Malalamiko yangu kwa watu maarufu dhidi ya kesi ya Mbowe

monde arabe

JF-Expert Member
Oct 22, 2017
8,486
13,017
Habar za muda huu ndugu wanajukwaa,zimepita siku kadhaa sasa tangu Mh.Freeman Aikaeli Mbowe alipotekwa na kuwekewa madawa ya kulevya pamoja na bastola kisha kupelekwa kwenye vyumba tofauti tofauti vya mateso na hatimaye kupelekwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Kwa wale ambao hawafahamu ukweli kuhusu kesi ya FAM (Freeman Aikaeli Mbowe) ukweli ni huu

Kabla Magufuli hajafariki uliandaliwa mkakati wa kuua chama cha Chadema kwa kupandikiza mtu wa ccm kwenye nafasi ya Mwenyekiti na hapa aliandaliwa Cecil Mwambe akiwa ni Mbunge wa jimbo la Ndanda. Kwa kuwa intelijensia ya CHADEMA ipo imara Mwambe akashtukiwa so, mpango ukakwama wa kumpandikiza Mwambe kama Mwenyekiti wa Chadema (hapa Mwambe angekuwa anaongoza chama kwa maelekezo ya ccm so, Chadema ingekuwa ccm B).

Pia, kabla Magufuli hajafa, ulifanyika mkakati wa kumnunua Mbowe lkn,wakashindwa kumnunua kama walivyoweza kuwanunua wabunge na madiwani wengine kutoka Chadema.

Baada ya mambo yote hayo kushindikana likapelekwa file kwa Meko likiwa na agenda ya kumfunga Mbowe. Kwa bahati mbaya sana Meko alikataa agenda ya kumtengenezea kesi Mh. FAM lakini, inadaiwa alisema "jambo hili litatuharibia kwenye macho ya kimataifa ni bora akapigwa risasi hadi kufa then, tutasema aliuawa na watu wasiojulikana".

Kwa hiyo kesi ya FAM,ni muendelezo kutoka kwenye file la zamani alilopewa Meko na kulikataa lakini, kwa bahati mbaya sana file lile lilihifadhiwa kwenye Wizara ambayo sasa ipo kwenye mikono ya Mkwe wa Mama so, alichofanya Mkwe ni kutumwa tu kabatini na kulichomia file na kuanza kulifanyia kazi upya!

Baada ya kupata utangulizi kuhusiana na kesi hii,sasa naomba niwageukie ninyi watu maarufu hapa Bongo Tanzania (watu maarufu kutoka kwenye tasinia tofauti tofauti kama vile Bongo movies, Bongo flavour, football, waandishi wa habari na watu wa kada nyingine).

Tangu FAM, alipotekwa na kupelekwa Kisutu ninyi watu maarufu hapa Tanzania (hapa tunamtoa Ney wa Mitego) wote mmekaa kimya kuanzia wasanii wa Bongo movies kama vile akina Ray, Wema Sepetu na wengineo lakini, pia wasanii wa Bongo flavour kama vile Mond Platnumz na wengineo mmeamua kukaa kimya kama vile hakuna kitu kibaya kinachoendelea kwenye nchi yetu.Wako wapi wasanii wa kaliba ya Bob Marley, Fela Kuti (the King of Afro beat) na Franklin Boukaka?

Ninyi mnataka sisi tuje kwenye matamasha yenu,mnataka mkiumwa au kupata matatizo sisi kama jamii mnataka tuwachangie. Kumbukeni tulivyowachangia Sajuki na Wastara na wengineo lkn,leo mtu muhimu katka jamii aliyebeba ndoto na dira ya Taifa anatekwa na kupewa kesi mshenzi wote mpo kimya itafikia mahali kila kundi sasa litaanza kupigana vita kivyake.

Ninyi wasanii na watu maarufu kumbukeni CCM ndiyo walioweka mifumo mibaya na hiyo ndyo inayowafanya ninyi kuwa masikini kwa mfano issue ya hatimiliki kwa kazi za sanaa bado ni kitendawili hadi hivi leo. Ninyi wasanii mkifa hivi leo familia zenu zinadhulumika kutokana na sera mbovu za ccm kwenye kazi zenu. Kama Taifa tunawatazama wakati wenu waja ambapo mtalia na kusaga meno.

Asanteni sana!
 
Wafute kisa nini sasa?

Tundu lisu aliulizwa swali, wewe unataka uone tanzania ikifika wapi?
Unajua alijibu nini...

Achana na hilo, ninaloweza kusema ni kwamba..
Sisi watanzania tulio wengi niwa jinga sana.
 
Kuna watu wanakufa kwa sababu ya kubeba laana na machozi ya watu,yu wapi Ben Rabiu Saanane, Kamanda Mawazo na Azory Gwanda?
Nani aliharibu uchaguzi wa 2020?

Sent from my TECNO-N8 using JamiiForums mobile app
Kuna uchaguzi ambao kwenu uliwah kuwa mzuri? Ngoja 2025 ukipata si mtasahau kama kama ulikuwepo wa 2020 pia? Uchaguzi wa upinzani kushinda ulikuwa wa 2015 tu!

Kama ilishindikana pale sioni tena mkisimama ata sasa sioni mkiwa agenda zakuwashika wananchi zaidi mnacheza singeri tu 2025 mje kusema tena ulikiwa uchafuzi sio uchaguzi.
 
imya kuanzia wasanii wa Bongo movies kama vile akina Ray, Wema Sepetu na wengineo lakini, pia wasanii wa Bongo flavour kama vile Mond Platnumz na wengineo mmeamua kukaa kimya kama vile hakuna kitu kibaya kinachoendelea kwenye nchi yet
Hizi i takataka tu!
 
Back
Top Bottom