Malalamiko kwa Bodi ya mikopo kutoka Urusi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malalamiko kwa Bodi ya mikopo kutoka Urusi

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mberembe.., Aug 10, 2011.

 1. M

  Mberembe.. New Member

  #1
  Aug 10, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Malalamiko kutoka kwa Wanafunzi Urusi…
  Tafadhali tunaomba utusaidie kutufukishia ujumbe wetu kwa Serikali .Sisi wanafunzi tunaosoma ,Urusi tumekuwa tunaonewa sana na Bodi ya Mikopo.Kwa mfano mwaka huu wa 2010/2011 wa masomo,Bodi ya mikopo imetukata wastani wa dola 411 $ ambazo ni fedha ya kulipia Bima Ya afya kwa kila mwanafunzi. Viongozi wa chama cha wanafunzi walilishughulika hili ikiwa ni pamoja na kutuma barua zaidi ya tatu kwenda bodi ya mikopo, kupiga simu mara kwa mara.Kila mara wakipiga simu huwa wanaongea na MR.Savalla au mhasibu mkuu wa bodi.Baada ya kuulizia hili swala tangu mwezi wa tatu ,mkurugenzi wa Bodi pamoja na mhasibu mkuu walikiri kwamba hizi pesa zilikatwa kwa makosa ,ila hawajaelewa ni nani aliyefanya hivyo na kwa dhumuni gani walihaidi kulishghulika ikiwa ni pamoja na kututumia kiasi cha fedha iliyokatwa.
  Mwezi huu wa saba uongozi wa wanafunzi ulipokea Ujumbe kutoka kwa ubalozi ukitueleza kwamba fedha zetu zimetumwa kutoka bodi tangu tarehe 11-07-2011,kwa hiyo bodi ilitutaka tukaangalie kama fedha zimekwishafika kwenye akaunti zetu.Hali iliyopo sasa hivi ni kwamba pesa hii haijafika hadi sasa hivi,uongozi umepiga simu kwa mkurugenzi wa Bodi alichojibu ni kwamba yeye hajui kuhusu hilo ila akahaidi kulishughulikia ,Mhasibu mkuu wa bodi wameongea naye pia alichojibu ni kwamba pesa yetu imetumwa tangu tarehe 11-07-2011 kwa hiyo ilitakiwa kwa mda huu tuwe tumeshapata hii pesa.Alitueleza kuwa fedha ilitumwa pamoja na mapungufu ya ada ya wanafunzi waliomaliza mwaka huu ambazo zilielekezwa kwenye akaunti ya ubalozi.Hadi sasa hivi hatuelewi kama fedha ipo kwenye akaunti ya ubalozi au bado ipo mikononi mwa wajanja wachache hapo Bodi ya mikopo.Wiki iliyopita tumepiga simu kwenye benki ambayo Bodi huitumia kututumia pesa zetu hii benki inaitwa M-BENKI ambayo inasadikiwa ni ya NIMROD MKONO, walitueleza kuwa pesa yetu ipo hapo benk bado hawajaituma kwa sababu hawajui mtu aliyeileta kwenye account.Kwa hiyo wanashindwa kuiprocess.Sasa hatuelewi ukweli uko wapi mhasibu au benki? Miaka ya nyuma kulikuwa na tabia ya maofisa wa ubalozi kuchelewesha fedha za wanafunzi kwa makusudi ili kutengeneza faida yao wenyewe kwa kupitia akaunti ya ubalozi , ila baada ya kuletwa balozi mpya Mheshimiwa JACKA MWAMBI alitokomeza huu mchezo na akashauri bodi kila mwanafunzi afungue akaunti yake mwenyewe ili bodi watume pesa moja kwa moja kwa mwanafunzi,tunamshukuru kwa hili.
  Kwasasa hivi hatuelewi kama kweli hiyo pesa imetumwa kwenye akaunti ya ubalozi kama alivyosema Mhasibu mkuu wa bodi ,na kama pesa imeelekezwa kwenye akaunti ya Ubalozi basi si ajabu balozi wetu halifahamu hilo ,kwa sababu tuna uhakika kama balozi angalifahamu kuhusu ilo basi tungeshapata fedha zetu au bado hii pesa iko Tanzania. Tunaomba serikali ilishughulikie hili swala kwani hali ya wanafunzi kwa sasa ni ngumu sana. Wiki iliyopita kuna wanafunzi wa Kitanzania wameshikwa wakiiba supermarket yote hii ni kwasababu hawana pesa za matumizi ,dada zetu nao kazi wanazofanya usku ni aibu na balozi hataki kutute​tea ili tuongezewe japo ela ya kujikimu.Jamani hapa Moscow haturuhusiwa kufanya kazi kabisa,kwa hiyo hatuna njia ya kujiingizia kipato .Tumekuja huku kusoma na hatujaja huku kuteseka .Kuna watu wachache bodi ya mikopo wanatulazimisha tuteseke kwa roho zao za ubinafsi.
  ASANTE SANA..
  WANAFUNZI URUSI.
   
 2. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Join Date : 10th August 2011
  Posts : 1
  Rep Power : 0  Wewe mkali kweli. Umejiunga kwa ajili ya kupost malalamiko yako. Lakini mkuu huku tunahagaika na mafuta na umeme, sijui watakusikiliza.
   
Loading...