Malawi,Tanzania begin talks over Lake Malawi dispute

Tuingie na kwenye comments zao, nasi tupost humo.

I trust in God, I am Confident in JF
 
Ni maajabu! Hizo ramani za google kaweka nani? Na sisi washamba bado tumelala? nina miaka zaidi ya hamsini na ramani tulizofundishiwa na zilizopo zinaonyesha mpaka uko katikati ya ziwa. Hizo zo Google ni mikakati iliyoandaliwa kwani wanajua wa TZ tumelala. Mwaka jana nilifika Mbamba bay port hata lile gati ni kichekesho kwani halitumiki tangu limejengwa. Wale wabongo wa pale kula yao vaa yao vyote vyatoka Malawi what a shame! Ila ardhi yake ni nzuri mno including the lake. Serikali imezoea kudili na upinzani, migomo wanaacha mambo ya muhimu kama haya. Hata wale wachina wanaotengeneza barax2 Songea Mbinga mbamba bay wanachimba madini kule msituni na hakuna anayewafuatilia! Mimi niko tayari kwenda mstari wa mbele kutetea ardhi-maji yetu kwa ajili ya vizazi vyetu vijavyo. Najua huo utafiti una mkono wa mataifa makubwa lakini cha msingi waishie hukohuko kwenye mpaka tunaoujua na kuuheshimu sisi. Hata kama mazungumzo yanaendelea tusikubali kabisa walete mitambo yao upande wa kwetu. JWTZ Songea mbele kwa mbele ziwani you have a work to do!
 
Well done Man, i real love your work......

sikujua mchezo wa Uingereza, between 1914-1948.

sikujua kwamba Joyce banda ni ndugu na Kamuzu Banda.

Someni makala iliyoandikwa na Ndugu JAMES ZOTTO

Sakata la mpaka kati ya tanzania na malawi: POLITICS VERSUS FACTS

Ndugu zanagu, huenda mnafuatilia vizuri tatizo la mpaka wetu wa ziwa nyasa na malawi! Nilishtushwa sana na hotuba ya bwana waziri. mimi napenda utaifa wangu na uzalendo wangu. lakini napenda sana kutetea mambo yangu kwa kuukubali ukweli, kujua facts zaidi, kukubali hata zile zinazonipinga na ndipo najipanga kujenga joja.

Eneo hili nafanyia study yangu ya PhD. Sidhani kama nipo sahihi zaidi na lengo langu si kusema nani anamiliki nini! Ukweli naoufahamu, tatizo si kubwa kivile kama tunavyolifikiri kama tutachukua muda kupitia documents zote na muhimu. Tunahitaji kwenda Public Records Office-Uingereza, Colonial Archives Potsdam, ujerumani, pia malawi national archives, tanzania national archives, libraries za UDSM na Chancellor college malawi. naamini ubishi utaisha kwa kuwa documents zote zipo.

Angalizo: ziwa nyasa liligawanywa na mabeberu wa kiingereza, kijerumani na kireno. mkataba wa 1890 uitwao anglo-german agrrement unasema mpaka wa German east africa(tz bara ya leo) na nyasaland(malawi ya leo) unapita kandokando ya ziwa nyasa kutoka mto ruvuma mpaka mto songwe! huu ni mkataba wenyewe, upo ktk documents nyingi sana.....!!international law inajua hili na international lawyers wanaelewa nini nazungumza! Sehemu nyingine ilikuwa ni 1891 kati ya ujerumani na ureno, mpaka ulianzia mto ruvuma kuelekea Portuguese east africa(msumbijin ya leo) na pia ureno ikawekeana mpaka na british nyasaland(malawi)...kwahiyo, kipindi cha ujerumani, mpaaka unasomeka 'it passes along the shore of the lake(nyasa).....

Mabadiliko ya mipaka: kipindi cha kikoloni, kabla ya mjerumani kuondoka, marekebisho ya mipaka yalifanyika kati ya mjerumani na mreno kwa kuspgeza mpaka mbele 0.5 KM from the original tripartite point, na vijisiwa vya mto ruvuma vikagawanywa. mpaka leo ipo hivyo. na eneo lingine ni kati ya mwingereza na mreno, ambapo, kisiwa kilichopo eneo la malawi linamilikiwa na msumbiji mpaka leo na eneo la ardhi lililopo msumbiji linakaliwa na malawi. mhuo ulikuwa mkataba wa marekebisho na ipo hivyo mpaka leo. kwahiyo, tulivyorithi mipaka, tumerithi na mabadiliko haya na hivyo hatuwezi kugombana na msumbiji wala msumbiji hawawezi kugombana na malawi. Mpaka wetu na malawi haukurekebishwa popote pale mpaka mjerumani anatoka...

