Maktaba ya kuelea yatia nanga Dar es Salaam

Maktaba ya kuelea yatia nanga Dar es Salaam

Jamjicho

Member
Joined
Jan 25, 2016
Posts
15
Reaction score
11
proxy

Meli ambayo imebebea maelfu ya vitabu, ambayo huhudumu kama maktaba, imetia nanga bandarini Dar es Salaam.

Meli hiyo ina zaidi ya vitabu 5,000 pamoja na video.

Itakuwa bandarini Dar es Salaam kwa muda wa wiki tatu hivi, hadi tarehe 17 Februari

proxy

Wananchi wataruhusiwa kuingia kati ya saa tatu unusu asubuhi na saa kumi na mbili jioni Jumanne hadi Jumamosi.

Jumapili, itafunguliwa kati ya saa sita unusu mchana hadi saa kumi na mbili jioni. Jumatatu, haitafunguliwa.

proxy

Ada ya kiingilio ni Sh1,000 za Tanzania.Wanaopanga kuingia, wanatakiwa kupepa vitambulisho vya kitaifa au pasipoti.Nahodha wa meli hiyo ni Bw Durke.(VICTOR)

proxy

Wahudumu wote 400 kwenye meli hiyo ni wa kujitolea, hakuna anayelipwa mshahara.

proxy

Waziri wa Elimu Tanzania Joyce Ndalichako, aliyelaki meli hiyo bandarini, amesema taifa hilo litapanua huduma za maktaba wilayani na vijijini.

proxy

Baada ya kuondoka Dar es Salaam, MV Logos Hope inatarajiwa kuenelea mjini Maputo, Msumbiji na baadaye Durban nchini Afrika Kusini.

Meli hiyo humilikiwa na shirika lisilo la Kijerumani la GBA (Gute Bucher fur Aller/Vitabu Vizuri kwa Wote.CHANZO BBC
 
Wataeneza vp vitabu vijijini wakati umesema wataondoka na meli yao

Jigo
 
Meli imepaki wapi?direction ya kufika ilipopaki?
Hizo passport zinazotakiwa ni za kusafiria au passport size?
 
Kitabu unaondoka nacho au ndio kusomea humo humo? au ni kuona vitabu tu?
 
Mbona hawajasema kama ukikipenda kitabu unaweza kukinunua ???
 
Vitambulisho Vya TAIFA Na PASSIPOT Tu, SIO Vitambulisho Vingine!!!?? WATANZANIA WENGI Hatuna Hivyo Vitambulisho Na Passipot!! JE, Watu Waingiaje Sasa!!!?? ALAFU Hicho Kiingilio Wamepanga Akina Nani!! Ni Wageni Au Wenyeji Wao!!!! MIAKA Ya 90 Tulikuwa Entrance Free!!!
 
kweli mkuu mm nakumbuka nipo
o-level forodhani tulikuwa tunaingia bure miaka ya 95 hv.
 
kweli mkuu mm nakumbuka nipo
o-level forodhani tulikuwa tunaingia bure miaka ya 95 hv.
Haa kumbe hii meli inakuja mara nyingi. nakumbuka nikiwa Forodhani Sec. School zamani sana wakati wa (Uniform zinatoka Italy!) nilifurahia saana hii trip ilikuwa bure lakini kulikuwa na limitation nakumbuka walichukua kila darasa wanafunzi 5 bora kwa ufaulu. Ila ilitenga kwani wengine walitamani kwenda hawakuweza kwenda. Nimependa hii kuwa kila mtu anaweza kwenda. Nakumbuka kuna mtoto fulani wa Mh Malechela ( R.I.P) alikuwa form one aliuliza maswali kadhaa kwa kiingereza fasaha! ( mh wale wa zamani watanielewa unapoingia form one na Kiingereza jamani ilikuwa majanga hivi kile kitabu cha ' Learning through Language! bado kipo?
Nakumbuka vitabu walukuwa wanauza pia mi nilinunua kitabu cha hesabu cha Algebra! Wanaoweza kwenda ni fursa nzuri hata kupeleka watoto pia!
 
