Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 3,024
- 4,031
Katika uendeshaji wa mambo yake serikali hujikuta wakati mwingine inafanya maamuzi au hatua ambazo zinakuwa zinagharimu sana. Si makusudio ya serikali kuletea shida raia wake lakini ndo hivyo tena yanatokea tu kwahiyo kikubwa ni kuikumbusha na kuishauri serikali ili kuchukuliwe hatua stahiki
Tujadili baadhi ya makosa yaliyowahi kufanywa/ yanayofanywa na serikali na tutoe maoni ya utatuzi (panapobidi/panapowezekana)
1. Kuweka expire date kwenye vitambulisho muhimu mfano kitambulisho cha uraia.
Hii inaleta picha mbaya kwamba uraia wa mtu unaexpire hivyo inabidi auhuishe. Tena mbaya zaidi ni pale ambapo inaonekana mtu analipia uraia wake (maana kurenew kitambulisho kunatozwa fedha). Bora kadi za bima ya afya kuletwa utaratibu wa kuexpire ndo ilikuwa sahihi kwakuwa kuna wategemezi wanaokosa sifa siku za mbeleni
2. Kuweka masharti ya wategemezi kwenye bima ya afya ya taifa
Huku tunahubiriwa bima ya afya kwa watu wote huku tena tunawekewa masharti kibao ya kuwaingiza wategemezi sasa hili ndio kosa. Kwa lugha nyepesi ni kwamba kuna watu daima dumu kamwe hawataweza kuwa na bima ya afya kutokana na masharti yaliyopo. Tuchukulie mfano mtumishi ambae yupo single na wazazi wake hawapo au wana bima zao maana yake yeye hawezi kuwa na uwezo wa kuingiza mtu yeyote kwenye bima yake wakati huohuo kwa upande wa ndugu zake wengine kama wajomba na mashangazi ambao hawana uwezo kabisa wataendelea kuteseka as long as hawana mtu wa kuwakatia bima.
Ushauri katika hili ni bora wangeweka tu kipengele cha idadi ya wategemezi lakini uhusiano waondoe au iwe kwa namna nyingine siyo huu wa sasa (mwenza mkwe mzazi na mtoto tu!)
3. Kushusha gharama za maji kwenye miradi ya RUWASA
Tangu mwanzo miradi mingi ilikuwa inajiendesha yenyewe ingawaje kwa taabu hivyohivyo lakini hatahivyo hakukuwa na ukomavu bado kwenye miradi hiyo. Wananchi walishazoea gharama za 50 au 100 sasa kuwaambia itakuwa 20 ni kosa litakaloleta shida kwenye wasimamizi na uendeshaji wa mradi. Maana yake itabidi posho za mawakala na wasimamizi wengine zipungue kwa zaidi ya 50% kitu ambacho hata hiyo waliyokuwa wanapewa walikuwa kila siku wakiomba iongezwe. Ikumbukwe kwamba shida ya maji vijijini kinacholalamikiwa ni upatikanaji wa maji na wala si bei ya kugharamia maji kwahiyo serikali ingeangalia namna ya kufanya maji yapatikane muda wote na si yanapohiyajika na si kushusha gharama huku maji bado ni kitendawili. Mbaya zaidi waendeshaji wanaambiwa wasijali gharama kushushwa kwani mradi ukiishiwa pesa za uendeshaji watakopeshwa kutoka benki! What a waste is this!?
4. Kuwapa uhuru wa kuchagua kusoma Kemia na/au Fizikia wanafunzi wa O-Level pindi wanapofika kidato cha tatu
Hiyo nayo ni miongoni mwa makosa makubwa sana tena yanatengeneza bomu baya sana mbeleni kwenye mfumo wetu wa elimu. Kwa mfano miaka ya nyuma wanafunzi tulilishwa kasumba ya kwamba Sayansi ni ngumu hivyo ikapelekea watu wengi kukimbilia upande wa arts na kufanya waliosomea Kemia Baolojia na Fizikia kuwa wachache sana nchini.
Serikali kupitia hali hiyo ikaamua kuja na mkakati wa kuwapa kipaumbele sana waliosomea Sayansi kama tunavyoona sasa. Hilo ni kosa lingine juu ya kosa la kwanza, maana yake ni kwamba wanafunzi watakomaa na Sayansi wakapuuza masomo ya arts tena kisha tukarudi kulekule mwanzo kwa namna ya kinyume chake (na hili halina muda mrefu kutokea kwani mimi binafsi ni mwalimu na tayari naona wanafunzi kwa sasa Sayansi na Hisabati kwao ni masomo ya kawaida bali ugumu umehamia kwenye Uraia Maarifa ya Jamii na English)
Ushauri wangu kwa Serikali ni bora wasingeweka uhiari huo kwa Sekondari yaani wangeacha mtu asome na kufanyia mtihani masomo yote bila kuchagua kwa level ya O-Level kisha kwenye kwa upande wa ajira, udahili na maswala mengine kama hayo wasingekuwa wanatangaza kuwapa kipaumbele watu fulani bali wangetangaza nafasi watu wapambanie kisha wakachukua kimya kimya hao wanaowataka ili kutowakatisha tamaa wale waliosomea tofauti na wale wanaotakiwa
5.Kutoa uhiari kwa wananchi kwenye maswala au mazoezi mbalimbali ya kitaifa mfano
A.(Kuhesabiwa) sensa
B.Kujiandikisha na/au kupiga kura
C.Chanjo ya uviko-19
Hiari hizo na nyingine kama hizo zinawatesa wengi katika wananchi hasa kundi la watawaliwa kwani watendaji na watekelezaji wakifika kwenye uhalisia wao badala ya kushawishi wananchi utawakuta wanafosi wanakwambia hakuna cha hiari wala nini tena wanaweka mifumo ambayo unajikuta huna namna. Kwa sisi watumishi ndio kabisa unaambiwa kuna hiari za namna nyingi kuna hiari ya lazima n.k mfano mchango wa mwenge
Ushauri kuhusu mambo kama haya- serikali itoe tamko la wazi na la mojakwamoja tu la amri ili watu wasijengeane ubaya pia fedha zisiwe zimepotea bure kwasababu haiwezekani serikali itumie fedha nyingi sana huku wakati huohuo iwaambie watu kitu chenyewe ni cha hiari. Pia unapoipa uhiari unawapa dauti raia kwamba kwanini iwe hiari kama ina umuhimu sana
Ongezea na mengine na mengine na usisahau kutoa ushauri wako kwa serikali.