Makwaia wa kuhenga na serikali mbili

Makwaia wa kuhenga na serikali mbili

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,756
Reaction score
2,646
Huwa nafuatilia kipindiki cha Je, tutafika, lakini siku hizi napata ukakasi. Huyu jamaa siku hizi anapiga debe serikali 2 tu. Anaalika wageni wenye kazi ya kuponda rasimu ya katiba tu.
My take: Kwa nini mwandishi usichukue watu wenye pande mbili tofauti na mawazo tofauti ili kuwaacha watazamaji waamue wenyewe? Maana yake sasa huku sasa ni kuvaa tu koti la CCM kama alivyofanya Prof. Shivji.
 
Attachments

  • 1396639505404.jpg
    1396639505404.jpg
    66 KB · Views: 271
Huyu Mzee kachoka sana siku hizi,asipoendesha kipindi kwa ushabiki kiasi kile tonge halitakwenda mdomoni,kwa sasa atabaki kuwa mchumia tumbo tu,Aaarrggh!linachefua sana.
 
Mpaka aendeshe kipindi cha kushabikia upande wako ndiyo atakua bora kwako
 
Huwa nafuatilia kipindiki cha Je, tutafika, lakini siku hizi napata ukakasi. Huyu jamaa siku hizi anapiga debe serikali 2 tu. Anaalika wageni wenye kazi ya kuponda rasimu ya katiba tu.
My take: Kwa nini mwandishi usichukue watu wenye pande mbili tofauti na mawazo tofauti ili kuwaacha watazamaji waamue wenyewe? Maana yake sasa huku sasa ni kuvaa tu koti la CCM kama alivyofanya Prof. Shivji.

Pole sana,, Ngoja nitaweka kipande cha wiki iliyopita mabapo alikuwa na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum ambapo mwisho wa kipindi alipewa maagizo na huyo Makamu Mwenyekiti kwamba ahakikishe anawatumia watu waendelee kuiponda Rasimu na kumshambulia Waryoba kwenye kila Kipindi chake.

Hapo yupo Kazini, Maskini Makwaiya amesahau kwamba Mabadiliko hayazuiwi kwa kiganja cha Mkono, hayo ni sawa na mafuriko. Ngoja aendelee kujidanganya na watawala waliokwisha aga wananchi.
 
Tumwonee huruma tumpuuze njaa ikipanda kichwani unategemea nini afadhali enzi zile ikiwa tumboni kilikuwa kati ya vipindi ukikosa unajilaumu.
 
Mpaka aendeshe kipindi cha kushabikia upande wako ndiyo atakua bora kwako

Ukweli ni kuwa maadili ya uandishi, yanamtaka a-balance kipindi; angewaalika watu wenye mitazamo miwili tofauti, kipindi kingekuwa poa sana
 
hivi seříkali mbili wanazozitaka ni na ipi?
 
Ukweli ni kuwa maadili ya
uandishi, yanamtaka a-balance kipindi; angewaalika watu wenye mitazamo
miwili tofauti, kipindi kingekuwa poa sana

Acha umbwiga,,,,ku-balance ni suala moja na ukweli ni jambo la pili,,,,hata kama kalenga ccm 79.4% na cdm 20.23% abalance?mwenyewe unaona inavyoshindikana.
 
Ila kwa jinsi nilivyojaribu kufuatilia maelezo juu ya serikali tatu na yale ya serikali mbili, nimeona dhahiri kuwa katika serikali tatu Muungano utadhoofu na hatimaye utakufa. Ila kwa sasa serikali mbili haziwezekani tena kwakuwa Tanganyika inaonekana wazi kulivaa koti la muungano.

My take.

Zipigwe kura bara kwa watu wabara wangapi wanautaka muungano na wangapi hawautaki.Hali kadhalika kwa wazanzibari ifanyike hivyohivyo na wao watoe matokeo yawe bayana. Ila matokeo ya Zenji na Tanganyika yasichanganywe. Kama wengi hawautaki basi tuache malumbano tuuvunje tu, kama wengi wanautaka basi tuuboreshe kuliko kuupeleka huu mchakato kibabe eti na Rais anaingia kwenye Ligi ya mvutano halafu hajui cha kufanya.
Mi nachoka na uongozi wa mheshimiwa huyu yaani anaanzisha kitu then anashindwa hata kutabiri tatizo litakuwa wapi sa ndo elimu gani aliyonayo .
Unaambiwa Tume zote Tatu suala la muungano na hoja ya Zanzibar na Tanganyika zimekuwa zikiibuka ilitakiwa awe ameshajua akifika hapo nini kifanyike kama alishaliona ni suala gumu basi angeugomea huu mchakato kama Bwana Ben. Sasa yeye kalianzisha halafu anashangaa moto, nadhani ataelekeza lawama kuwa alishauriwa vibaya
 
Mpaka aendeshe kipindi cha kushabikia upande wako ndiyo atakua bora kwako

Nafikiri bila kuweka ushabiki; huyu mzee alikuwa vizuri sana kipindi cha nyuma.. Ila naona pia siku hizi amekuwa anakuja na milengo yake kwenye hivyo vipindi vyake.. Binafsi pia nimeacha kumuangalia as kuna siku alinikera sana... Yaani anaponda vitu obvious kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe na hao wanaom-support..

Kama uko naye karibu, mshauri arudi kulee kwa zamani..
 
Acha umbwiga,,,,ku-balance ni suala moja na ukweli ni jambo la pili,,,,hata kama kalenga ccm 79.4% na cdm 20.23% abalance?mwenyewe unaona inavyoshindikana.
Huko sahihi mkuu, haikushindikana Kalenga tu hata Arumeru.
 
Tatizo la wanahabari wetu njaa kwao ni donda ndugu!
 
Kama huyu ndo ana njaaaaa balaaa anaomba mpaka hela ya gazeti ukikutana naye pale lumumba falcon
 
Back
Top Bottom