Malawi,Tanzania begin talks over Lake Malawi dispute

Malawi,Tanzania begin talks over Lake Malawi dispute

Kinachosubiriwa ni sahihi ya Amiri Jeshi Mkuu, Mhe JK. Tumeshafanya uchunguzi na upembuzi yakinifu wote, tumeshamkabidhi proposal zote. Na conclusion ni kuwa atangaze vita wakati wowote ili tuwachapa wamalawi. It sounds crazy but it is the fact. Wamalawi wanawabeza sana watanzania, it is high time kuwaonyesha kuwa watz si slaves wa UK kama walivyo wao.
 
Ni hatari sana nchi kutawaliwa na mwanamke. Anaweza kuwa na akili mbaya kama ya Yezebeli
 
watapitia wapi mpaka wafanye utafiti na upande wa Tanzania? Leo bungeni mpaka wawakilishi toka zenji wamelililia ziwa nyasa
 
Diplomasia itumike katika kusovu huu mgogoro kama vp waelimishwe mwisho wa mipaka yao,kama ikishindikana jeshlitatumika
 
Mazee mie sishangai sana sophia banda ku anzisha fujo kwetu. nakumbuka miaka 80 kwa tuliokulia bushi miaka ya ujamaa tulipo kuwa tuki kimbia mchakamchaka asubuhi tuliimba hivi "Nawe banda wa malawi kutuvalia ngozi ya simba na kututishia watanzania hatujali hatujali"wimbo huu hadi leo umenifanya kila nimuonapo mmalawi namuona kama adui wa mtanzania. Nikiwa nje ya tz bado malawi sihesabii.
 
Mazee mie sishangai sana sophia banda ku anzisha fujo kwetu. nakumbuka miaka 80 kwa tuliokulia bushi miaka ya ujamaa tulipo kuwa tuki kimbia mchakamchaka asubuhi tuliimba hivi "Nawe banda wa malawi kutuvalia ngozi ya simba na kututishia watanzania hatujali hatujali"wimbo huu hadi leo umenifanya kila nimuonapo mmalawi namuona kama adui wa mtanzania. Nikiwa nje ya tz bado malawi sihesabii.

usemalo ni sahihi, bali viongozi wetu waleo wamesahau kuwa malawi bado anauadui nasisi, wamebweteka, walitakiwa kuhakikisha sophia banda na chama chake hawaingii ikulu. Kosa wamelifanya, je; watarekebisha?!.
 
Wewe Gama, peleja Umalawi wako huko Blandaya! Unamtisha nani au unamdanganya nani? Eti kuna wamalawi hapa Tz frm Ikulu,Tiss mpk boys and house girls? Hata kiswahili chako inaonyesha ww ni Mmalawi! Kawaambie nduguzo kuwa sisi Wtznia inapofika suala la Utaifa; hakuna wa chadema, ccm au rangi, kabila au atokako mtu; Sote tunashikamana hatuna masiara na maslahi na mustakabali wa nchi yetu Mama Tanzania! Sasa ngoja maana kama sio kesho ni keshokutwa mtakataa tamko letu alafu tuwashikishe adabu ndo utajua umoja wetu na ushirikiano wetu ulivyo! Peleka taarifa hii kwa mkeo na wote waliokutuma! Poof rubbish!!!!
 
Hapana kaka, si rahisi kama unayodhani; Jaribu kusoma kidogo historia, mgogoro huu si wa leo wala jana, na Wamalawi wamekuwa wakiamin kuwa Ziwa lote ni la kwao, isipokuwa sehemu inayomilikiwa na Mozambique! Kwa vile Watanzania hatuna viongozi wenye msimamo tumekaa kimya mpaka yalipotokea masuala ya mafuta ndy tunaona ziwa ni la kwetu pia! Tofauti na hapo tulikuwa hatuna shida na Ramani wanazofundishwa watoto wa Malawii kuwa ziwa ni Mali yao Tanzania hawana chao!!! Ukifanya search ya Harakaharaka Google utapata kuona Ramani nyingi zinaonesha Tanzania haina kipande chochote katika hilo ziwa: https://www.google.co.tz/search?q=m...JyKFYTj4QSZrIFw&ved=0CF0QsAQ&biw=1024&bih=578

Hata Google Map wameonesha Ziwa lipo nje ya mipaka ya Tanzania!

Miaka yote hiyo Tanzania imekaa kimyaa!

