Malaigwanan wazidi kumbana Lowassa

Malaigwanan wazidi kumbana Lowassa

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,538
Na Paulo Sarwatt, Arusha

VIONGOZI wa kimila wa jamii wa wafugaji wa kimaasai (Malagwanan) wilayani Monduli, wameendelea na ‘msuguano mkali’ kati yao na Mbunge wa Jimbo hilo, Edward Lowassa, wakidai ndiye chanzo cha wao kujihusisha masuala ya kisiasa.Viongozi hao wamemtaja Lowassa katika barua yao kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kupinga hatua ya serikali wilayani humo kupiga marufuku mikutano na mikusanyiko ya viongozi hao, kwa madai kuwa wanaingilia masuala ya kisiasa.

Tayari serikali wilayani humo kupitia Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Jowika Kasunga, ilipiga marufuku wazee hao kufanya mikutano kupitia barua yenye kumbukumbu namba AB.115/122/01/1 ya Februari 20, mwaka huu.Katika barua hiyo DC Kasunga aliwaagiza maafisa tarafa, watendaji wa kata na vijiji kuhakikisha wanazuia mikutano na mikusanyiko ya wazee akiwatuhumu kuwa wamekuwa wakiingilia masuala ya kisiasa, hasa suala ubunge wa Jimbo la Monduli katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, mwaka huu.

Barua ya viongozi hao ni mwendelezo wa mgogoro na mpasuko mkubwa ulioibuka katika jimbo hilo, baina ya viongozi wa kimila kuhusu nani hasa atarithi kiti cha Lowassa kama mbunge wa jimbo hilo, baada ya mbunge huyo aliyewahi kuwa Waziri Mkuu kutangaza rasmi kutagombea tena nafasi hiyo.Chimbuko la mgogoro na mpasuko huo miongoni mwa viongozi wa kimila ni kuhusu hatua ya Lowassa kumpendekeza Namelok Sokoine kuwa mgombea pekee wa CCM katika uchaguzi huo.

Namelok ni mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine, aliyefariki kwa ajali ya gari mkoani Morogoro, mwaka 1984 na pia Mbunge wa Vitimaalumu Mkoa wa Arusha.

Barua ya kwenda kwa RCKatika barua yao kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, iliyotiwa saini na mwenyekiti wao, Sandet ole Ngewa, wazee wanaeleza kuwa wamemwandikia barua mkuu huyo wa mkoa kumfahamisha nini hasa kinaendelea kuhusu sakata hilo. Mwenyekiti huyo anafafanua kuwa ni kweli viongozi wa kimila hawaruhusiwa kujihusisha na masuala ya kisiasa na wamekuwa wakifanya hivyo kwa miaka yote, isipokuwa viongozi hao wanaweza kushiriki siasa kwa utashi binafsi wa mtu bila kukiuka taratibu, sheria na kanuni za chama husika.

“Kwa kumbukumbu zetu, zaidi ya mkutano wa Maligwanan wote (mkutano mkuu) ambao ulihudhuria pia na wenyeviti wa vijiji uliofanyika Februari 13, mwaka huu, katika kata ya Esilalei kupokea rasmi ‘agizo’ la Lowassa la kutaka Namelok Sokoine awe mrithi wake katika nafasi ya ubunge Jimbo la Monduli kwani yeye anakwenda kugombea urais, hakuna tena mkutano mwingine wa kisiasa uliofanyika ndani ya wilaya hii,” ilisomeka barua hiyo.
Barua hiyo inaendelea kueleza: “Kwa bahati nzuri alikuwepo mtumishi wa serikali ambaye ni Katibu Tarafa ya Kisongo, Paul Kiteleki, kwenye kikao hicho kilichofanyika Tarafa ya Makuyuni, akidai kumwakilisha Lowassa.”

Mwenyekiti huyo anaeleza kuwa kabla ya mkutano huo wa Februari 13 kulikuwa na mikutano midogo iliyoitishwa na baadhi ya Malaigwanan iliyofanyika katika kata za Esilalei, Monduli Juu na Lokisale wakisema wametumwa na Mbunge wao, Lowassa, kumfanyia kampeni Namelok Sokoine awe mrithi wake. Kwa mujibu wa barua hiyo, gharama za kuwajulisha au kufanya mikutano hiyo alizotoa Lowassa na Februari 18 mwaka huu, wazee hao walikutana tena na kutoa tamko la kukataa mpango huo wa Lowassa na wafuasi wake wa kutaka binti huyo wa Sokoine awe mgombea pekee wa ubunge wa jimbo hilo.

