi kuweka masihara kwenye vitu sereous.
Kwa sasa napitia changamoto katika kuishi na watu hasa jamii zetu za asili maana natafsiriwa kama mtu nisiejali, mkorofi, nina maswali mengi, amri nyingi na najiskia. Nimechumbia zaidi ya mara 4 naghairi na kwingine nakuwa nimekwisha lipa na mahali kabisa ila nina samehe, sababu kubwa ni wenza hao kushindwa kuvumilia speed yangu ya utendaji, kutokuwa na muda nao mwingi wa kuongea nao au kuwa nao pamoja kulingana na hali yangu ya kujali mambo yangu zaidi. Mapenzi ndio kabisa yalinishindaga kitambo toka nipo advnc sijawahi kudum na Mwanamke miezi 6 kisa kuonekana sijali na m binafsi sana.
Kazini napitia changamoto za migogoro na wenzangu kwa tabia za kutaka mambo yalionyoka, sipendi braabraa na huwa si mtu wa story sana nikiona tabia za mtu zitaniathiri kwenye mambo yangu nitamwambia mara moja tu mtu ajirekebeshe kwa yale ninayoamini mimi anakosea, japo nakuwa napendwa sana na mabosi kwa utendaji na u sereous wangu kitu ambacho najihisi nakuwa chanzo cha kugombanisha watumishi na mabosi zao kwa upande mmoja kunichukia kuona najipendekeza na kujiona mimi najua huku upande mwingine kuwaona wenzangu hawafanyi kazi yao ipasavyo kwa kulinganisha na mimi. Tatizo hili limenifanya niache kazi mara kadhaa mana huwa sipendi migogoro.
Kwa kifupi mwenzenu napitia changamoto hizo hasa nikiwa nyumbani Afrika mana kwa shughuli zangu nafanyia nje zaidi. Kwa aliyepitia aina hii ya malezi na hayuko kama mimi naomba anisaidie nini cha kufanya na ambao mnapitia challenge kama zangu naomba tupeane uzoefu.