Wenzenu wanaendelea na kazi Ziwani nyie mnakenua meno, haya mkawang'oe sasa kama Nia mnayo, Sababu Mnayo, na muangalie kama Uwezo pia mnao! Kama ni vita, atakayeanza kurusha risasi ni Tanzania! Act wisely.

Na tutarusha kweli! Kama ww ni mmalawi huna bahati na kama ww ni mtzn basi ww ni msaliti na punguani! Hata hatua moja haichukuliwi!
 
Malawi vowed Tuesday to press on with oil and gas exploration on Lake Malawi, dismissing a demand by Tanzania, which claims half of the lake, to halt prospecting.
"We categorically put it to them (Tanzania) that as far as we are concerned, the entire lake belongs to Malawi," Patrick Kabambe, principal secretary in the ministry of foreign affairs, said in a statement.
"So our view is that there is no reason to stop the project," he added.
Tanzania has claimed that 50 percent of the lake which forms its border with Malawi is part of its territory.
Tanzanian Foreign Minister Benard Membe last week told domestic media that "exploration activities in the northeast part of the lake should be shelved to pave way for the ongoing discussions to resolve the crisis."
Malawi, a former British colony, and Tanzania, once ruled by Germany, are due to hold talks on the disputed border in the northern Malawian town of Mzuzu on August 20.
Kabambe cited a 1890 agreement between the former colonial powers that stipulates the border between the two countries as lying along the Tanzanian shore of the waters of Lake Malawi.
"Our terms are very clear on this, but we will continue to engage with Tanzania as a good neighbour," Kabambe said.
Mozambique also owns part of the lake.
In September last year, the government of Malawi's late president Bingu wa Mutharika awarded a British firm, Surestream Petroleum, a licence to prospect for oil and gas on the giant lake.
The company has been conducting an environmental impact assessment.
The 29,600 square kilometre lake is Africa's third-largest freshwater lake. In Tanzania, the lake is called Lake Nyasa, which is taken from Malawi's colonial name.

Malawi vows to continue oil-gas exploration on disputed lake Malawi | www.malawitoday.com
 
Tanzania
The Tanzanian People's Defence Force (TPDF) is the least threatened of the
Front-line armed forces, since, in geographical terms, Tanzania is really an East
African, not a Southern African state. However, Tanzanian foreign policy has
long been enmeshed in Southern African affairs as a result of President Nyerere's
philosophy of Pan-African liberation. In addition, Tanzania does border both
Zambia and Mozambique, The TPDF is a much more competent military force
than either FAPLA or FAM. The Tanzanian Army has had long experience in
training guerrillas and in the financial and logistical requirements laid down by
the Tanzania-dominated O AU Liberation Committee. Operationally, Tanzanian
troops were deployed defensively in Mozambique during the Rhodesia-
Zimbabwe war and some 300 military training personnel still operate there and in
the Seychelles. Moreover, the Tanzanian Army is one of the few African armies to
have had a taste of conventional warfare. In 1978-9, 10,000 Tanzanian troops
demolished with methodical skill Idi Amin's Ugandan Army and easily routed
some 2.000 Libyan troops supporting the Ugandans.26 Nevertheless, there are real
impediments to Tanzania's participation in a major Front-line State security role
in the form of severe economic problems, distance, logistics and insufficient airlift
capacity to project force. Most importantly, perhaps, Tanzania is not physically
threatened in the true geostrategic 'front line' against South Africa.
 
Someni makala iliyoandikwa na Ndugu JAMES ZOTTO

Sakata la mpaka kati ya tanzania na malawi: POLITICS VERSUS FACTS

Ndugu zanagu, huenda mnafuatilia vizuri tatizo la mpaka wetu wa ziwa nyasa na malawi! Nilishtushwa sana na hotuba ya bwana waziri. mimi napenda utaifa wangu na uzalendo wangu. lakini napenda sana kutetea mambo yangu kwa kuukubali ukweli, kujua facts zaidi, kukubali hata zile zinazonipinga na ndipo najipanga kujenga joja.

Eneo hili nafanyia study yangu ya PhD. Sidhani kama nipo sahihi zaidi na lengo langu si kusema nani anamiliki nini! Ukweli naoufahamu, tatizo si kubwa kivile kama tunavyolifikiri kama tutachukua muda kupitia documents zote na muhimu. Tunahitaji kwenda Public Records Office-Uingereza, Colonial Archives Potsdam, ujerumani, pia malawi national archives, tanzania national archives, libraries za UDSM na Chancellor college malawi. naamini ubishi utaisha kwa kuwa documents zote zipo.

