Malaria 150: wataalam hebu tuelewesheni hii kitu.

DASA

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
1,031
301
Habari members, Jamani mimi nikipata malaria 4 ni balaa nahisi kufa, Hali inakuwa mbaya sana. Zamani sana kuna jirani yangu alikuwa na 100, nilishangaa sana, alikuja kupona kwa shida sana, Sasa najaribu kufikiria wadudu 100-150, na hii sidhani kama ni kitu cha kawaida, Huyu mtu imekuaje mpaka afikishe 100-150. wataalam hebu tupeni elimu ya hii kitu, inakuaje mpaka mtu unafikisha kiasi hicho!!, au kunakuwa na tatizo llingine linalofanya ufikishe kiasi hicho.

Ufafanuzi tu inakuaje mpaka inafika 100-150, na wewe upo kawaida tu.
 
Bwn/Bi Dasa, Malaria 150 ni kawaida sana, wala hai'qualify kuitwa severe malaria kama haijaenda kwenye baadhi ya sehemu za mwili km ubongo, ini, figo n.k
Kichwa kuuma sana inaweza kuwa dalili ya maambukizi/matatizo mengine ambayo yanaweza kusababisha pressure ndani ya system ya ubongo na uti wa mgongo kupanda!
Na uelewe kwamba mpaka sasa dawa nzuri zaidi ya malaria ni Artemether pamoja na Quinine ambazo zipo nyingi sana hapa nchini, hivyo ukiona mgonjwa hapati nafuu kwa dawa hizo ni lazima ufikirie magonjwa mengine pia!
 
Kawaida vijidudu vya malaria (malaria parasite) huesabiwa ukilinganisha na idadi chembe nyeupe za damu(white blood cells),majibu tuliozoea idadi ya chembe nyeupe za damu huwa ni 200 kwa mfano mtu mwenye malaria 4 kawaida inamaanisha huyu mtu vijidudu vinne vilionekana katika chembe nyeupe za damu 200,sasa kama vijidudu 150 vimepatikana katika chembe nyeupe za damu 200 ni malaria kali sana lakini kama vijidudu hivyo 150 vimeonekana katika chembe nyeupe za damu nyingi zaidi kwa mfano katika chembe nyeupe za damu 50000 hiyo nikawaida si ya kushangaza,so inategemea hao malaria parasites walihesabiwa per how many white blood cells, thats ol i know
 
Mwenye vijidudu vya malaria 150, vigawanye kwa 40 i.e around malaria 4 hivi. nilwahi kudokezwa na dk mmoja wa hospitali kubwa hapa Tz.
 
Kawaida vijidudu vya malaria (malaria parasite) huesabiwa ukilinganisha na idadi chembe nyeupe za damu(white blood cells),majibu tuliozoea idadi ya chembe nyeupe za damu huwa ni 200 kwa mfano mtu mwenye malaria 4 kawaida inamaanisha huyu mtu vijidudu vinne vilionekana katika chembe nyeupe za damu 200,sasa kama vijidudu 150 vimepatikana katika chembe nyeupe za damu 200 ni malaria kali sana lakini kama vijidudu hivyo 150 vimeonekana katika chembe nyeupe za damu nyingi zaidi kwa mfano katika chembe nyeupe za damu 50000 hiyo nikawaida si ya kushangaza,so inategemea hao malaria parasites walihesabiwa per how many white blood cells, thats ol i know

kwahiyo 160 = 4!
 
Madaktari ndani ya nyumba tufahamisheni kwa uzuri ili swala la vijidudu 150 etc. Jamani we are used to vijidudu 1,2,3 na 4...rarely nimesikia vijidudu 20
 
DASA;2727037]kwahiyo 160=4!

sijaelewa swali

naanza kusiki kizunguzungu sijui itakuwa ngapi! manake madakitari wanatoa maelezo kila mmoja na lake, au fani ya uganga haijitoshelezi?
 
bia za usiku wa manane huku mbu wakifanya mashambulizi miguuni zitawaondoa kabla ya siku zenu!
 
DASA;2727037]kwahiyo 160=4!

sijaelewa swali

kutokana na maelezo yako ya awali, nadhani unamaanisha malaria 150 ni sawa na 4 tu. hapa umeniacha mkuu, ina mana mtu mwenye 9 ni sawa na 9x40=360. sasa ina mana hawa muhimbili wao utaratibu wao wa kutoa majibu ni tofauti na wengine au!.
 
no D hujanielewa.niliandika kuwa usually malaria parasite (mp)huhesabiwa per 200 white blood cells (wbc's) so kama walihesabu wakapata 150mp/200wbc's ikimaanisha katika wbc's 200 wameona malaria parasite 150 that means ni malaria kali,kwa uelewa wangu mdogo najua hvo, cjui umenielewa mkuu!
 
kutokana na maelezo yako ya awali, nadhani unamaanisha malaria 150 ni sawa na 4 tu. hapa umeniacha mkuu, ina mana mtu mwenye 9 ni sawa na 9x40=360. sasa ina mana hawa muhimbili wao utaratibu wao wa kutoa majibu ni tofauti na wengine au!.

hii huhesabiwa per 200 white blood cells. Sasa kama kwenye kila 200 kuna wadudu 150,na norma range ya WBCs ni 4 to 11 times ten power nine. Nafikiri utagundua kwamba kulikuwa na vijidudu vingi sana ndo maana ikawa severe malaria. Over
 
..Dhana ya kuitazama malaria na idadi ya wadudu(parasite) ni potofu, na hii lugha ya malaria moja, mbili nk imepanda sana chati na ongezeko la utitiri wa maabara za binadamu ambazo (nyingi) uwezo/weledi wa wafanyakazi wake na vitendea kazi vyao ni questionable! Sambamba na hili pia ni ongezeko la hospitali binafsi (za kibiashara). Kifupi ni matokea ya biashara huria. Severity ya malaria haipimwi kwa idadi ya vidudu/parasites (kuna mchangiaji kaeleza) kinachoangaliwa ni parasites wameshambulia mwili kwa kiasi gani (mf. je ubongo , figo nk vimehusika? na hii huangaliwa kwa kum examine mgonjwa na kuangalia dalili zake. Kwa mfano mtoto mwenye malaria inayoambatana na degedege (Convulsion) husemwa kuwa na malaria kali (severe) na suala la parasite wangapi per WBcs halina umuhimu hapa. Pia Vipimo kama renal function test, Liver function test nk huweza kusaidia. Mfano mtu mwenye malaria na dalili za kuchanganyikiwa (altered mental state) huyu ana malaria kali hata kama ana malaria moja! (I hate this language, malaria moja!?$#**). Mwisho, severity ya malaria pamoja na mabo mengine inategeme sana previous exposure ya mtu kwa ugonjwa wa malaria; yaani, je ulishawahi kuugua kabla? Ndio maana, watoto wachanga chini ya miaka 5 ndio wanaokufa na malaria zaidi kwa malaria na pia watu wanaotoka nje ya malaria endemic areas(maeneo yenye ugonjwa) e.g. Europe, nk wakiugua malaria huwa severe zaidi. wanaojua zaidi wanaweza kuongezea......Nitarudi on this thread ueleza pia mama mjazito na malaria
 
.... Severity ya malaria haipimwi kwa idadi ya vidudu/parasites (kuna mchangiaji kaeleza) kinachoangaliwa ni parasites wameshambulia mwili kwa kiasi gani (mf. je ubongo , figo nk vimehusika?
Kwa hiyo wewe unatumia vipimo gani ku assess level of severity ya Malaria?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom