Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Kwa muda mrefu tumekuwa tukiona viongozi wakuu wastaafu kama Marais na Mawaziri Wakuu wakilindwa na walinzi. Binafsi nilikuwa naamini kuwa walinzi wale ni walinzi binafsi wa viongozi hao kwa vile nilikuwa nawaona muda wote wakiwa na mabosi wao. Tena wakati mwingine nawaona walinzi hao wakiwa na mabosi wao kwenye maeneo ambayo mabosi wao wanakuwa wakiishambulia serikali.
Kutokana na ukimya wa viongozi hao na kuendelea kuwalinda viongozi wao, hakika ilikuwa haiingii akilini kuamini kuwa walinzi hao ni wa Serikali. Tukio la kuondolewa mlinzi wa Edward Lowasa, Aloyce Tendewa limenifumbua macho. Sasa najua kumbe walinzi wale ni wa Serikali. Binafsi sikujua kama Aloyce Tendewa alikuwa ni mlinzi wa Serikali. Niliamini kuwa ni mlinzi wake binafsi na analipwa na Lowasa. Maana muda mwingi alikuwa naye na hata wakati ambapo mzee aliharibikiwa, Tendewa ndiye alikuwa wa kwanza kumsitiri.
Malalamiko ya baadhi ya watu baada ya kuondolewa mlinzi huyo hakika yanazua swali jingine. Je Mlinzi wa kiongozi mstaafu anapaswa kuwa huyo huyo au wanaweza kulinda kwa shift kama wanavyofanya kwenye majengo? Nimezoea sana kwenda Jeshini kwenye kambi ya Jeshi ya Huduma iliyopo Ruhuwiko Songea kumtembelea rafiki yangu anayefanya kazi hapo. Kila nikipita pale getini nakuta kunakuwa na sura tofauti ya walinzi. Nikaamini kuwa Walinzi wa Serikali hawakai kwenye lindo moja kwa muda mrefu.
Imenishtua sana kusikia kuwa Tendewa amekuwa mlinzi wa Lowasa kwa zaidi ya miaka 10. Kumlinda mtu mmoja kwa zaidi ya miaka 10 tena mtu mwenyewe anapingana na serikali iliyoko madarakani hakika ni jambo la kushangaza. Ni dhahiri kwamba mtu akiwa mlinzi wa mtu mmoja kwa zaidi ya miaka 10 hakika mlinzi huyo anageuka kuwa kijakazi wa bosi wake. Ndivyo ilivyotokea kwa Tendewa. Bila shaka kitendo cha kukaa na Lowasa kwa zaidi ya miaka kumi kilimfanya Tendewa kuwa si mlinzi wa serikali bali mlinzi binafsi wa Lowasa.
Hili la Tendewa na Lowasa liwe funzo kwa Serikali. Kwa vile CHADEMA wamesema kuwa wapo tayari kumpatia ulinzi Lowasa kufidia pengo la Tendewa, ni wakati sasa wa Serikali kumuondoa hata yule mmoja aliyepo ili kusiwe na mwingiliano wa majukumu yamkiulinzi kwa vile naamini kuwa mlinzi wa Serikali atakuwa amepata mafunzo tofauti ya ulinzi wa viongozi na yule mlinzi wa CHADEMA