Angalizo: ziwa nyasa liligawanywa na mabeberu wa kiingereza, kijerumani na kireno. mkataba wa 1890 uitwao anglo-german agrrement unasema mpaka wa German east africa(tz bara ya leo) na nyasaland(malawi ya leo) unapita kandokando ya ziwa nyasa kutoka mto ruvuma mpaka mto songwe! huu ni mkataba wenyewe, upo ktk documents nyingi sana.....!!international law inajua hili na international lawyers wanaelewa nini nazungumza! Sehemu nyingine ilikuwa ni 1891 kati ya ujerumani na ureno, mpaka ulianzia mto ruvuma kuelekea Portuguese east africa(msumbijin ya leo) na pia ureno ikawekeana mpaka na british nyasaland(malawi)...kwahiyo, kipindi cha ujerumani, mpaaka unasomeka 'it passes along the shore of the lake(nyasa).....

Mabadiliko ya mipaka: kipindi cha kikoloni, kabla ya mjerumani kuondoka, marekebisho ya mipaka yalifanyika kati ya mjerumani na mreno kwa kuspgeza mpaka mbele 0.5 KM from the original tripartite point, na vijisiwa vya mto ruvuma vikagawanywa. mpaka leo ipo hivyo. na eneo lingine ni kati ya mwingereza na mreno, ambapo, kisiwa kilichopo eneo la malawi linamilikiwa na msumbiji mpaka leo na eneo la ardhi lililopo msumbiji linakaliwa na malawi. mhuo ulikuwa mkataba wa marekebisho na ipo hivyo mpaka leo. kwahiyo, tulivyorithi mipaka, tumerithi na mabadiliko haya na hivyo hatuwezi kugombana na msumbiji wala msumbiji hawawezi kugombana na malawi. Mpaka wetu na malawi haukurekebishwa popote pale mpaka mjerumani anatoka...

Marekebisho ya mipaka kipindi cha uingereza: sote tunajua german east africa, sisi pamoja na ruanda na urundi tuligawanywa katika sehemu mbili, ttukiwa chini ya League of nations tukiangaliwa na uingereza. Kunamabo nahitaji tuweke sawa. tukaitwa mandated territory na uingereza ni mandatory power. turudi ktk kamusi tutofautishe a an annexed colony and a mandate! Mpaka ukawekwa kati ya ubelgiji na uingereza, uliitwa the MILNER-ORTS AGREEMENT OF 1922! katika mkataba huu, mto kagera ulikatwa katikati na mpaka leo tumerithi hivyo. Hapakuwa popote pale ambapo eneo la ziwa nyasa lilirekebishwa kwa njia ya mkataba baina ya nyasaland state na tanganyika state...., isipokuwa, tofauti na mandates zote, tanganyika pekee, ilikuwa na tofauti ndogo, ambapo, mpaka wa ziwa nyasa ukapewa wanachoitwa 'wording', na hivyo, ramani ya tanganyika na official records zikaonyesha kuwa mpaka umepita katikati ya ziwa nyasa! na hapa ndipo tatizo linapoanza na sisi tumechukulia hii ndo absolute fact, hatuendi mbele kidogo. haya yapo pale national archives secreatarita files, ACCESSION NUMBERE AB 8 na AB 30! nafikiri hotuba yote ya bwana mkubwa jana imetoka ktk files hizi, ndizo walizopelekewa!!!

twende mbele kidogo, ni kweli, kama mheshimiwa alivyosema jana, ramani nyingi kuanzia 1922 mpaka 1939 zinaonyesha mpaka upo katikati ya ziwa! je, ukweli huu utatutosha pekee mbeleni tukifikishana mbali? hapana!mheshimiwa hakusema kuwa ramani zingine, japo chache muda huu huu na official reports hazionyeshi mpaka au zinaonyesha mpaka upo chini. lakini ni chache! kwanini hili?bado natafuta majibu, lakini kwa harakaharaka, unaweza ukasema kuwa uingereza ilitamani tanganyika iwe koloni lake na si mandate! na pia ilishinikizwa na wawekezaji na hata jeshi ilisema afadhari waiteke ili liwe koloni na waachane na mandate! nahitaji tuelwe maana ya mandate.