Marekebisho ya mipaka kipindi cha uingereza: sote tunajua german east africa, sisi pamoja na ruanda na urundi tuligawanywa katika sehemu mbili, ttukiwa chini ya League of nations tukiangaliwa na uingereza. Kunamabo nahitaji tuweke sawa. tukaitwa mandated territory na uingereza ni mandatory power. turudi ktk kamusi tutofautishe a an annexed colony and a mandate! Mpaka ukawekwa kati ya ubelgiji na uingereza, uliitwa the MILNER-ORTS AGREEMENT OF 1922! katika mkataba huu, mto kagera ulikatwa katikati na mpaka leo tumerithi hivyo. Hapakuwa popote pale ambapo eneo la ziwa nyasa lilirekebishwa kwa njia ya mkataba baina ya nyasaland state na tanganyika state...., isipokuwa, tofauti na mandates zote, tanganyika pekee, ilikuwa na tofauti ndogo, ambapo, mpaka wa ziwa nyasa ukapewa wanachoitwa 'wording', na hivyo, ramani ya tanganyika na official records zikaonyesha kuwa mpaka umepita katikati ya ziwa nyasa! na hapa ndipo tatizo linapoanza na sisi tumechukulia hii ndo absolute fact, hatuendi mbele kidogo. haya yapo pale national archives secreatarita files, ACCESSION NUMBERE AB 8 na AB 30! nafikiri hotuba yote ya bwana mkubwa jana imetoka ktk files hizi, ndizo walizopelekewa!!!

twende mbele kidogo, ni kweli, kama mheshimiwa alivyosema jana, ramani nyingi kuanzia 1922 mpaka 1939 zinaonyesha mpaka upo katikati ya ziwa! je, ukweli huu utatutosha pekee mbeleni tukifikishana mbali? hapana!mheshimiwa hakusema kuwa ramani zingine, japo chache muda huu huu na official reports hazionyeshi mpaka au zinaonyesha mpaka upo chini. lakini ni chache! kwanini hili?bado natafuta majibu, lakini kwa harakaharaka, unaweza ukasema kuwa uingereza ilitamani tanganyika iwe koloni lake na si mandate! na pia ilishinikizwa na wawekezaji na hata jeshi ilisema afadhari waiteke ili liwe koloni na waachane na mandate! nahitaji tuelwe maana ya mandate.

Hii yote ilitokea baada ya Donald Cameroon, governor wa tanganyika kusema kuwa tanganyika is a part of the british empire and it will remain so! hii ni siasa na si ukweli kama unaelewa maana ya kuwa wao hawakuwa wamepewa koloni kama mali yao, bali kuliangalia mapaka wananchi wapate 'akili' ili wapewe uhuru! kwa hiyo, kimsingi, kwa maana ya sheria ya kimataifa, tanganyika haikuwa part ya british empire kama yalivyo makoloni yaliyotekwa mojakwa moja na uingereza yenyewe! hapa pakatokea mvutano mkubwa sana katika house of Lords na house of commons! na hivyo basi, mtafaruku huu wa mpaka ulianzia hapa, kwa kauli hii na hivyo hata waingereza wenyewe walivutana kuhusu mpaka. ipo hivi, mwaka 1926, wajumbe wa mabaraza waliibana serikali iseme mipka ya tanganyika na ule wa ziwa nyasa! mabishano, kama haya yetu leo yalikuwa makubwa, ila si kwa kutishiana kwa kuwa walikuwa wenyewe na walitaka kuwekana sawa! ndipo secretary of state for colonies alibanwa na mjadala ulikuwa wa kisheria zaidi ukihoji status of the mandate, british empire, n.k; na kama waingereza wanamamlaka ya kujipangia kuhusu koloni waliolokabidhiwa kuliangalia(nieleweke na si kulimiliki)! mwishowe, mtu huyu mwenye dhamana alisema kwamba, hata yeye anashindwa kuelewa, 'what exactly is the sovereignty of tanganyika lying'! jamani mnamwelewa huyu mtu? kwamaana hiyo, haelwi vizuri mipaka yetu, ambayo wenyewe ndo wameirekebisha au kuipa 'wording'!! hivyo, tatizo linaanzia hapa na si muda mwingine wowot!!!