“Nakala ya barua ya mkuu wa wilaya ambayo ni amri halali ya serikali imetupa shida ya kuelewa ni siasa zipi tunazifanya kama viongozi wa kimila, zaidi ya zile zilizoitishwa kwa maelekezo ya mbunge,” ilieleza.Alisema wanatilia shaka na amri hiyo ya DC kwa sababu awali, Lowassa alikakarriiwa katika mikutano miwili ya hadhara iliyofanyika Mto wa Mbu na Moita kwamba amekwishamwagiza mkuu wa wilaya kupiga marufuku mikutano ya viongozi wa kimila ambao hawaungi mkono harakati zake za kutaka Namelok awe mrithi wake.

“Tunaomba ieleweke kuwa siyo kwamba tunamkataa Namelok kuwa mbunge wa Monduli isipokuwa njia inayotumika kumleta ya kulazimisha na kutumia vitisho ndiyo tunayopinga, kwani muda wa kampeni bado. Huku ni kuvunja haki za watu wengine wanaotaka kugombea na ukiukwaji mkubwa wa kanuni na taratibu za chama chetu (CCM),” aliendelea.
Anaeleza zaidi kuwa iwapo uthibitisho wa madai yao utahitajika katika ngazi yoyote ya chama na serikali, watawasilisha picha na rekodi mbalimbali za Lowassa akimnadi Namelok na pia watu wanaotumiwa kufanya kazi hiyo, kinyume cha taratibu za Chama.

“Viongozi wa chama ngazi ya wilaya wanaona na wanashiriki katika ukiukwaji huu kwa kisingizio kuwa mbunge anakagua shughuli za maendeleo. Kuendelea kulazimishwa na mbunge kumchagua Namelok itakuwa ni kupokonya na kutumia madaraka yake vibaya na pia kuua demokrasia katika Wilaya ya Monduli,” alisisitiza.

Maagizo kwa viongozi wa mila
Aidha katika barua hiyo, Mwenyekiti huyo amewaagiza viongozi wote wa kimila kwa sasa kuzingatia amri hiyo na serikali wakati wakijipanga kuchukua hatua nyingine kuhusu sakata hilo.
“Tunaagiza shughuli zote za kimila zisimamamishwe kwa muda huu wote ili kuepuka kuchanganya mambo. Malaigwanani wote wa rika zote ‘lalisheni’ rungu zenu hadi ufumbuzi wa suala hili utakapopatikana au muda wa uchaguzi kupita,” aliagiza Mwenyekiti huyo.

Agizo hilo la Mwenyekiti pia limemtaka Lowassa kuacha kutumia rungu alilokabidhiwa kama mzee wa kimila na kueleza zaidi kuwa mkutano wa Malagwanani wote kutoka wilaya zinazokaliwa na jamii ya wafugaji wa kimaasai utafanyika muda wowote kuanzia sasa kujadili suala hilo. “Kwa wale baadhi ya Malaigwanani wa Monduli na wale wa wilaya za Simanjiro na Longido waliokuwa wanahoji uhalali na taratibu zilizotumika katika kumchagua na kumfanya Lowassa kuwa Laigwanan Mkuu wa Afrika Mashariki tofauti na taratibu zinazotumiwa kuwachagua Malaigwanani wengine ndani ya jamii ya Wamaasai, watapata fursa ya kujadili katika mkutano huo,” alifafanua Mwenyekiti huyo. Nakala ya barua hiyo imetumwa kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mwenyekiti wa Baraza la Malaigwanani Mkoa wa Arusha (MARIA), Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya taifa, wakisisitiza barua hiyo kuifikia Kamati ya Maadili ya Chama na viongozi wa kimila wa wilaya za Longido, Ngorongoro na Simanjiro.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, David Felix Ntibenda, hakuweza kuzungumzia suala hilo kwa undani Jumatatu wiki hii, kwa maelezo kuwa yupo katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana, wilayani Ngorongoro.