Hii yote ilitokea baada ya Donald Cameroon, governor wa tanganyika kusema kuwa tanganyika is a part of the british empire and it will remain so! hii ni siasa na si ukweli kama unaelewa maana ya kuwa wao hawakuwa wamepewa koloni kama mali yao, bali kuliangalia mapaka wananchi wapate 'akili' ili wapewe uhuru! kwa hiyo, kimsingi, kwa maana ya sheria ya kimataifa, tanganyika haikuwa part ya british empire kama yalivyo makoloni yaliyotekwa mojakwa moja na uingereza yenyewe! hapa pakatokea mvutano mkubwa sana katika house of Lords na house of commons! na hivyo basi, mtafaruku huu wa mpaka ulianzia hapa, kwa kauli hii na hivyo hata waingereza wenyewe walivutana kuhusu mpaka. ipo hivi, mwaka 1926, wajumbe wa mabaraza waliibana serikali iseme mipka ya tanganyika na ule wa ziwa nyasa! mabishano, kama haya yetu leo yalikuwa makubwa, ila si kwa kutishiana kwa kuwa walikuwa wenyewe na walitaka kuwekana sawa! ndipo secretary of state for colonies alibanwa na mjadala ulikuwa wa kisheria zaidi ukihoji status of the mandate, british empire, n.k; na kama waingereza wanamamlaka ya kujipangia kuhusu koloni waliolokabidhiwa kuliangalia(nieleweke na si kulimiliki)! mwishowe, mtu huyu mwenye dhamana alisema kwamba, hata yeye anashindwa kuelewa, 'what exactly is the sovereignty of tanganyika lying'! jamani mnamwelewa huyu mtu? kwamaana hiyo, haelwi vizuri mipaka yetu, ambayo wenyewe ndo wameirekebisha au kuipa 'wording'!! hivyo, tatizo linaanzia hapa na si muda mwingine wowot!!!

Kipi hakusema bwana mkubwa jana: kuanzia 1939, mambo yalibadilika na hawa hawa watu tunaochukua ashahidi kutoka kwao, wakafanya madudu! na ilipoisha vita ya pili ya dunia, jamani oneni haya, hawa waingereza katika ramani zao, tena nyingi mno,(kaangalieni East africana section, university of dar es salaam, sehemu ya thesis, kuna cabins 3 zimejaa ramani na bado ni mpya sana kutokana na kutunzwa na pia kutotumka sana), kuimbezinaonyesha, bila shaka yoyote, kuwa mpaka wa tanganyika na nyasaland unapita pembeni mwa ziwa na si katikati! mkuu hakusema hili. aliishia 1939! kumbe hawa jamaa walichora tena ramani zote zikionyesha mpaka upo pembeni mwa ziwa!!!! kwanini hili?natafuta majibu, lakini nkwa haraka naweza nikaspeculate mawili. mosi, karibu na vita vya pili vya dunia, ilisikika tetesi kule duniani kuwa, ujerumani inarudi na inakuja kuchukua malokoni yake. (kasome national archives of tanzania, secreatariat files zote zenye kichwa cha habari, 'the future of tanganyika in british empire'). kwa hiyo, waingereza walihofia kutimuliwa na kurudi kwa wajerumani, na hivyo, wakarudisha ule mpaka wa awali wa 1890! na pia, muda huu, baada ya kwisha vita, tanganyika ikawa chini ya UNO ambapo ilipewa trusteeship status!maana ya hii ni rahisi kuliko mandate!ilimaanisha to be granted immediate independence! maana ya neno immediate hapa ni kwamba, kwa tafsiri yangu, waingereza wlifahamu wanatimka mapema mno kwani mkataba unasema hivyo....nafikiri, wakarudisha ramani zikionyesha mpaka upo pembeni...na kitabu ch Nyasaland cha mwaka 1958, kinaonyesha mipaka ya nyasaland na ziwa lote likiwa kwao! tukitaka kuwashinda wamalawi, lazima tukisome vizuri kipindi hiki na tuelewe facts zipi zinawapa kiburi na zipi sisi tuzitumie, la sivyo, tunaweza.............!!!!!!!!!!!!! kwahiyo future of tanganyika ilikuwa contested, uncertain, etc kipindi hiki, pamoja na mipaka yake pia!! tujiulize, kwa maana ya mandate, waingereza walikuwa na legal authority 'kurekebisha' mpaka wa ziwa nyasa? na je makosa waliyofanya waingereza, ndo legal backing yetu sisi? ebu tuzame tena tutafute facts tuwashinde hawa jamaa!

