CHA The GREAT
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 651
- 855
Malcolm X, anatajwa kama moja ya watu weusi wenye ushawishi mkubwa kuwahi kutokea. Katika moja ya hotuba zake, Malcolm X anazungumzia uhusiano uliopo baina ya elimu duni na umasikini. Kwamba, ukiwa unaishisehemu duni, basi utakuwa unaishi sehemu ambayo ina shule duni. Na unapoishi sehemu iliyo na shule duni, basi utakuwa na walimu duni. Na unapokuwa na walimu duni, maana yake ni kwamba, utapata elimu duni; na ukipata elimu duni maana yake ni kuwa masikini maisha yako yote.
"When you live in a poor neighborhood, you are living in an area where you have to have poor schools. When you have poor schools, you have poor teachers. When you have poor teachers, you get a poor education. When you get a poor education, you are destined to be a poor man and a poor woman the rest of your life".~Malcolm X.
Hapa Malcolm alikuwa akijaribu kuwaamsha watu weusi katika kupigania haki zao ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa elimu bora na si bora elimu. Katika kipindi chote cha maisha yake kama mwanaharakati mpigania haki za watu weusi, Malcolm hakusita kusema kile alichokiamini kwa uwazi. Kwa lugha rahisi, Malcolm X alikataa unafiki.
Unakumbuka lipi juu ya Malcolm X kupitia vitabu na hata makala mbalimbali?