“Hapa unaponipigia nipo katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, ziara imetuchanganya siwezi kuzungumzia suala hilo mpaka nitakaporudi ofisini,” alisema Ntibenda. Aidha hakuna kiongozi wa CCM Monduli na Mkoa wa Arusha kwa ujumla aliyepatikana kuzungumzia suala hilo, wote wakidai kuwamo katika ziara ya Kinana. Moja wa wasemaji wa Lowassa (aliyeomba jina lake lihifadhiwe) aliliambia Raia Mwema kuwa kwa ufahamu wake, sakata hilo ni sehemu ya mpango wa kumpaka matope Lowassa mbele ya jamii ili kukwamisha ndoto zake za kugombea urais.

Katika ziara yake ambayo inaendelea mkoani Arusha, akiwa wilayani Monduli, Kinana katika mkutano wa hadhara na wa Halmashauri Kuu alisisitiza njia za kidemokrasia zitumike kumpata mrithi wa Lowassa ambaye amekwishatangaza kutogombea tena ubunge. Akimkariri Kinana mmoja wa viongozi wa CCM wilayani humo alisema: “Najua watu wa Monduli ni waaminifu sana kwa CCM na mmekomaa kidemokrasia, hivyo natarajia mtatumia njia hiyo kumpata mrithi wa Lowassa kwa kutoa nafasi sawa kwa wagombea wote watakajitokeza.”

Hata hivyo, wachunguzi wa mambo wanaeleza kuwa mgogoro huo kwa namna moja au nyingine umetia doa taswira ya Lowassa kisiasa katika jimbo hilo, kwa kuwa viongozi wa kimila wamekuwa na ushawishi mkubwa katika jamii hiyo ya wafugaji na mgawanyiko uliotokea unaweza kumgharimu mbunge huyo ambaye alitawala siasa za jimbo lake kwa zaidi ya miaka 20

Sorce Raia mwema
 
Na Paulo Sarwatt, Arusha

VIONGOZI wa kimila wa jamii wa wafugaji wa kimaasai (Malagwanan) wilayani Monduli, wameendelea na msuguano mkali kati yao na Mbunge wa Jimbo hilo, Edward Lowassa, wakidai ndiye chanzo cha wao kujihusisha masuala ya kisiasa.Viongozi hao wamemtaja Lowassa katika barua yao kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kupinga hatua ya serikali wilayani humo kupiga marufuku mikutano na mikusanyiko ya viongozi hao, kwa madai kuwa wanaingilia masuala ya kisiasa.

Tayari serikali wilayani humo kupitia Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Jowika Kasunga, ilipiga marufuku wazee hao kufanya mikutano kupitia barua yenye kumbukumbu namba AB.115/122/01/1 ya Februari 20, mwaka huu.Katika barua hiyo DC Kasunga aliwaagiza maafisa tarafa, watendaji wa kata na vijiji kuhakikisha wanazuia mikutano na mikusanyiko ya wazee akiwatuhumu kuwa wamekuwa wakiingilia masuala ya kisiasa, hasa suala ubunge wa Jimbo la Monduli katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, mwaka huu.

Barua ya viongozi hao ni mwendelezo wa mgogoro na mpasuko mkubwa ulioibuka katika jimbo hilo, baina ya viongozi wa kimila kuhusu nani hasa atarithi kiti cha Lowassa kama mbunge wa jimbo hilo, baada ya mbunge huyo aliyewahi kuwa Waziri Mkuu kutangaza rasmi kutagombea tena nafasi hiyo.Chimbuko la mgogoro na mpasuko huo miongoni mwa viongozi wa kimila ni kuhusu hatua ya Lowassa kumpendekeza Namelok Sokoine kuwa mgombea pekee wa CCM katika uchaguzi huo.

Namelok ni mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine, aliyefariki kwa ajali ya gari mkoani Morogoro, mwaka 1984 na pia Mbunge wa Vitimaalumu Mkoa wa Arusha.