Tulishindwana na uingereza kurekebisha mipaka. mwalimu alisubiri mpaka malawi iwe huru!akatoa miaka mitatu tu na asingetambua mipaka ya kikoloni(soma hansard, 1962). walipopata uhuru, kukawa na matatizo ambayo jana bwana mkubwa aliyaeleza. nampongeza ni dhahiri, 1964 cabinet crisis ya malawi na wale mawaziri kutorokea nchini kwetu kupitia ziwa, banda akaona ziwa ni infiltratio route! sera zetu za mambo ya nje zilikuwa tofauti. tulikuwa frontline state kwa ukombozi, wenzetu wakasapoti makaburu na wareno na wakawa na balozi sehemu hizo.....wakagombana na mwalimu, military show down miaka ya 1967-8; matusi na kejeli zikatawala kati ya mwalimu na banda, sisi na malawi.....kipara cha banda kinamagamba, tuliimba tukiwa jeshini, mwalimu akasema mpaka a sensible leader akitokea malawi ndipo tutajadili tena swala hili na si na kamuzu banda! tulikuwa kimy, na kuanzia 1975, hatukuwa na tatizo,lakini si kusema kuwa tulitatua tatizo la mpaka!

Tulikaa kimya!mipaka haina tatizo isipokuwa ni time bomb ambapo ikitokea spark ni explosion! Tuliirithi kupitia Article III ya OAU CHARTER ya 1964 BAADA YA DEBATES KUBWA NA WENGI WAKARIDHIA TUIRITHI, uti possidetis, ita possidetis principle (so as you exist, so may you exist), kama kawaida yetu tulidesa ya kibeberu, Westphalia principle, border inviolabiliy! hatukupata muda mwingi wa kutafakari na kuangalia kila mpaka na matatizo yake....tulirithi na matatizo na yanatutatiza leo!!!

Way forward! naikiri tuna namna tatu ya kulimaliza! moja ni kwa majadiliano ya kawaida yaani diplomacy kama bwanamkubwa alivosema jana. pili ni kupigana vita. (war is another means of diplomacy), mnataka kuniona kichaa!huo ndo ukweli, atakayeshindwa atasalimu kama ilivyokuwa kwa uganda na sis. tatu ni mahakama ya kimataifa yaani International Court of Justice! hapa ninawasiwasi. kama facts zenyewe ni zile za jana tu, sijui kama tutatoka.tutulie, tuite wataalamu wetu wajikite ndani sana. ni kweli kama alivyosema jana bwana mkubwa kwa kunukuu kesi nyingi na zilizoshinda, na kwa kusema kuwa, tukienda mahakama ile sisi ndo tutashinda!!!ninashaka....tumejipa favour ya verdict! kabla ya kesi.sijui.ninashaka kubwa!kunakushinda, kushindwa au suluhu!ninashaka tena na tena!

mimi nimzalendo,nataka ukweli kwa njia ya mahojiano na kuumiza kichwa, tutetee mali zetu tukijua tunawashinda kwa hoja.....!!!!

Wasiwasi: inasemekana kuna mafuta ziwani!!! kwahiyo mjue marekani na washirika wake hawako mbali! tujue operation ya military imperialism na huyu mama, mpwa wa kamuzu banda, anapata wapi hiki kiburi...nyuma yake kuna nini na nani!!1tuangalie haya pia.

Hitimisho. tusiwe na hoja moj tu mkononi kama ndo water-tight evidence. tujaribu kuzibishanisha hoja zetu. na hoja nzuri ni zile zinazopingana nasi na tusizozipenda, tukizielewa na kuzikubali ndipo tutajipanga namna ya kuzigalagaza. tumwelewe vizuri adui yetu.....MUNGU IBARIKI TANZANIA!ZIWA NYASA!WANYASA!WATANZANIA!

Tusing'ang'anie tu REPARIAN LAW!
 
