malalamiko ya Rais kwa wafanyakazi

Michael Chairman

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
922
583
1. Kuwepo kwa wafanyakazi Hewa ambao kwa takwimu alizozipata jana ni wafanyakazi hewa 10295 ambao kwa miaka mitano wamelipwa bilioni 699 na kwa bilioni hizi zingetosha kujenga madaja ya kigamboni matatu n.k
2. Hotuba ya katibu mkuu wa Tucta imeshindwa kulaani sakata la wafanyakazi hewa nimeshangaa sana.
3. Mbaya wa wafanyakazi ni wafanyakazi wenyewe , hii ni kwa wale ambao wameendelea kuchukua mishahara ya wafanyakazi hewa.
4.Inasikitisha sana maana kuna wakati huwa najiuliza kwanini niliomba urais.
5. mbona makao makuu ya TUCTA yapo mnazi mmoja Dar es salaamu , huku akiomba serikali ihamie Dodoma.
6.kuna vyama vingine (vya upinzani) vinaomba serikali kuhamia Dodoma hali ya kuwa vyenyewe havina hata makao makuu Dodoma nakipongeza chama cha mapinduzi.
HAYA NI SEHEMU TU YA HOTUBA YA RAIS HUKO DODOMA LEO KWENYE SIKU YA WAFANYAKAZI.
 
Raisi JPM, kajitolea nafsi yake ... ili aokoe taifa lililozama katika ufisadi ulotukuka!!
Pole sana Rais wa JMT!!
 
Nimemshangaa sana rais Magu kwa kuwalalamikia wafanyakazi hewa na eti wanapaswa kulaaniwa. Mimi nilidhan alipaswa awalaani hawa waliotengeneza wafanya kazi hewa . Mfano unamlaumuje marehemu anayeendelea kulipwa? Nani anamlipa. Hivyo badala ya kulaumu wafanyakazi hewa ambao kimantiki hawapo, walaumiwe wasimamizi na viongozi waliolea hilo. Magufuli amekuwa anakwepa kuxungumxia kiini cha tatizo anahangaika na matokeo!
 
Kuna umuhimu sasa wa kutajiwa wafanyakazi hewa kwa majina yao na mishahara wanayolipwa ili tufahamu huu mchezo ulivyochezwa na nani alikuwa anachukua mishahara hiyo.
 
Dodoma bado sana,hapa tuache siasa,mji mkuu ni Dar es Salaam.Huhitaji kusoma jiografia sana kufahamu hili.Tusing'ang'anize mbuzi kuwa ng'ombe.Dar ni lango na ndiyo sura ya Tanzania.
 
Hili la kigugumizi cha Serikali kuhamia Dodoma ni kichekesho tu na hasa inapo fikia hatua ya wakubwa kuanza kusutana kuwa "mbona nyie hamja hamia" serikali inge chukua tu uamuzi wa kubatilisha huo uamuzi maana kila serikali inayo ingia ina lizungumzia tu juu juu na kujipita,wakati dhamira hasa ilisha ondoka na walio liasisi jambo lenyewe,pale awali serikali ya Nigeria ilipo kuwa ina wazo la kuazisha mji mkuu(Abuja) ili tuma ujumbe na timu za wataalam kuja kujifunza namna ya utendaji wa CDA nakadhalika, lakini cha ajabu mwanafunzi amefaulu ila mwalimu bado anasoma Abuja ime jengwa na imejengeka ni jiji hasa, imekuja Brazil wamehamisha jiji toka Rio de Janeiro kwenda Brasilia wame maliza hapa bado ni hadithi tu ya nyani mvua inapo nyesha ndio wana kumbushana kujenga nyumba,ofisi za Balozi zote zilipewa maeneo ya ujenzi ila wamestuka kutaka kufanywa wao wawe chambo, mgeni atangulie mwenyeji aje nyuma uliona wapi,ondoeni aibu kubalini kushindwa,vinginevyo ni Usanii mtupu.
 
1. Kuwepo kwa wafanyakazi Hewa ambao kwa takwimu alizozipata jana ni wafanyakazi hewa 10295 ambao kwa miaka mitano wamelipwa bilioni 699 na kwa bilioni hizi zingetosha kujenga madaja ya kigamboni matatu n.k
2. Hotuba ya katibu mkuu wa Tucta imeshindwa kulaani sakata la wafanyakazi hewa nimeshangaa sana.
3. Mbaya wa wafanyakazi ni wafanyakazi wenyewe , hii ni kwa wale ambao wameendelea kuchukua mishahara ya wafanyakazi hewa.
4.Inasikitisha sana maana kuna wakati huwa najiuliza kwanini niliomba urais.
5. mbona makao makuu ya TUCTA yapo mnazi mmoja Dar es salaamu , huku akiomba serikali ihamie Dodoma.
6.kuna vyama vingine (vya upinzani) vinaomba serikali kuhamia Dodoma hali ya kuwa vyenyewe havina hata makao makuu Dodoma nakipongeza chama cha mapinduzi.
HAYA NI SEHEMU TU YA HOTUBA YA RAIS HUKO DODOMA LEO KWENYE SIKU YA WAFANYAKAZI.

Serikali ina kila kitu kwahiyo tuache kulalamika tuchukue hatua kwa sababu hao waliofanya hayo wanajulikana na akaunti zao zinajulikana zilipo hivyo jambo la kufanya ni kuzifuatilia fedha zetu na kuzirejesha period.......mambo ya kusimama majukwaani na kulalamika yanatupotezea muda
 
Lowassa aliwahi kusema, Mwananchi analalamika, Waziri analalamika, hata Rais naye analalamika...sasa nani amsikilize mwenzake??
Lowassa...ni living legend.
 