Kipi hakusema bwana mkubwa jana: kuanzia 1939, mambo yalibadilika na hawa hawa watu tunaochukua ashahidi kutoka kwao, wakafanya madudu! na ilipoisha vita ya pili ya dunia, jamani oneni haya, hawa waingereza katika ramani zao, tena nyingi mno,(kaangalieni East africana section, university of dar es salaam, sehemu ya thesis, kuna cabins 3 zimejaa ramani na bado ni mpya sana kutokana na kutunzwa na pia kutotumka sana), kuimbezinaonyesha, bila shaka yoyote, kuwa mpaka wa tanganyika na nyasaland unapita pembeni mwa ziwa na si katikati! mkuu hakusema hili. aliishia 1939! kumbe hawa jamaa walichora tena ramani zote zikionyesha mpaka upo pembeni mwa ziwa!!!! kwanini hili?natafuta majibu, lakini nkwa haraka naweza nikaspeculate mawili. mosi, karibu na vita vya pili vya dunia, ilisikika tetesi kule duniani kuwa, ujerumani inarudi na inakuja kuchukua malokoni yake. (kasome national archives of tanzania, secreatariat files zote zenye kichwa cha habari, 'the future of tanganyika in british empire'). kwa hiyo, waingereza walihofia kutimuliwa na kurudi kwa wajerumani, na hivyo, wakarudisha ule mpaka wa awali wa 1890! na pia, muda huu, baada ya kwisha vita, tanganyika ikawa chini ya UNO ambapo ilipewa trusteeship status!maana ya hii ni rahisi kuliko mandate!ilimaanisha to be granted immediate independence! maana ya neno immediate hapa ni kwamba, kwa tafsiri yangu, waingereza wlifahamu wanatimka mapema mno kwani mkataba unasema hivyo....nafikiri, wakarudisha ramani zikionyesha mpaka upo pembeni...na kitabu ch Nyasaland cha mwaka 1958, kinaonyesha mipaka ya nyasaland na ziwa lote likiwa kwao! tukitaka kuwashinda wamalawi, lazima tukisome vizuri kipindi hiki na tuelewe facts zipi zinawapa kiburi na zipi sisi tuzitumie, la sivyo, tunaweza.............!!!!!!!!!!!!! kwahiyo future of tanganyika ilikuwa contested, uncertain, etc kipindi hiki, pamoja na mipaka yake pia!! tujiulize, kwa maana ya mandate, waingereza walikuwa na legal authority 'kurekebisha' mpaka wa ziwa nyasa? na je makosa waliyofanya waingereza, ndo legal backing yetu sisi? ebu tuzame tena tutafute facts tuwashinde hawa jamaa!

Tulishindwana na uingereza kurekebisha mipaka. mwalimu alisubiri mpaka malawi iwe huru!akatoa miaka mitatu tu na asingetambua mipaka ya kikoloni(soma hansard, 1962). walipopata uhuru, kukawa na matatizo ambayo jana bwana mkubwa aliyaeleza. nampongeza ni dhahiri, 1964 cabinet crisis ya malawi na wale mawaziri kutorokea nchini kwetu kupitia ziwa, banda akaona ziwa ni infiltratio route! sera zetu za mambo ya nje zilikuwa tofauti. tulikuwa frontline state kwa ukombozi, wenzetu wakasapoti makaburu na wareno na wakawa na balozi sehemu hizo.....wakagombana na mwalimu, military show down miaka ya 1967-8; matusi na kejeli zikatawala kati ya mwalimu na banda, sisi na malawi.....kipara cha banda kinamagamba, tuliimba tukiwa jeshini, mwalimu akasema mpaka a sensible leader akitokea malawi ndipo tutajadili tena swala hili na si na kamuzu banda! tulikuwa kimy, na kuanzia 1975, hatukuwa na tatizo,lakini si kusema kuwa tulitatua tatizo la mpaka!

