"Makoti" ya Android: Sehemu ya 1

"Makoti" ya Android: Sehemu ya 1

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159
16/03/2013

"Makoti" ya Android: Sehemu ya 1


​
Sifa kubwa ya Android ni kuibadili upendavyo. Watengeneza simu wa kampuni kubwa huivalisha OS ya Android "koti" ili kuitofautisha na Android nyingine. Hivyo tutazungumzia baadhi ya makoti ambayo Android huvalishwa hasa na kampuni kubwa kwa ufupi tu. Katika sehemu hii tutaizungumzia Android safi ambayo haikuvalishwa koti ambayo inajulikana kama Stock Android.

Android hii ni safi kwa sababu inatoka bila ya kuongezewa chochote. Simu na tablet maarufu zinazotoka na Android hii ni zile zinazotolewa na kampuni mbali mbali kwa ushirikiano na wamiliki wa Android yaani Google, na gajeti hizi zimepewa jina la brand kama Nexus. Kampuni pekee ambazo mapaka sasa zilizopata nafasi ya kutoa gajeti za Nexus ni HTC, Asus, Samsung na LG.

Simu ya karibuni kabisa ambayo inatumia Android hii ni LG Nexus 4, tableti ya 7" ni ile iliyotolewa na Asus yaani nexus 7 na tablet ya Samsung yenye ukubwa wa 10" ambayo ni Nexus 10. Toleo jipya kabsa katika Andriod hii ni Jelly Bean 4.2.2, mwaka huu kuna matarajio kwamba Google watatoa Android mpya ambayo itajulikana kama Android Key Lime Pie 5.0.
​
Endelea kusoma »


 

Similar Discussions

Back
Top Bottom