Makubwa haya madogo yana nafuuu!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makubwa haya madogo yana nafuuu!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtu wa Pwani, May 22, 2008.

 1. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Moses Mujibila aachia ngazi
  2008-05-22 11:42:10
  Na Mary Edward, PST Dodoma


  Hatimaye Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Tawala Tanzania Bara, Bw. Moses Mujibila aliyetoa shutuma nzito kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimentri ya Utumishi Umma Bi. Hawa Ghasia, dhidi ya Wakuu wa Wilaya, amejiuzulu.

  Hayo yamebainika jana, wakati wa kufunga mkutano wa Makatibu Tawala wa Wilaya, uliofanyika kwa siku mbili mjini Dodoma.

  Bw. Mujibila aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo kwamba, ameamua kujiuzulu ili kunusuru utendaji kazi wa makatibu tawala wenzake.

  Bw. Mujibila ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Muheza alifikia hatua hiyo, kutokana na kile kinachodaiwa kutoa shutuma za uongo kwa Waziri Ghasia dhidi ya wakuu wa wilaya nchini. Juzi, wakati Waziri Ghasia akifungua mkutano huo, mwenyekiti huyo alitoa shutuma nzito dhidi ya wakuu wa wilaya alipokaribishwa kutoa shukrani.

  Alizitaja baadhi ya shutuma hizo, kuwa ni pamoja na wakuu wa wilaya wamekuwa hawaelewani na makatibu tawala wao na kutokubali kushauriwa kwa kila jambo.

  Pia alidai wamekuwa wakitoa majungu kwa waaajiri wao wakitaka wahamishwe na kufanya ufisadi kwenye matumizi ya mafuta na magari.

  Kadhalika, alidai wamekuwa wakiwafokea mbele za watu wanaowaongoza, kujiona wao ndio wakubwa wa kila kitu na hivyo kuwadhalilisha.

  Mwenyekiti huyo alisema, imefikia kipindi kwa baadhi ya wakuu hao wa wilaya wanadiriki kuwazushia tuhuma za wizi wa mafuta ya petroli na mali mbalimbali na hivyo kushindwa kuelewa kiini cha matatizo hayo.
  Hata hivyo, Waziri Ghasia alilazimika kujibu shutuma hizo moja baada ya nyingine na kuwageuzia kibao akidai kuwa wao ndiyo walioshindikana kwa tabia. Bi. Ghasia ambaye alizungumza kwa mifano huku akisema anawafahamu Makatibu Tawala wenye migogoro kwenye wilaya zao, huku akisita kujata majina yao na kuahidi atayaweka hadharani kwenye mkutano wa pamoja, kati ya Wakuu wa Wilaya na Makatibu Tawala hao, utakaofanyika baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge la Bajeti Mwaka huu.
  Kutokana na kauli hiyo, baadhi ya makatibu tawala walikanusha vikali usemi huo kwa madai kuwa, hawakumuagiza aseme hivyo, kwani hayo ni maneno yake binafsi.

  Kiongozi huyo alijiuzulu nafasi hiyo mbele ya Katibu Mkuu wa Tume ya Utumishi, Bw. George Yambesi kitendo ambacho kilisababisha kufanyika tena uchaguzi wa Mwenyekiti mwingine.

  Katika uchaguzi huo, ambao ulikuwa na wajumbe 108, Katibu Tawala wa Wilaya ya Longodo, Bw. Mohamed Pawaga aliibuka kidedea baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti kwa jumla ya kura 92.

  Katibu wake ni Bi. Mwanaidi Mwanga, Katibu Tawala wa Mkuranga ambaye naye alipitishwa bila kupingwa na wajumbe hao.

  Mapema akifunga mkutano huo, Katibu Mkuu Bw. Yambesi aliwataka kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya kazi kwa mujibu wa sheria.

  Bw. Yambesi alisema ni lazima mtumishi wa umma afanye kazi kwa kuzingatia taratibu za kazi ili kuweza kutoa huduma bora kwa wanachi.

  SOURCE: Nipashe


  ukweli ni upi? jee wamemtoa kafara mwenzao baada kutajwa ya kwao au kulikoni?

  na jee vipi utawala unaendeshwa katika ngazi za wilaya?
   
 2. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kwa jinsi Tanzania inavyokwenda shutuma hizi huenda ni sahihi mimi namuunga mkono japo kajiuzulu. Mathalani nitoe mfano ambao utaonyesha jinsi gani Watanzania wengi tunaishi kisanii.
  Mshahara 80,000 kwa mwezi
  Matumizi 300,000 kwa mwezi
  Tofauti ni 220,000 zinapatikana toka wapi?
  Kwa njia hii Mafisadi tupo wengi including Wakuu wa Wilaya zetu.
   
Loading...