ManiTek TV
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 410
- 159
23/03/2013
Chanzo: http://www.gajetek.com/2013/03/makoti-ya-android-samsung-touchwiz.html
TouchWiz ndio koti pekee ambalo limevalishwa kwenye android na bado linatumika kwenye OS iliyotolewa na Samsung wenyewe yaani Bada OS. Ingawa kwa sasa si simu nyingi za Samsung ambazo hutengenezwa na kuwekewa OS ya Bada, hata hivyo Samsung inaendelea kutumia OS hiyo kwenye simu za bei rahisi.
Toleo la Sansumg TouchWiz kwenye Galaxy S3 linajulakana kama TouchWiz Nature UX, huku likipewa kauli mbiu "inspired by nature", TouchWiz imeiingiza sana Samsung matatani baada ya Apple kuwapeleka mahakamani wakidai kwamba Samsung inaiga muonekana na ufanyaji kazi wa iOS ya Apple.
Makala hii tutazungumzia mambo mbali mbali ya TouchWiz iliyoko kwenye toleo la SIII na simu nyingine zenye TouchWiz Nature UX na baadhi ya mambo ambayo yanapatikana kwenye Samsung Galaxy S4 peke yake kwa sasa. Ingawa watumiaji wa S3 na Note 2 wataweza kutumia mambo haya pale Samsung itakapotoa uboreshwaji (update) wa makoti yao, ambapo tayari Samsung wameshatoa taarifa inayowahakikishia watumiaji hao kwamba wataboresha TouchWiz zao.
Tukiingia kwenye ufanyaji kazi wa TouchWiz, kwanza inakuruhusu kupiga picha ya skrini kwa kusugua kiganja kizima kwenye skrini kutoka upande mmoja kwenda mwengine (SIII), pia TouchWiz inaruhusu kufanya kazi zaidi ya moja sambamba (mulit tasking) kwa mfano unaweza kuweka video yako juu ya sehemu ya skirni na kwa sehemu ya chini ukaandika ujumbe mfupi (SIII).
TouchWiz toleo la Nature UX humruhusu mtumiaji kusimamisha video kwa kufunika kiganja kwenye skrini ya simu (SIII), kwenye S4 utendaji huu umebadilishwa na badala yake video hujisimamisha (pause) mtumiaji anapoacha kuangalia skrini, teknolojia iliyotumika kufanikisha uwezo huu inatokana na mawasiliano baina ya kamera na sensa za simu kuweza kutambua retina za macho hivyo zinapokuwa hazionekani kwenye kamera, sensa huitambulisha simu kusimamisha video, hii hali hufanyika kwa haraka mno kiasi kwamba video haizidi hata sekunde moja kucheza wakati huangalii.
Mtumiaji anapoandika ujumbe mfupi kisha akabadili mawazo na kuamua kupiga simu, anachotakiwa kufanya ni kuweka simu sikioni tu, TouchWiz itatambua kwamba mtumiaji anataka kumpigia simu yule ambaye alikuwa anamuandikia ujumbe na hivyo kupiga simu hiyo wenyewe.
Kivutio kukibwa katika utofautishaji wa Android ya Samsung ni kule kuiwekea simu hiyo apps mbali mbali za ziada ambazo hupatikana katika Simu za Samsung peke yake, mfano app ya S Voice, ambayo ni jibu la Samsung kwa Siri ya iOS, watumiaji huzungumza na simu zao, na App kama vile S Note, S Pen (simu na tableti za Galaxy Note tu ambazo huwa na peni maalum) na S Translator ambayo kwa sasa hupatikana kwenye Galaxy S4 tu, hii humuwezesha mtumiaji kuzungumza lugha moja na Galaxy S4 inatafsiri kwa sauti anachokizungunza kwa lugha nyingine, ni lugha chache tu ambazo zinaweza kutumika kwenye app hii ikiwa ni pamoja na Kiingereza, Kifaransa, Kichina na Kijerumani. Samsung pia wana appstore kwa ajili ya watumiaji wa simu za Samsung peke yao.
Pia Galaxy S4 ina S Health ambayo inahusika na masula ya ufanyaji wa mazoezi na mambo ya kiafya, app hii inashirikiana na sensa mbali mbali zilizo kwenye simu kama vile jairoskop na akselerometa kukupa taarifa za kalori unazounguza, pia samsung wametoa mizani maaluma ya simu hii kwa ajili ya kujipima na mizani hiyo hupeleka data za uzito wako moja kwa moja kwenye simu na hivyo kuhifadhiwa kwa muda mrefu ili kuweza kujifuatilia kama unaongezea au kupungua uzito.
Toleo jipya la lililoko kwenye S4 lina mambo mengine mbali mbali ambayo hatutarudia kuyazungumzia kwa vile tumeyazungumzia kwenye makala za Galaxy S4 Yazinduliwa na Kamera ya Galaxy S4.