Kasiano Muyenzi
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 13,972
- 22,933
Tulipokubali kuoana, mimi na Naomi wangu tuliandika malengo yetu ya uhusiano.
Tulikubaliana kukua pamoja kitaaluma na kusaidia malengo ya kazi ya kila mmoja.
Tulikubaliana kusaidiana katika ustawi wetu wa kiakili, kimwili na kiroho.
Tulikubaliana tuwe na maombi na kusoma maandiko pamoja kila siku.
Tulikubaliana tuwe tunakula chakula cha jioni pamoja kila siku.
Tulikubaliana tuwe tunatembea pamoja mara moja kwa wiki.
Tulikubaliana tuwe tunafunga pamoja mara moja kwa wiki.
Tulikubaliana tuwe tunatoka out kwa chakula cha jioni ili kubarizi pamoja angalau mara moja kwa wiki.
Tulikubaliana tuwe tunaenda likizo sisi wawili tu angalau mara moja kwa mwaka - na angalau mara mbili na watoto wetu.
Tulikubaliana lazima tuwe na muda mzuri na watoto wetu kila siku - na kwamba hatutapingana kamwe mbele ya watoto wetu, wazazi, ndugu, marafiki au mtu mwingine yeyote kwa jambo lolote.
Sasa basi tulipoanza kuishi pamoja hatukuwahi kufikiria kutakuwa na mzozo wowote katika ndoa yetu. Lakini baada ya muda mizozo ilianza kuibuka, hapo ilitubidi tukubaliane namna bora ya kusuluhisha mizozo, kila inapotokea.
Pia tulikubaliana jinsi ya kuongeza ukaribu katika ndoa yetu ili kuepusha uhusiano wetu kusambaratika. Baadaye, tulikutana na zana ya mawasiliano ambayo imetusaidia tunapokuwa na ajenda nzito mezani.
Tunasonga mbele kufikia malengo yetu.
For many couples, the great tragedy is not falling to reach their goals, but having no relationship goals to reach.
Je, mmeandika malengo yenu ya uhusiano kama wanandoa?
#USIKATAE NDOA.
Ubarikiwe.