Unaweza kutumia kitambulisho chochote,kuna watoto waameenda leo na vitambulisho vya shule na wengine wametumia vya kupigia kura,vitabu vinauzwa kwa units gharama zao ni nafuu sana ni fursa nzuri mno ya kujifunza .
 
Toeni direction (step by step )namna ya kuifikia hiyo meli imepaki wapi?? Sisi tupo mbali kidogo na bandari..
 
Toeni direction (step by step )namna ya kuifikia hiyo meli imepaki wapi?? Sisi tupo mbali kidogo na bandari..
Mkuu gate la kuingilia ni pale Posta maeneo ya station stand ya magari ya mbagala, unavuka upande wa Central Police ile barabara ya kuelekea Office za TASAF, kwenye kona utaona gate la kuingia.

Siyo kwamba kuna vitabu zaidi ya 5,000, bali kuna Title za vitabu zaidi ya 5,000, kwa maana kuwa title 1 inawezakuwa na vitabu hata 500.

Kwa wapenzi wa vitabu tembelea meli hiyo mnunue vitabu kwa bei nafuu. Kiingilio unacholipa ni kama nauli ya kukutoa pale getini na kukusogeza mahala meli ilipo pia kukurudisha baadaye.
uploadfromtaptalk1454522466608.jpg

MV Logos Hope.
uploadfromtaptalk1454522527114.jpg

uploadfromtaptalk1454522559233.jpg

Duka la Vitabu.
uploadfromtaptalk1454522593053.jpg

Mgahawa.
uploadfromtaptalk1454522619361.jpg
 
Imebadilishwa jina hiyo Melissa iliwahi kufika hadi Mtwara mwaka 1995
 
Masharti sio. Magumu. Unatakiwa kwenda na Kitambulisho chochote na Tsh:1000/- ambayo ni kama. Nauli ya kukusafirisha kwa basi lenye Full kiyoyozi toka Geti namba 2 hadi meli ilipo.Wastani wa 1.8Km. Kwenda na. kurudi.

Kuhusiana na Idadi ya vitabu. Meli hiyo imesheheni vitabu zaidi ya 5,000/- Pamoja na Videos Mbalimbali za Music na Documentaries. Kilichonivutia, ni kuona Baadhi wa Wabongo kupenyeza kazi zao humo pia. Nilibahatika kuona vitabu Vya Kiswahili kama Tenzi za rohoni n.k
 
kweli mkuu mm nakumbuka nipo
o-level forodhani tulikuwa tunaingia bure miaka ya 95 hv.[/QUOTE

mm nakumbuka mwaka 2002 nilikuwa volunteer pale watu walikuwa wanaingia bure sasa nashangaa hicho kiingilio cha mwaka huu kwanini
ilishawahi kuja hivi karibuni anapo hakukuwa na kiingilio sasa kwanini sasa wanaingia na viingilio?

serikali imeamua kutoa kiingilio au waon wenyewe maana kuna mkanganyiko hapa hatuelewi elewi?
 
Masharti sio. Magumu. Unatakiwa kwenda na Kitambulisho chochote na Tsh:1000/- ambayo ni kama. Nauli ya kukusafirisha kwa basi lenye Full kiyoyozi toka Geti namba 2 hadi meli ilipo.Wastani wa 1.8Km. Kwenda na. kurudi.

Kuhusiana na Idadi ya vitabu. Meli hiyo imesheheni vitabu zaidi ya 5,000/- Pamoja na Videos Mbalimbali za Music na Documentaries. Kilichonivutia, ni kuona Baadhi wa Wabongo kupenyeza kazi zao humo pia. Nilibahatika kuona vitabu Vya Kiswahili kama Tenzi za rohoni n.k
sasa hapo mkuu nimekuelewa kuhusu hicho kiingiilio kumbe ni nauli mm nilidhani ukiingia pale unalipishwa hiyo 1000 asante kwa kunielewesha
 
Back
Top Bottom