Hili la kigugumizi cha Serikali kuhamia Dodoma ni kichekesho tu na hasa inapo fikia hatua ya wakubwa kuanza kusutana kuwa "mbona nyie hamja hamia" serikali inge chukua tu uamuzi wa kubatilisha huo uamuzi maana kila serikali inayo ingia ina lizungumzia tu juu juu na kujipita,wakati dhamira hasa ilisha ondoka na walio liasisi jambo lenyewe,pale awali serikali ya Nigeria ilipo kuwa ina wazo la kuazisha mji mkuu(Abuja) ili tuma ujumbe na timu za wataalam kuja kujifunza namna ya utendaji wa CDA nakadhalika, lakini cha ajabu mwanafunzi amefaulu ila mwalimu bado anasoma Abuja ime jengwa na imejengeka ni jiji hasa, imekuja Brazil wamehamisha jiji toka Rio de Janeiro kwenda Brasilia wame maliza hapa bado ni hadithi tu ya nyani mvua inapo nyesha ndio wana kumbushana kujenga nyumba,ofisi za Balozi zote zilipewa maeneo ya ujenzi ila wamestuka kutaka kufanywa wao wawe chambo, mgeni atangulie mwenyeji aje nyuma uliona wapi,ondoeni aibu kubalini kushindwa,vinginevyo ni Usanii mtupu.
Hata malawi walihamia mji mpya baada ya kupata darasa CDA, kuna pesa nyingi zimeliwa na wajanja hapo CDA kwa kisingizio cha kuijenga Dodoma, wakiamua kufanya Uchunguzi magereza yatafurika wafungwa wa pesa za kuijenga Dodoma, Nchi Nyingi hata Marekani mji mkuu huwa haukai kwenye mji wa Heka heka nyingi sana, hata Africa kusini mji wa kijanja Johannesburg, Daban wameiacha ifanye biashara wao wapo pritoria na bunge lipo capetown ili kusambaza Maendeleo nchi nzima, Tanzania wabunge wote na viongozi wote wapo Dsm hata wakuu wa mikoa, Wilaya huko wanaenda kufanya kazi lakini nyumba zao zipo Dsm, Hiki kioja kipo Tanzania pekee hapa Duniani ni vigumu maendeleo kusambaa mikoa mingine kutokana na Ujinga wa kulundikana Dsm na kuzidisha foleni na misafara isiyokwisha.
 
Dodoma bado sana,hapa tuache siasa,mji mkuu ni Dar es Salaam.Huhitaji kusoma jiografia sana kufahamu hili.Tusing'ang'anize mbuzi kuwa ng'ombe.Dar ni lango na ndiyo sura ya Tanzania.
sura gani? Mvua ikinyesha siku moja mafuriko hakuna mipango miji, Uswahilini kumejengwa hovyo hovyo tu, foleni, misafara ni kero ya kudumu, kwani lazima Serikali ikae Dodoma au Dsm wabadilike waje na wazo jipya ijengwe New Dar-es-salaam katikati ya pwani na Moro au Tanga, wafanye kama india Serikali ilijenga mji mpya kabsa kisha wakazi ndio wakawafuata mji umepangiliwa Vizuri sana, uwe mji wa kisayansi na sheria za kuhamia hovyo na kuweka Uswahilini ziwe kali, watu waishi wa mpangilio mzuri.
 
Kuna umuhimu sasa wa kutajiwa wafanyakazi hewa kwa majina yao na mishahara wanayolipwa ili tufahamu huu mchezo ulivyochezwa na nani alikuwa anachukua mishahara hiyo.
Wengi ni ndugu zao hawatawataja kabsa wataishia kusema wamewachukulia hatua tu lakini upepo ukipita watazua skendo ingine hilo linasahaulika haraka.
 
Likija shindano au mashindano ya Dunia ya Nchi zenye Vioja Duniani, Tanzania itabeba kombe la Dunia bila upinzani wowote na Ushindi wataupatia kwenye, wabunge, mawaziri, viongozi, wasitaafu woote kulundikana mji mmoja na kuacha kusambaza maendeleo Mikoani, kwenye, ulalamishi na kuongea sana Tanzania bia itakuwa bingwa, magumashi na Uchakachuaji itakuwa Bingwa hata mara 1000 , Nyerere alijua kuwa ipi siku Nchi hii itakuja kuwa na vioja vya kulundikana jiji Dsm na kuhatarisha Usalama wa Nchi na kudumaza maendeleo mikoani akaja na wazo la kuhamia Dodoma, lakini wamepuuza hilo wazo wote wameamua kubanana Dsm hatujuia hatima yake.
 
Hata malawi walihamia mji mpya baada ya kupata darasa CDA, kuna pesa nyingi zimeliwa na wajanja hapo CDA kwa kisingizio cha kuijenga Dodoma, wakiamua kufanya Uchunguzi magereza yatafurika wafungwa wa pesa za kuijenga Dodoma, Nchi Nyingi hata Marekani mji mkuu huwa haukai kwenye mji wa Heka heka nyingi sana, hata Africa kusini mji wa kijanja Johannesburg, Daban wameiacha ifanye biashara wao wapo pritoria na bunge lipo capetown ili kusambaza Maendeleo nchi nzima, Tanzania wabunge wote na viongozi wote wapo Dsm hata wakuu wa mikoa, Wilaya huko wanaenda kufanya kazi lakini nyumba zao zipo Dsm, Hiki kioja kipo Tanzania pekee hapa Duniani ni vigumu maendeleo kusambaa mikoa mingine kutokana na Ujinga wa kulundikana Dsm na kuzidisha foleni na misafara isiyokwisha.
Uko vizuri tu, na kwa kuhamia Dodoma tutegemee ajali nyingi barabara ya Dar to Dodoma
 
Back
Top Bottom