Barua ya kwenda kwa RCKatika barua yao kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, iliyotiwa saini na mwenyekiti wao, Sandet ole Ngewa, wazee wanaeleza kuwa wamemwandikia barua mkuu huyo wa mkoa kumfahamisha nini hasa kinaendelea kuhusu sakata hilo. Mwenyekiti huyo anafafanua kuwa ni kweli viongozi wa kimila hawaruhusiwa kujihusisha na masuala ya kisiasa na wamekuwa wakifanya hivyo kwa miaka yote, isipokuwa viongozi hao wanaweza kushiriki siasa kwa utashi binafsi wa mtu bila kukiuka taratibu, sheria na kanuni za chama husika.

Kwa kumbukumbu zetu, zaidi ya mkutano wa Maligwanan wote (mkutano mkuu) ambao ulihudhuria pia na wenyeviti wa vijiji uliofanyika Februari 13, mwaka huu, katika kata ya Esilalei kupokea rasmi agizo la Lowassa la kutaka Namelok Sokoine awe mrithi wake katika nafasi ya ubunge Jimbo la Monduli kwani yeye anakwenda kugombea urais, hakuna tena mkutano mwingine wa kisiasa uliofanyika ndani ya wilaya hii, ilisomeka barua hiyo.
Barua hiyo inaendelea kueleza: Kwa bahati nzuri alikuwepo mtumishi wa serikali ambaye ni Katibu Tarafa ya Kisongo, Paul Kiteleki, kwenye kikao hicho kilichofanyika Tarafa ya Makuyuni, akidai kumwakilisha Lowassa.

Mwenyekiti huyo anaeleza kuwa kabla ya mkutano huo wa Februari 13 kulikuwa na mikutano midogo iliyoitishwa na baadhi ya Malaigwanan iliyofanyika katika kata za Esilalei, Monduli Juu na Lokisale wakisema wametumwa na Mbunge wao, Lowassa, kumfanyia kampeni Namelok Sokoine awe mrithi wake. Kwa mujibu wa barua hiyo, gharama za kuwajulisha au kufanya mikutano hiyo alizotoa Lowassa na Februari 18 mwaka huu, wazee hao walikutana tena na kutoa tamko la kukataa mpango huo wa Lowassa na wafuasi wake wa kutaka binti huyo wa Sokoine awe mgombea pekee wa ubunge wa jimbo hilo.

Nakala ya barua ya mkuu wa wilaya ambayo ni amri halali ya serikali imetupa shida ya kuelewa ni siasa zipi tunazifanya kama viongozi wa kimila, zaidi ya zile zilizoitishwa kwa maelekezo ya mbunge, ilieleza.Alisema wanatilia shaka na amri hiyo ya DC kwa sababu awali, Lowassa alikakarriiwa katika mikutano miwili ya hadhara iliyofanyika Mto wa Mbu na Moita kwamba amekwishamwagiza mkuu wa wilaya kupiga marufuku mikutano ya viongozi wa kimila ambao hawaungi mkono harakati zake za kutaka Namelok awe mrithi wake.

Tunaomba ieleweke kuwa siyo kwamba tunamkataa Namelok kuwa mbunge wa Monduli isipokuwa njia inayotumika kumleta ya kulazimisha na kutumia vitisho ndiyo tunayopinga, kwani muda wa kampeni bado. Huku ni kuvunja haki za watu wengine wanaotaka kugombea na ukiukwaji mkubwa wa kanuni na taratibu za chama chetu (CCM), aliendelea.
Anaeleza zaidi kuwa iwapo uthibitisho wa madai yao utahitajika katika ngazi yoyote ya chama na serikali, watawasilisha picha na rekodi mbalimbali za Lowassa akimnadi Namelok na pia watu wanaotumiwa kufanya kazi hiyo, kinyume cha taratibu za Chama.

Viongozi wa chama ngazi ya wilaya wanaona na wanashiriki katika ukiukwaji huu kwa kisingizio kuwa mbunge anakagua shughuli za maendeleo. Kuendelea kulazimishwa na mbunge kumchagua Namelok itakuwa ni kupokonya na kutumia madaraka yake vibaya na pia kuua demokrasia katika Wilaya ya Monduli, alisisitiza.

