makovu mwilini

Mimi ninakovu mguuni niliungua nilitoka kwa jirani kuokoa moto asa ile nimeweka kwenye kuni nataka niiname nipulize kumbe nikapiga goti kwenye kibati cha moto duuh niliungua week nzima sikwenda shule enzi hizo darasa la nne
 
Umenkumbusha mbali 1993... nakumbuka nlikuwa hata cjaanza primary..mama alikuwa anenda kazin anarud mchana kula then anarudi kazini na kaka angu pia ambaye alikuwa darasa la tatu kipindi hicho...sasa ilikuwa ikifika saa sita mie nawasha jiko nabandika maji ya ugali anayewah kati ya mama na bro wangu anakuja kupika...
Bro alikuwa anamtegea mama mara nuingi sasa siku hyo kajichelewesha ila haikusaidia akafika kabla ya mama...ikabidi apike ugali sasa ila alikasirika kweli. Sasa wakati anaanza kupika ule uji wa ugali unachemka akaniambia niongezee mkaa ile naweka mkaa uji ule ukaruka ukanimwagikia kwenye mkono..uwii nililiaje na hapo nilikuwa namsikia mama kwa mbali anakuja...sikufuta mpaka mama akafika bado...kuutoa ukatoka na ngozi...
Mpaka leo nna kovu kwa mbali....
Ila kaka angu nae alichezea kipondo kweli.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…