Malecela azungumzia afya yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malecela azungumzia afya yake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Jun 23, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 22 June 2011 21:40 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Boniface Meena
  MWANASIASA mkongwe na kada maarufu wa CCM, John Malecela, amezungumzia afya yake kutokea nchini Uingereza, akieleza kuwa inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo katika Hospitali ya Wellington North nchini humo.

  Hata hivyo, taarifa za kitaalamu zilizolifikia gazeti hili zinaonyesha kuwa Malecela alipata tatizo la kuvimba kwa mishipa inayotoa damu moyoni kwenda mwilini na kusababisha mtiririko wa damu kuyumba kwa kiasi.

  Taarifa zilisema kutokana na hali hiyo, njia pekee ya kuondoa tatizo hilo ilikuwa kumfanyia upasuaji mkubwa wa moyo ambapo madaktari walilazimika pia kuchukua mishipa kutoka katika mguu wake na kuweka kwenye moyo wake.

  Lakini jana, Malecela mwenyewe aliyezungumza na Mwananchi kutoka Uingereza alikolazwa baada ya kufanyiwa upasuaji huo, alisema kuwa madaktari wamemshauri afanye mazoezi kwa muda wa wiki tatu hadi sita ili waangalie hali yake na baada ya hapo wataweza kumpa ruhusu ya kurudi nchini.

  "Ninaendelea vizuri na madaktari wameniambia nifanye mazoezi kwa muda wa wiki tatu hadi sita kuiangalia hali ikoje ili waweze kunipa certificate (cheti) ya kuweza kurudi nyumbani,"alisema Malecela.

  Mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, amezungumzia hali ya mwenendo wa afya yake baada ya juzi Spika wa Bunge, Anne Makinda, kuwatangazia wabunge taarifa za kutokuwapo bungeni kwa Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela kutokana na mumewe kuwa mgonjwa na kufanyiwa upasuaji wa moyo.

  Mama Kilango naye azungumzia
  afya ya mumewe

  Akizungumzia hali ya mumewe, Kilango alisema kuwa walikwenda nchini Uingereza Mei 11 mwaka huu wa ajili ya kumfanyia Malecela uchunguzi wa kawaida wa afya kama ilivyo kwa viongozi wa Serikali na alikuwa hana tatizo lolote.

  Alisema kuwa yeye na mumewe wana kawaida ya kufanya mazoezi kila siku na kwamba walipokuwa katika mazoezi ya kawaida nchini Uingereza ambapo Malecela alianza kulalamika kuwa anapumua kwa shida, ndipo walikwenda hospitali ambapo alipimwa na daktari kumweleza kuwa ana matatizo ya moyo.

  "Madaktari walimpima wakaona kuna mishipa inayotoa damu moyoni kwenda mwilini ambayo ilikuwa imevimba kutokana na Calcium kujikita kwenye mishipa na kuzuia mtiririko wa damu," alisema Kilango.

  Kilango alisema upasuaji huo ulifanyika Mei 31 mwaka huu katika Hospitali ya Wellington North na daktari aitwaye Rakesh Uppal.

  "Upasuaji umefanikiwa na yuko nyumbani sasa. Anatakiwa afanye mazoezi mara tatu kwa siku, dakika 20 asubuhi, dakika 20 mchana na dakika 20 jioni. Anafanya mazoezi akiwa na mlinzi wake pamoja na mimi hapa,"alisema Kilango.

  Habari za kuumwa kwa mwanasiasa huyo ambaye ameshika nyadhifa mbalimbali serikalini na CCM zilitangazwa juzi na Makinda wakati akiahirisha Kikao cha Bunge.
  Malecela,77, ameshika nyadhifa kadhaa zikiwamo za uwaziri na mbunge kwa vipindi tofauti hadi alipostaafu siasa mwaka jana akiwa Mbunge wa Mtera.

  Aliwahi pia kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara, ambako alishiriki katika kazi nyingi zikiwamo za kuwapigia kampeni wagombea wa chama hicho kila ulipojitokeza uchaguzi mdogo
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Afya njema kwako mzee!
  For better, for worse, bado unahitajiwa sana!
   
 3. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Pona haraka mzee wetu, Jahazi linazama huku...na upepo unazidi kugeuka.
   
 4. F

  Froida JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Tunakuombea upone haraka urudi nyumbani salama
   
 5. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Nakutakia afya njema baada ya Upasuaji. Kwa wanajamii forum hivi ni nani anaye eneza uvumi wa kua kuna kitu kama raisi mstaafu, waziri mkuu mstaafu,mbunge mstaafu n.k????Hawa wananatakiwa wawe wanaitwa aliyekua....Kwa tafsiri ya moja kwa moja kwenye kiingereza ni Former=Aliyekua na Retired=Mstaafu. Vyeo vya kisiasa nilivyovitaja havina mstaafu. Hii tabia ya kufurahisha watu kwa kuwapa 'titles' sisizozao inakera sana. Angalia kwa mfano anamwita Malecela mbunge mstaafu wakati alishindwa kwenye uchaguzi. Kwa mtazamo wangu hii haikubaliki. Waandishi kuweni na umakini jamani mtajenga taifa la "Mazumbukuku"
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kila laheri Mzee Malecela kwenye kurudisha afya yako! Kuna habari ziliisha anza kuenea jamani lol
   
 7. MANI

  MANI Platinum Member

  #7
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,410
  Likes Received: 1,863
  Trophy Points: 280
  Ugua pole mzee wetu uje usaidie huku mambo yanawazidi wenzio.
   
 8. M

  Masuke JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Pole mzee wetu Malecela, Mungu akupe nguvu upone haraka urudi nyumbani.
   
Loading...