Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,273
Chama cha mapinduzi kinapita kwenye kipindi kigumu kuliko watu wengi wanavyofikiri, hii ni kwakuwa watu wengi wamenyimwa uhuru wakupata habari...
Chama kimegawanyika makundi matatu makubwa ambayo huenda yakazaa enzi mpya baada ya 23/7/2020...
Lipo kundi la Wahafidhina ambalo linaamini kuwa Chama kwa sasa kinahitaji kiongozwe na mwenyekiti mwenye historia ya uzoefu katika siasa na uongozi,
Kundi la pili ni lile la Wafadhiri wa Chama ambalo tangu kuasisiwa kwa mfumo wa wizi ndani ya ccm, lenyewe lilijipa jukumu la kusaidia chama kupitia mlango ya wizi ikiwemo ukwepaji kodi. Hili tayari limeshajeruhiwa na utawala wa Magufuli, na limejidhatiti kuhakikisha linakwenda na kura ya veto kuzuia chama kisikabidhiwa kwa Magufuli, Sababu kuu inaelezwa kuwa kundi hili liligharimia chama mabilioni ya pesa ambapo ilitakiwa kundi hilo lilipwe baada tu ya Rais kuingia madarakani, lakini kinyume na matarajio yao, Rais amezuia malipo hayo na kwamba hayo ni madeni ya chama sio ya nchi.
Kundi la Tatu hili ni mtandao imara wa Mh Lowassa, huu umekaa katikati, kazi yake ni kuwapa elimu ya uraia wanaccm kuwa "jamani ehee, chama ni cha hiyari, mkiona mnanyanyaswa njooni huku aliko mzee wetu, hamuoni anavyoishi vizuri siku hizi?" Furahi ya kundi hili ni kuona ccm inavurugana iwe kwa kupewa JPM uenyekiti ama kwa njia yoyote ile....
Kwa vigezo vyovyote vile vya utawala na uongozi, Rais John Magufuli "anatawala" zaidi kuliko kuongoza, Kokote kule duniani, siasa huongozwa sio hutawaliwa, Hatuna historia ya Uongozi wa aina yoyote wa kisiasa wa John Pombe Magufuli,
Lakini kwenye kutawala tumemuona akihudumu katika Wizara na katika Urais sasa kwa miezi kadhaa, anatawala kwakutilia mkazo zaidi maamuzi yake katika nyanja zote za maisha ya Watanzania kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Hili linafanya kwa wadadisi wa siasa na uongozi aonekane kuwa kero kwenye mizani ya kisiasa na kidemokrasia, sio kwa wapinzani tu bali kwa taifa kwa ujumla, huenda ni ugeni wake katika uongozi ama ni aina yake ya kupendelea kutawala kuliko kuongoza.
Tofauti ya mtawala na kiongozi nikuwa, Kiongozi huongoza kwa kusikiliza anaowaongoza zaidi, na mtawala hutawala yale ayaaminiyo yeye kuwa ni sahihi, yaani zidumu fikra za mkubwa....
Pamoja na takwa la kikatiba nikuwa Rais akabidhiwe uenyekiti, Bado mkutano mkuu unaoketi kesho unayo fursa ya kutengua matakwa hayo ya kikatiba kwa maslahi ya chama na taifa.
Kwamaoni yangu ccm isimpe uenyekiti Magufuli angalau kwa miaka miwili mbele kuelekea 2020.