Lake Malawi belongs to Malawi as per treaty. Every map I have ever seen agrees with this position. I fully support Malawi's position. Hopefully they can find oil and other resources inside that Lake, that can help uplift the living standards of their wonderful people.
Thats a very shallow observation.
The heligoland Treaty did not focus on Lake Malawi, it was a "Temporary" agreement mainly to define the Northern border between German East Africa and British East Africa's "Sphere of Influence". Spheres of influence are lands, not interterritorial waters, unless there's an island in those waters, then the dermacation line will be formed. That's why british and German soldiers marched up to 1 degree line on lake victoria, so that German East Africa can have Ukerewe, the same was done with the mocambican border because they had islands in between.

Since we don't have habitable islands between us, Lake Nyasa was considered to have a status of "International" waters and German and British had their gunboats roving arround up to 1914, when Hedwig Von Hossmann was blown as the first Naval engagement of the first world war.

Malawi will never own the whole Lake, until all Tanzanians are dead. The Heligoland treaty was never meant to give Lake Nyasa to Malawians, and if you peruse The British House of commons Hansard dated March 24, 1959 there you will find how the lords back in England view Nyasaland as being the country laying on the belt "along" the Western shore of Lake Nyasa.

Malawi will always be a "Shame" to mother Africa,
A nation full of cry babies, owning Islands on Mocambican waters (like your fellow B!#@es Kenya on Migingo), and made believe by your God, Kamuzu that you own the Lake and part of our land.

Please do us a favor, shut the hell up and keep tending to our gardens, and babysitting our kids, we appreciate having maids who speak English but please don't start nothing, It won't be nothing.
 
Pengine kuna mbabe ambaye anamchochea MALAWI ili aanzishe vita na TANZANIA halafu yeye apate njia ya kupita kwa kumsaidia MALAWI,halafu aje TANZANIA kubeba hata madini mengine maana pengine ameona hiyo itakuwa rahisi sana,kwa hiyo kumpiga MALAWI itategemeana na nguvu ya msaada anayopata
 
Malawi will always be a "Shame" to mother Africa,
A nation full of cry babies, owning Islands on Mocambican waters (like your fellow B!#@es Kenya on Migingo), and made believe by your God, Kamuzu that you own the Lake and part of our land.

Please do us a favor, shut the hell up and keep tending to our gardens, and babysitting our kids, we appreciate having maids who speak English but please don't start nothing, It won't be nothing.

now now....are you on heat or are civil exchanges a demenor to your ego? Son you lack respect!!!!! Infact you talk like a street urching. Very dissappointing for a full grown man throwing collossal tantrums/abuses/bigotry and alot of childish enthusiasm only because one person aired his views which btw are modest in any scale. We dont talk shit about Tz but theres alot of dung about her but we ignore. Respect Kenyans, respect the mothers that bore this blood. SHAME ON YOU!!!!
 
now now....are you on heat or are civil exchanges a demenor to your ego? Son you lack respect!!!!! Infact you talk like a street urching. Very dissappointing for a full grown man throwing collossal tantrums/abuses/bigotry and alot of childish enthusiasm only because one person aired his views which btw are modest in any scale. We dont talk shit about Tz but theres alot of dung about her but we ignore. Respect Kenyans, respect the mothers that bore this blood. SHAME ON YOU!!!!
Why would I respect a (bad word) like you? Or a country like yours?
I've said it before and I'm sayin' it right now, Kenya and Malawi will always be a "Shame"
to Africans (black Africans).
ALWAYS!!!
 
Hamna cha mpambe wala nini huyu mama anataka atutambue wananch wake kwanza chakula chenyewe kinawashinda, huyu mama kama akitaka itamnyeshea ya masika na cyo ya rasharasha kwa sababu choppa tunazo mazee.
 
Mbona wa tz tunaongea sana kuhusu vita na Malawi? Kwani Malawi walishajibu lolote kwamba wameonyesha jeuri? Kwamba wamekataa kuzungumza kuhusu mgogoro wa mpaka? Kama bado Malawi haijasema chochote kwa nini viongozi wetu wanaendelea kutoa matamko ya vita? Au ni rahisi sana kuongea tu kwa kuwa athari za vita hawataziona wao bali masikini wa nchi hii, kina mama na watoto? Yaonekana kama vile watz tuna hamu sana na vita! Hii haijakaa vizuri hata kidogo.
 
Hii thread ungeifanya comment humuhttps://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/304695-wanasiasa-na-lugha-ya-vita-hekima-ya-kupunguza-sababu-ya-kuingia-vitani-na-malawi.html#post4392726
 
Back
Top Bottom