Malaria imekimbilia tumboni

sajosojo

JF-Expert Member
Apr 14, 2010
1,017
619
Msaada tafadhari nina maralia imekimbilia tumboni upande wa kushoto or kwenye bandama tumbo linaniuma sana
 
kapime uanze kutumia dawa mkuu usifanye utani na bora umefaham ni malaria..mi hii kitu ilitaka kunitoa uhai tumbo liliniuma nikawa nahahrisha mfululizo nikadhani nimekula uchafu. Nilikomaa na dawa za tumbo bila mafanikio kuongea na kulalamika ndo kulinisaidia.. Wadau waliniambia kapime+malaria.. Na kweli bana baada ya kuanza dozi tumbo likapoa..
 
Ndugu, pole sana na kuumwa.
Vijidudu vya malaria vikiingia mwilini vina stage kama 4 hivi, vikibadilishana kati ya damu na kwenye ini (liver). Sina hakika unamaanisha nini na umejuaje kama malaria imekimbilia kwenye bandama (na sio kweli). Nina hakika unahitaji kwenda hospitali upate matibabu sahihi. Ni kweli malaria inaua kuliko ukimwi, usizembee.
 
Msaada tafadhari nina maralia imekimbilia tumboni upande wa kushoto or kwenye bandama tumbo linaniuma sana

Hakuna malaria ya tumboni. After all umejuaje kuwa ni malaria? Note: different unrelated infections could have similar symptoms/signs presentation. To be on the safe side, nenda hospitali upate majibu ya madaktari.
 
Msaada tafadhari nina maralia imekimbilia tumboni upande wa kushoto or kwenye bandama tumbo linaniuma sana
Naona sasa madaktari mmeanza kuwa wengi. Wenzenu wanasoma zaidi ya miaka mitano ili walau wapate degree za kwanza ya udaktari; wewe waamka tu na kuanza kusema malaria imekimbilia huku na kule. Unajua pathophysiology ya malaria wewe? Au na wewe umeanza uwongo wa Dr. Ndodi? Hebu nenda hospitali wewe, usije fia hapo kitandani.
 
Back
Top Bottom