'Maktaba ya kuelea' yatia nanga Dar es Salaam

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
160126142840_mv_logos_hope_dar_es_salaam_512x288_bbc.jpg

Meli ya MV Logos Hope hujulikana kama 'maktaba ya kuelea'
Meli ambayo imebebea maelfu ya vitabu, ambayo huhudumu kama maktaba, imetia nanga bandarini Dar es Salaam.

Meli hiyo ina zaidi ya vitabu 5,000 pamoja na video.

Itakuwa bandarini Dar es Salaam kwa muda wa wiki tatu hivi, hadi tarehe 17 Februari

160126144700_mv_logos_hope_dar_3_512x288_bbc.jpg

Meli hiyo ina vitabu vinavyoangazia fani mbalimbali
Wananchi wataruhusiwa kuingia kati ya saa tatu unusu asubuhi na saa kumi na mbili jioni Jumanne hadi Jumamosi.

Jumapili, itafunguliwa kati ya saa sita unusu mchana hadi saa kumi na mbili jioni. Jumatatu, haitafunguliwa.

160126144921_mv_logos_hope_dar_6_512x288_bbc_nocredit.jpg

Ada ya kiingilio ni Sh1,000 za Tanzania.

Wanaopanga kuingia, wanatakiwa kupepa vitambulisho vya kitaifa au pasipoti.

Nahodha wa meli hiyo ni Bw Durke.

160126144752_mv_logos_hope_dar_4_512x288_bbc.jpg

Wahudumu wote 400 kwenye meli hiyo ni wa kujitolea, hakuna anayelipwa mshahara.

160126144604_mv_logos_hope_dar_3_512x288_bbc.jpg

Wahudumu wanaoishi kwenye meli hiyo wanatoka mataifa mbalimbali
Waziri wa Elimu Tanzania Joyce Ndalichako, aliyelaki meli hiyo bandarini, amesema taifa hilo litapanua huduma za maktaba wilayani na vijijini.

160126144837_mv_logos_hope_dar_5_512x288_bbc.jpg

Baada ya kuondoka Dar es Salaam, MV Logos Hope inatarajiwa kuenelea mjini Maputo, Msumbiji na baadaye Durban nchini Afrika Kusini.

Meli hiyo humilikiwa na shirika lisilo la Kijerumani la GBA (Gute Bucher fur Aller/Vitabu Vizuri kwa Wote)


'Maktaba ya kuelea' yatia nanga Dar es Salaam - BBC Swahili
 
Daah ipo mpaka lini wajameniii!! sisi wa mkoani ili tujipange?
 
Utakuta ni majasusi wa kutupwa wapo kazini
Most likely ni hivyo, ni watu na kazi zao maalum, walikuja wanajeshi wa China na jimeli Lao kuubwa eti wamekuja kuturembelea kumbe ni wezi Vibaka na majambazi wa nyara zetu
 
Most likely ni hivyo, ni watu na kazi zao maalum, walikuja wanajeshi wa China na jimeli Lao kuubwa eti wamekuja kuturembelea kumbe ni wezi Vibaka na majambazi wa nyara zetu

Umeshakolea kiroba tayari.WEKA USHAHIDI
 
Hiyo Maktaba ni usanii tuu kuna ajenda kubwa hapo nyuma ya pazia, kama si biashara haramu ya madawa waangaliwe sana hawa jamaa. Wazungu wana mipango mingi sana ya kufanya biashara hizi kwa mbwembwe na kutumia njia zaidi za Dini.
 
Back
Top Bottom