phil_kabuje
Member
- Mar 27, 2014
- 67
- 73
Wadau wa Jf kuna hii topic nzuri sana kwa waandika CV nikaona nishare link yake!
wenye hiyo blog wao hawakubali kukopi na kupaste ndo maana nimeweka.
==========================================================
1.Epuka Kukosea herufi za maneno (spelling) kwenye CV yako, hili ni kosa kubwa na itaonyesha ni jinsi gani huna umakini wakati wa kufanya mambo ya muhimu.
2.Usiongeze vitu usivyoweza kuvifanya kwani vitakuumbua siku ya kufanya usaili na kuonekana hujui mengine yote!
3. Epuka kuonekana umefanya kazi nyingi kwa kipindi kifupi kifupi. Mathalani umemaliza chuo mwaka 2012, umeshafanya kazi na makampuni manne tofauti mpaka kufikia mwaka 2014
4. Wasifu wako hautakiwi kuwa na vifupisho bila kuchanganua mfano, nimefanya kazi TRA, AMD, na NIC. Sio wote wanayajua makampuni hayo.
5. Usisahau kuweka mawasiliano yako hasa namba ya simu na anuani yako ya barua pepe
6. Kuweka namba za wadhamini ambazo hazipatikani, pengine walishabadili namba hizo ila kutokana na kwamba huna mawasiliano nao, hujui chochote!
7.Mpangilio mbovu wa wasifu wako, na kushindwa kuelezea kiundani uwezo wako.
8. Epuka kuandika wasifu usioendana na matakwa ya kule unakoupeleka unapoomba kazi. Daima fanya marekebisho kila unapoomba kazi sehemu nyingine.
9. Epuka kuiga wasifu wa mtu mwingine au kukopi kutoka kwenye mitandao matokeo yake mwajiri anakutana na CV kadhaa zinazofanana!
10. Daima panga karatasi zako vizuri kufuata mtiririko kuepuka kumchnganya msomaji na matokeo yake ni kuitupa kapuni na kuendelea na wengine.
Chanzo;kumimuhimu blog