Malezi: Nimekuta nguo za kike zimefichwa kwenye sanduku la vijana wangu

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,523
27,016
Aisee leo nimepanic kwa ghadhabu, hata nimesahau kuwasalimia.

Nina vijana wangu watatu wa kiume wote, umri wao ni miaka 13, 12 na 8 ambao nawalea mwenyewe [singo dadi] baada ya kutelekezwa na mama zao. Ni vijana watulivu kwa tabia, wenye heshima japo utundu ni kawaida na changamoto za hapa na pale kwa sababu ya makuzi.

Basi bwana leo yamenikuta, ile kujifanya mpekuzi, nimefukunyua moja ya sanduku lao nikaibuka na mshangao na butwaa. Nikafurusha ‘vinguo vya kike’ katika moja ya ‘zip’ vilivyokunjwa na kuhifadhiwa kwa ustadi mkubwa.

Ni kiblauzi na kisketi, makadirio labda binti wa miaka 12 hivi umbile la wastani, nimesikitika na kukaa Irina kwa wakati mmoja.

Nikafanikiwa kujizuia na kuvirudishia kama vilivyokuwa, nipate kwanza utulivu na ushauri wa mbinu gani nitumie ili kujua ukweli.

Kwa haraka haraka nimewaza hawa madogo wameshaanza kutafuna, na je hizi nguo wamepora kwa binti wa watu wamepewa au wamenunua kwa lengo la kupeleka zawadi..?

Maswali ni mengi sana wakuu, nimefanikiwa kudhibiti ghadhabu yangu hadi hapa sijasema kitu, natafuta namna bora kabisa ya kujua ukweli wa hili.

Hebu tupeane mawili matatu, napenda sana utani ila linapokuja suala la watoto nasimama juu ya mstari, sina uzoefu zaidi na malezi ila napambana kwa kila namna ninayoweza na inayofaa hivyo nakubali mapungufu.

YAMENIFIKA HAPA.
 
Nadhani ni vyema kuwauliza

kujadiliana nao
Na kuwakanya pia
Wa kuchapa hapo labda wa miaka 8

Hao wengine ni kuelekeza kipi cha kufanya
13 na 12 wafundishe kujiheshimu ..bidii ikiwekwa kwny shule ama biashara

lakini pia wafundishe juu ya STDs na kutumia condoms
 
Mkuu kwanza pole sana

Pili kwa ujumla wetu tuombe Mungu theory yako iwe sawa yaani ziwe ni za binti kaamua kumpa kijana wako kama sehemu ya kujifunza mapenzi maana maisha ya sasa changamoto ni nyingi sana mkuu, siombei na wala hatuombei ila usipaniki kaa na chunguza vizuri, isije kuwa mwanao ni za kwake hizo anavaaga

Dunia imeharibika sana na vijana wengi wamekuwa wahanga wa ushoga

NARUDIA TENA, GOD FORBID MWANAO ASIWE KWENYE HILO KUNDI na usimame kifua mbele ujisifu kuwa kidume kimeanza kuhongwa nguo na 'videmu' vyake.................
 
Ha
Pole sana Mkuu,Dunia ya leo imekaa vbaya sana fanya research kimya kimya huenda ukagundua na mambo mengine mengi
Pia,huenda unapokuwa umetoka huyo dogo mwenye umri wa miaka 18 huwa anafanya mjengo wako kuwa machinjio so,inavyoelekea kuna mtoto wa kike alikuja kupigwa kipala akaziacha nguo zake hapo kwako!

Sent using Jamii Forums mobile app

Hakuna mwenye miaka 18 kutokana na mleta uzi ni miaka 13 bado ni Watoto wadogo sana.
 
Utajiuliza mengii uumize kichwa.
Cha kufanya ni kuwaita wote na kuwaambia wachukue mabegi na watoe nguo moja baada ya nyingine Kisha zikionekana hizo za kike uliza ni za Nani na zimefikaje hapo.

Huenda Ni za ndugu kwa mama zao Kama ulivyosema ni Kama Kila mtu ana mama.

Maana kwa akili yangu siamini binti wa 12 yrs atoke nyumbani na nguo ya kubadili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je, unawalaza chumba kimoja? (Kwangu ni sawa watoto wa kike kulala pamoja ila si wakiume)
Kuna mengi unaweza fikiri vijana wameanza kufanya kazi kumbe ni za mmoja wao anavaa.. naombea isiwe hivyo. Bora iwe ya mtoto wa kike kaiacha.

Ni kweli wanalala chumba kimoja, hawana tabia wa mienendo ya kike kuhisi labda wanavalishana au wana michezo ya hovyo.... kwa kweli hili litakuwa la mwisho sana hata kulifikiria.
 
Utajiuliza mengii uumize kichwa.
Cha kufanya ni kuwaita wote na kuwaambia wachukue mabegi na watoe nguo moja baada ya nyingine Kisha zikionekana hizo za kike uliza ni za Nani na zimefikaje hapo.

Huenda Ni za ndugu kwa mama zao Kama ulivyosema ni Kama Kila mtu ana mama.

Maana kwa akili yangu siamini binti wa 12 yrs atoke nyumbani na nguo ya kubadili.

Sent using Jamii Forums mobile app

Likizo kuu waliyoweza kusafiri mbali ni disemba labda walikuja nazo, hii walifika hadi kwa mama zao na kukaa kwa muda... waliporejea ndipo mmoja wao alithubutu kuniuliza “Baba utaoa lini..?”.

Huyu mdogo mama yake hayupo mbali hivyo hukaa naye kwangu anakuja wikendi tu, kuhusu kuwaita wote na kuwahoji ni njia nzuri.... ngoja tuone.
 
Ingelikuwa ni mimi nisingewauliza, ningefanya uchunguzi wa siri siri sana nikishajua nini kinachoendelea ndio nawauliza na kuweka mambo yote hadharani na kuwaelimisha au kuwachapa kadri matokeo ya uchunguzi yalivyoonyesha

Namna gani naweza kufanya uchunguzi..?
 
Vijana wa saiv unaweza shangaa niza mmoja wapo ana taka kuwa tofauti na wenzie



Time is a drug. Too much of it kills you

Kwa kadri ninavyopata muda kuwa nao, sijawahi hata kuhisi viashiria vyovyote.... wanashinda shule halafu wikendi nakuwa nao kama ni ibadani au batani.
 
Nadhani ni vyema kuwauliza

kujadiliana nao
Na kuwakanya pia
Wa kuchapa hapo labda wa miaka 8

Hao wengine ni kuelekeza kipi cha kufanya
13 na 12 wafundishe kujiheshimu ..bidii ikiwekwa kwny shule ama biashara

lakini pia wafundishe juu ya STDs na kutumia condoms

Asante mkuu, ipi sababu ya kumchapa wa miaka 8 pekee..?
 
Back
Top Bottom