Funa the Wild
Senior Member
- Aug 1, 2022
- 174
- 288
KabisaTanzania tuna vitu vizuri sana vya kujivunia kama taifa
Nimejifunza kitu hapo mkuuKabisa
Asante sana mkuu👍nimejifunza kitu hapo mkuu
ASANTE KWA TAARIFA NZURI YA UTALIIUtalii wa milimani.
Ukiachilia mbali hifadhi ya taifa ya Mikumi na Uzdungwa basi safu za milima Uluguru ni miongoni mwa maeneo ambayo shughuli za ki utalii zinapamba moto sana.
Uluguru Mountains/Milima Uluguru (Eastern Arc Mountains).
Milima Uluguru hupatikana Tanzania katika mji wa Morogoro. Kuna aina 12 za milima tofali katika ukanda wa Afrika mashariki milima Uluguru ndiyo milima tofali mirefu zaidi kuliko milima tofali mingine. Ina urefu wa mita zisizopungua 2600 kutoka usawa wa bahari.
Milima hii ni miongoni mwa milima inayotumika kama hifadhi ya viumbe ambavyo vipo katika hatari ya kutoweka kutokana na shughuli mbalimbali za kibanadamu kitaalamu maeneo kama hayo hufahamika kama
Biodiversity hotspots.
Milima hii ni chanzo cha maji ya mto Ruvu unaosambaza maji yake katika maeneo ya Kibaha na jiji la Dar es salaam. Pia kwa wakazi wa Morogoro huwa wanapata maji kutoka kwenye safu za milima iyo.
Upekee wa Mlima Uluguru.
Unaweza ukashangaa lakini huo ndiyo uhalisia. Ivi unajua kwamba kuna baadhi ya viumbe vinapatikana eneo moja tu ulimwenguni kote na huvikuti maeneo mengine..!!
Ndani ya safu za milima Uluguru kuna jamii ya ndege hufahamika kama Uluguru Bush Shrike. Hii ni jamii ya ndege inayopatikana ndani ya safu za milima Uluguru pekee na hutoikuta maeneo mengine duniani kote kitaalamu huitwa Endemic Species (Viumbe wanaopatikana eneo moja pekee na hawapatikani maeneo mengine) . Imeitwa ilo jina kutokana na eneo ambalo hupatikana ndege uyo.
View attachment 2312719
Mbali na uwepo wa ndege hao. Pia kuna shughuli mbalimbali za utalii huwa zinafanyika, kama kupanda milima, kutembelea maporomoko ya maji mfano Choma, Hululu. Kutembelea makazi ya wajerumani waliokuwa wakiishi miaka ya nyuma na njia walizopita, Kutembelea kanisa la wajerumani, kuona mawio na machweo, kupunga upepo na kutuliza mawazo. Kutembelea makazi ya chief wa waluguru wa kumi na tano aliyefahamika kwa jina la Chief Kingalu.
Pamoja sana. Asante kwa ufuatiliajiASANTE KWA TAARIFA NZURI YA UTALII
Sawa motivation speaker😅👍. UmeskikaTafuta pesa wewe acha kufuatilia historia zisizo na tija
asante kwa taarifa chiefView attachment 2313786
Saltwater Crocodiles, Hawa ni mamba wanaopatikana zaidi Asia na Australia. Ni mamba wanaoishi kwenye maji chumvi na ni wakubwa kuliko mamba wote duniani wana kilo 1000kg. Si kawaida hapa kwetu Africa kuwa na aina ya mamba wanaoishi kwenye maji chumvi lakini kwa Tanzania utawakuta mamba wa aina iyo.
Mto Wami ni miongoni mwa mito inayomwaga maji yake bahari ya hindi. Mto huu umekatiza ndani ya hifadhi ta taifa Saadani ikiwa ndani yake kuna viumbe kama Mamba, Samaki na Viboko.
Kipindi cha kupwa (Kupungua) na kujaa (Kuongezeka) kwa maji ya bahari. Maji bahari yakiongezeka huchanganyikana na maji ya mto Wami na kusababisha mchanganyiko wa maji Chumvi(Bahari) na maji yasiyo chumvi (mto).
Mwendelezo wa kitendo icho hupelekea maji ya mto kuwa chumvi na mamba wanaoishi ndani ya mto kuzoea mazingira ya maji chumvi (Adaptation).
Pamoja sana mkuu👍🤝asante kwa taarifa chief
Nakumbuka kuna mwaka tulip8ta hapo na ATC anga lilikuwa dusty sana pilot akatangaza kuwa mlima Oldonyo Lengai umelipuka volcano"Mlima wa Mungu" (Ol Doinyo Lengai).
Ol doinyo Lengai ni neno la kimasai likimaanisha "Mlima wa Mungu". Mlima huu unapatikana kaskazini mwa nchi ya Tanzania katika mkoa wa Arusha mwishoni mwa upande wa mashariki mwa ziwa Natron.
Ni miongoni mwa milima yenye volcano iliyo hai (Active Volcano). Una mita za urefu zisizopungua 2900. Mlima huu una aina ya lava inayofahamika kama "Carbonatitic" ambapo ndani yake kuna kiwango kikubwa cha madini ya Sodium na Calcium. Na kiwango kidogo na Silica.
Kwa nini huitwa Mlima wa Mungu?
Wamasai hutumia mlima huu kama sehemu ya ibada. Hufanya ibada kwenye mlima huo ili kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili ikiwemo matatizo ya uzazi.
Asante sana mkuuTaarifa imetufikia mkuu.......
Yeah bado ni volcano iliyo hai. Mda wowote huwa inalipuka.Nakumbuka kuna mwaka tulip8ta hapo na ATC anga lilikuwa dusty sana pilot akatangaza kuwa mlima Oldonyo Lengai umelipuka volcano
Ebu fafanua kidogo, pale neno lipi ni Mungu na lipi mlima, maana Kuna General anaitwa Lengai Ole Sabaya.Yeah bado ni volcano iliyo hai. Mda wowote huwa inalipuka.
Oldoinyo maana yake "Mlima" Engai Maana yake "Mungu"Ebu fafanua kidogo, pale neno lipi ni Mungu na lipi mlima, maana Kuna General anaitwa Lengai Ole Sabaya.