Maagizo kwa viongozi wa mila
Aidha katika barua hiyo, Mwenyekiti huyo amewaagiza viongozi wote wa kimila kwa sasa kuzingatia amri hiyo na serikali wakati wakijipanga kuchukua hatua nyingine kuhusu sakata hilo.
Tunaagiza shughuli zote za kimila zisimamamishwe kwa muda huu wote ili kuepuka kuchanganya mambo. Malaigwanani wote wa rika zote lalisheni rungu zenu hadi ufumbuzi wa suala hili utakapopatikana au muda wa uchaguzi kupita, aliagiza Mwenyekiti huyo.

Agizo hilo la Mwenyekiti pia limemtaka Lowassa kuacha kutumia rungu alilokabidhiwa kama mzee wa kimila na kueleza zaidi kuwa mkutano wa Malagwanani wote kutoka wilaya zinazokaliwa na jamii ya wafugaji wa kimaasai utafanyika muda wowote kuanzia sasa kujadili suala hilo. Kwa wale baadhi ya Malaigwanani wa Monduli na wale wa wilaya za Simanjiro na Longido waliokuwa wanahoji uhalali na taratibu zilizotumika katika kumchagua na kumfanya Lowassa kuwa Laigwanan Mkuu wa Afrika Mashariki tofauti na taratibu zinazotumiwa kuwachagua Malaigwanani wengine ndani ya jamii ya Wamaasai, watapata fursa ya kujadili katika mkutano huo, alifafanua Mwenyekiti huyo. Nakala ya barua hiyo imetumwa kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mwenyekiti wa Baraza la Malaigwanani Mkoa wa Arusha (MARIA), Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya taifa, wakisisitiza barua hiyo kuifikia Kamati ya Maadili ya Chama na viongozi wa kimila wa wilaya za Longido, Ngorongoro na Simanjiro.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, David Felix Ntibenda, hakuweza kuzungumzia suala hilo kwa undani Jumatatu wiki hii, kwa maelezo kuwa yupo katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana, wilayani Ngorongoro.

Hapa unaponipigia nipo katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, ziara imetuchanganya siwezi kuzungumzia suala hilo mpaka nitakaporudi ofisini, alisema Ntibenda. Aidha hakuna kiongozi wa CCM Monduli na Mkoa wa Arusha kwa ujumla aliyepatikana kuzungumzia suala hilo, wote wakidai kuwamo katika ziara ya Kinana. Moja wa wasemaji wa Lowassa (aliyeomba jina lake lihifadhiwe) aliliambia Raia Mwema kuwa kwa ufahamu wake, sakata hilo ni sehemu ya mpango wa kumpaka matope Lowassa mbele ya jamii ili kukwamisha ndoto zake za kugombea urais.

Katika ziara yake ambayo inaendelea mkoani Arusha, akiwa wilayani Monduli, Kinana katika mkutano wa hadhara na wa Halmashauri Kuu alisisitiza njia za kidemokrasia zitumike kumpata mrithi wa Lowassa ambaye amekwishatangaza kutogombea tena ubunge. Akimkariri Kinana mmoja wa viongozi wa CCM wilayani humo alisema: Najua watu wa Monduli ni waaminifu sana kwa CCM na mmekomaa kidemokrasia, hivyo natarajia mtatumia njia hiyo kumpata mrithi wa Lowassa kwa kutoa nafasi sawa kwa wagombea wote watakajitokeza.

Hata hivyo, wachunguzi wa mambo wanaeleza kuwa mgogoro huo kwa namna moja au nyingine umetia doa taswira ya Lowassa kisiasa katika jimbo hilo, kwa kuwa viongozi wa kimila wamekuwa na ushawishi mkubwa katika jamii hiyo ya wafugaji na mgawanyiko uliotokea unaweza kumgharimu mbunge huyo ambaye alitawala siasa za jimbo lake kwa zaidi ya miaka 20

Sorce Raia mwema

Huyu bwana siku zote hajawahi kuandika anything positive kuhusu Lowassa. The story is long overdue and not balanced. Tulitegemea muandishi Wa habari hizi atueleze nature ya succession politics.

Wagombea Wa Mbunge jumbo LA Monduli ni wengi wapi Kama 9 hivi na muda utajapofika hakuna atakaependeleawa. Itakukuwa free for all atakaekubalika na wananchi ni hiyo hiyo.