Tulikaa kimya!mipaka haina tatizo isipokuwa ni time bomb ambapo ikitokea spark ni explosion! Tuliirithi kupitia Article III ya OAU CHARTER ya 1964 BAADA YA DEBATES KUBWA NA WENGI WAKARIDHIA TUIRITHI, uti possidetis, ita possidetis principle (so as you exist, so may you exist), kama kawaida yetu tulidesa ya kibeberu, Westphalia principle, border inviolabiliy! hatukupata muda mwingi wa kutafakari na kuangalia kila mpaka na matatizo yake....tulirithi na matatizo na yanatutatiza leo!!!

Way forward! naikiri tuna namna tatu ya kulimaliza! moja ni kwa majadiliano ya kawaida yaani diplomacy kama bwanamkubwa alivosema jana. pili ni kupigana vita. (war is another means of diplomacy), mnataka kuniona kichaa!huo ndo ukweli, atakayeshindwa atasalimu kama ilivyokuwa kwa uganda na sis. tatu ni mahakama ya kimataifa yaani International Court of Justice! hapa ninawasiwasi. kama facts zenyewe ni zile za jana tu, sijui kama tutatoka.tutulie, tuite wataalamu wetu wajikite ndani sana. ni kweli kama alivyosema jana bwana mkubwa kwa kunukuu kesi nyingi na zilizoshinda, na kwa kusema kuwa, tukienda mahakama ile sisi ndo tutashinda!!!ninashaka....tumejipa favour ya verdict! kabla ya kesi.sijui.ninashaka kubwa!kunakushinda, kushindwa au suluhu!ninashaka tena na tena!

mimi nimzalendo,nataka ukweli kwa njia ya mahojiano na kuumiza kichwa, tutetee mali zetu tukijua tunawashinda kwa hoja.....!!!!

Wasiwasi: inasemekana kuna mafuta ziwani!!! kwahiyo mjue marekani na washirika wake hawako mbali! tujue operation ya military imperialism na huyu mama, mpwa wa kamuzu banda, anapata wapi hiki kiburi...nyuma yake kuna nini na nani!!1tuangalie haya pia.

Hitimisho. tusiwe na hoja moj tu mkononi kama ndo water-tight evidence. tujaribu kuzibishanisha hoja zetu. na hoja nzuri ni zile zinazopingana nasi na tusizozipenda, tukizielewa na kuzikubali ndipo tutajipanga namna ya kuzigalagaza. tumwelewe vizuri adui yetu.....MUNGU IBARIKI TANZANIA!ZIWA NYASA!WANYASA!WATANZANIA!

Tusing'ang'anie tu REPARIAN LAW!
 
But webondo, mi naona hata base yao bado ni weak, kwa kuwa hiyo mikataba yoote tangu ule wa Heligoland iliingiwa na wakoloni tu on behalf of, na ile ya baadae pia.
Swali kwako webondo,
inasemekana nyerere baadae alikuja kuwithdraw kutoka kwenye iyo mkataba wa OAU unaotaka mikataba ya kikoloni iheshimiwe specifically ikiface malawi border hii ni kweli????
 
Tatizo la mpaka baina ya Malawi na Tanzania unatokana zaidi na Article ya kwanza ya Berlin Conference ya mwaka 1885. Chini ya makubaliano hayo ya Berlin, Ziwa Nyasa, Tanganyika na mito yote katika eno la Congo ilikuwa ni free trade areas. Sasa kwa vile Heligoland-Zanzibar treaty iliposainiwa, bado eno lote la Malawi lilikuwa halina mamlaka, mpaka wa German East Africa ulikubalika kuwa ukingoni mwa ziwa kwa kujua kuwa Ziwa Nyasa ni free trade area. Wakati utawala wa British Central Africa unatangazwa mwaka 1902, uliweka bayana kuwa himaya hiyo ni magharibi mwa Ziwa Nyasa, na hivyo kuacha eneo la Ziwa haligawanywa, nadhani kutokana na Article 1 ya Berlin Confenrence. Baada ya hapo mkutano mwingine wa mpaka uliofanyika ni ule uliorekebisha mpaka wa kaskazini ya Malawi na Zambia kwa vile ziwa lilikuwa bado ni free trade area. Sasa mabadiliko ya mpaka yaliyofanywa na uingereza baada ya kutawala maeneo yote mawili ndiyo yanayoleta utata kwani uingereza hiyo ilihamisha mpaka huo mara mbili kinyume cha sheria bila kuihusisha league of Nations ambayo ilikuwa na mamlaka juu ya Tanganyika; ndiyo maana mpaka huo haukidhi makubaliano ya OAU.
 
