Malaya na makahaba waziweka ndoa nyingi "chini ya ulinzi"

Malaya na makahaba waziweka ndoa nyingi "chini ya ulinzi"

winnerian

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
408
Reaction score
638
Unyenyekevu na utii wa wanawake walio kwenye ndoa umekua chini ya kiwango himilivu katika ndoa nyingi na hivyo kusababisha waume zao kupata pumziko la amani kwa wale wanawake wanyenyekevu, wastahimilivu, watii na wasiokuwa na makuu kwa namna yeyote ile. Hawa ndio wanaitwa malaya na makahaba ambao kwao kumuhudumia mwanaume katika ule uhalisia wa kimwanamke ndio kazi yao ili wapate kuishi. Hapa sizingumzii vile vibinti vinavyo jiuza Telegram na kwenye magroup ya whatsapp nazungumzia wale wanawake "emotionally matured women" ambao wanawatenda VYEMA wanaume wa wenzao kwa upendo, utii na ukarimu kama yasemavyo maandiko katika kitabu cha Waefeso: 22 Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.
23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.


Enyi wake watiini waume zenu haijalishi anapitia katika hali gani!

LAKINI JANGA KUBWA LINALOZALISHA HAYA YOTE NI WANAUME KUTOKUWAPENDA WAKE ZAO.

25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;
28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
29 Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.
 
"Unyenyekevu na utii wa wanawake walio kwenye ndoa umekua chini ya kiwango himilivu katika ndoa nyingi na hivyo kusababisha waume zao kupata pumziko la amani kwa wale wanawake wanyenyekevu, wastahimilivu, watii na wasiokuwa na makuu kwa namna yeyote ile."

 
Hilo ndilo BANGO KUBWA linalotakiwa kuwekwa pale Ferry karibu na Ikulu, Magogoni Street.
 
Back
Top Bottom