Kinachosumbua baadhi ya hapo kiongozi Wa kimila ni mfumo dume. Wamaasai hawaamini kuongozwa na mwanamke hata akiwa na ubungo ulioshuka kutoka mbinguni. Hii ni dhana potofu na haikubaliki katika jamii iliyostarabika.
 
Lowassa kimbia njoo huku vijana wako wa mtandao ni wamelala post Kali against wewe zinaruka Kama kipepeo porini
 
Kumtia doa Lowasa namna gani wakati kweli ameharifu taratibu?

Lowasa ni malicious dictator. Analazimisha uongozi wa wilalay ya Monduli upige marufuku mikutano ya wote wanaompinga uraisi!. Na ndiyvo atakuwa hata akipata madaraka makubwa zaidi.

Ameshakataa kugombea ubunge kwamba anagombea uraisi, ndipo anaanza kufanya sanaa ya kuita watu wa kumshawishi under media coverage. Eti sasa nimeshawishika nitagombea wakati alishautamani uraisi hata kabla mwalimu hajaaga dunia. Huu ni ulaghai na hila za hali za juu.

Kuwalazimisha watu wa Monduli wamchague Namelok kuwa Mbunge kinyume na ridhaa zao, ndiyo hayo hayo tuliyoyasikia juzi wana Monduli wakilalamika kwamba Lowasa baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa, alishinikiza waapishwe wagombea wa ccm ambao kumbe wala hwakushinda. Halfu anasema ccm ilishinda kwa asilimia 100!!. Rangi hii hii ikaonekana sehemu nyingi za nchi kwamba serikali inalazimisha waapishwe ccm walioshindwa!.

Tunaona Lowasa akitumia rungu kuhakikisha wana Monduli wasiomtaka hawafanyi vikao, sura hiyo hiyo tunaiona kwa serikali ikitumia kila liwezekanalo kuzamisha juhudi na haki za upinzani kwa visingizio, vitisho, na hila kibao.

Lowasa = Kikwete = Kinana = Ccm yote/wote.

UPONYAJI WA TAIFA NI KUIFUKKUZILIA MBALI CCM NA USHETANI WAKE!. TUNAHITAJI TANZANIA HURU NA SAFI!.
 
Huyu bwana siku zote hajawahi kuandika anything positive kuhusu Lowassa. The story is long overdue and not balanced. Tulitegemea muandishi Wa habari hizi atueleze nature ya succession politics.

Wagombea Wa Mbunge jumbo LA Monduli ni wengi wapi Kama 9 hivi na muda utajapofika hakuna atakaependeleawa. Itakukuwa free for all atakaekubalika na wananchi ni hiyo hiyo.

Kinachosumbua baadhi ya hapo kiongozi Wa kimila ni mfumo dume. Wamaasai hawaamini kuongozwa na mwanamke hata akiwa na ubungo ulioshuka kutoka mbinguni. Hii ni dhana potofu na haikubaliki katika jamii iliyostarabika.

Kwa hiyo unamaanisha wa masai hatuja staarabika?
 
Mamlaka ya mkuu wa wilaya kuzuia watu kukusanyika na kufanya mikutano inatoka katika sheria ipi
 
Lowassa anawawaashaa eeh dah post bila lowassa ainamshiko
gwajima kawambiaa mwacheni baba wawatu msitafute aibh 2015
 
Marekani taifa linalohubiri demokras lakini tangu wapate uhuru zadi ya marais 40 wamepita hakuna rais mwanamke hata mmoja.
 
CCM wanazani nchi ni mali ya koo zao. Lowassa akupendekeze Sokoine, duuuuh wapi na wapi simba akacheza na muwindaji wa simba
 
amekaa jimboni kwa miaka 30 lkn maji shida, barabara tabu kabisa mpaka leo urais atauweza
 
Tunaomba kwa Mungu atuepushe Mbali na Lowassa!! Anaminya sana demokrasia monduli na tunafanya sala maalumu hata hiyo urais asikie tu redioni
 
Sasa kama wewe unakwenda kugombea urais ya nini kuwachagula watu mgombea ubunge. Si uwaache wachague wenyewe?
 
Back
Top Bottom