KAMA KAWAIDA WATAKUWA WALILAALA AU HAWAKUSIKIA KILICHOONGELEWA KWASABABU TZ NI VIHIYO WA LUGHA HASA HAWA VIONGOZI WANAOWATEUA MAOFISA VIHIYO. TUTAKULA hasara ya mambo mengi sana kutokana na viongozi wenye uoni hafifu has a ktk masuala ya maslahi na hatima ya nchi yetu. watanzania tuwaondoe wababaishaji hawa tuweke watu watakaokesha kuilinda nchi hii na watu wake dhidi ya wenye uchu wa taifa letu. usishangae kesho lake tanganyika ikadaiwa ni ya drc , zambia na burundi na victoria ya kenya na uganda, indian ocean ya zanzibar, kenya na somalia sitashangaa. Tukae mtakuja kuniambia. CCM IMEZEEKA. NYUMBA IKIZEEKA NA KULIWA NA MCHWA NI VIZURI UKAIBOMOA NA KUIJENGA UPYA. MUSTAKHABALI WA TANZANIA HAUWEZI KUENDELEA KUWA CHINI YA CCM. TUJIULIZE HAO WAKUU WA WILAYA NA MIKOA WANA KAZI GANI WATU WANAFANYA EXPLORATION ZIWANI WAO WAMELALA TU WATU WANAANZA KUGAWA PLOT ZIWANI WANANCHI NDIO WANTOA TAARIFA. TUN HAJA GANI NA MFUMO HUU WAKUPEANA FADHILA?
 
If they are looking for a fight... they should be careful with whom they pick it... We will kick their behinds all the way to Lilongwe...

Stop the damn exploration till the issue is resolved.... if they want to be lead by the PMS of madame prezzo... shauri yao!
 
you must be binldens agent. Do you also want to be barried at the see. You are a funny ara agent. You grand mother is very poor and u want to go to war? Very stupid thinking!!!!

If they are looking for a fight... they should be careful with whom they pick it... We will kick their behinds all the way to Lilongwe...

Stop the damn exploration till the issue is resolved.... if they want to be lead by the PMS of madame prezzo... shauri yao!
 
you must be binldens agent. Do you also want to be barried at the see. You are a funny ara agent. You grand mother is very poor and u want to go to war? Very stupid thinking!!!!

Kyelatz if you cannot write English properly feel free to use kinyakyusa... Otherwise go back to grammar school or ask your betters to help you out!!

Learn to behave, learn to speak... then come back and argue with me.. and this time, leave my grandmother out of it... for surely she is richer than your mother who still keeps on being seen at kinondoni makaburini during questionable hours...
 
The leadership in both countries must be made to desist from fueling tension and hatred between the brotherly and sisterly peoples of Malawi and Tanzania ..They all must be forced by public pressure to accept the only sensible 20th century solution to the territorial dispute... adhering to the terms of the " the 1982 UN Convention on Law of the Sea that stipulates that in case nations are bordered by a water body (sea or lake), the border of the two nations will always be on the middle of the water body." We should NOT encourage our already power intoxicated and arrogant political leaders to beat war drums and adopt an hypocritical national jingoistic stance to hide their singular lack of patriotism in managing our natural resources, such as minerals including gas and oil... How can one fight a war successfully when ones' teachers and doctors have been drive into despair and are indeed on a warpath with the governmen. When Nyerere led the war against Iddi Amin the national was relatively united behind a national hero, Mwalimu Nyerere, whose integrity was impeccable. War under the leadership of an unethical assortment of self-seeking primitive accumulation Machiavellian dilettante would be a disaster!
Mwl. Lwaitama
 
na msije kabisa..simnajua tunajeshi la maji imara sana...
Mkuu jonas malawi hawana jeshi lolote imara njaa inawasumbua wataweza vita...???na cku zote meli zao (MV Ilala na MV Ntendere)zilikuwa zinapeperusha bendera za tz kwa misingi gn kama walikuwa wanapita kwenye ziwa lao????
 
Back
Top Bottom