VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Unafiki wangu upi Mkuu? Wengine ni akina nani hasa?Tupatupa ni mmoja wa Wanafiq wa hapa jf
Nakukubali sana wewe Vutankuvute am sure Chadema watakusikia na watafanya kazi .Sasa ni dhahiri kuwa CHADEMA ni chama kikuu cha upinzani nchini na tishio kwa CCM yetu kama chama tawala Tanzania tangu uhuru. Sasa pia,watanzania wanabadilika kwa kasi mno. Wanajiandaa kubadili siasa za Tanzania hapo 2014 na 2015 katika Chaguzi za Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu. Wananchi wa Tanzania wanajiandaa kuwachagua watu na si vyama. Watachagua wachapakazi na si waharibu demokrasia na maamuzi ya wananchi.Wananchi wako tayari.
Sasa siasa za CHADEMA na CCM ni zile za halali mtu hadi kukuche.Hatua njema sana. Hatua vutizi za kidemokrasia.Yanayotokea Bungeni pia ni kiashiria cha mabadiliko ya kifikra na kimapambano hasa ya kisiasa. Jambo jema linaweza kushadidiwa hata na vijimambo vibayavibaya. Kikubwa ni kuwa demokrasia,kama jambo kubwa na jema, inaimarika. Na wale wanaojaribu kuzuia makuzi ya demokrasia nchini,watakiona cha mtema kuni!
CHADEMA,katika harakati zake za kujitangaza na kujiaminisha kwa watanzania,wanafanya kosa moja kubwa. Wanajiegemeza hasa kwenye mikoa michache nchini. Mikoa mingine inatengwa.Inatembelewa kwa nadra sana. Mikoa inayosahaulika itatumiwa na chama chetu cha CCM isivyo halali kwenye chaguzi. Itatangazwa kuwa CCM imeshinda kwa mbali katika mikoa husika. Hatari kidemokrasia!
CHADEMA wangejielekeza katika hasa mikoa ambayo hata hawana Mbunge hata mmoja. Mikoa kama Mtwara,Pwani,Lindi,Kusini Magharibi,Kaskazini Magharibi na mingineyo ya aina hiyo yaweza kukodolewa macho zaidi. Hakuna haja kila mara kupitia (namaanisha viongozi waandamizi wa chama na makada mahiri) katika mikoa ambayo tayari wameijua na kuikubali CHADEMA. Mikoa hiyo ni kama Mbeya,Arusha,Kilimanjaro,Mara,Manyara,Iringa,Mwanza na Shinyanga,
CHADEMA iliwahi kufanya Operesheni Sangara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. Operesheni hii ikatoa matunda matamu sana kwa CHADEMA. Kanda ya Ziwa ndiyo inayoongoza kutoa Wabunge wengi kwa CHADEMA. Kwanini Operesheni kama hii isifanywe kwingineko? Kanda za kichama hazitoshi. Lazima zaidi kifanyike. Demokrasia ikiimarika,watanzania tutachagua watu bora zaidi.Tutaendelea. CHADEMA fanyeni jambo.
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Unafiki wangu upi Mkuu? Wengine ni akina nani hasa?
Chadema ni janga
Ukweli ni kuwa hadi sasa CHADEMA kipo katika kiwango cha Kanda, hawajafika katika kiwango cha kufikia kila jimbo ili hatimaye waende kila kata na baadaye kijiji na kitongoji. Nadharia za kufanya hivyo zipo, lakini utekelezaji wake ni slow. Nimesoma leo katika moja ya nyuzi humu JF kuwa Mbowe ameanza kwenda kata kwa kata, kijiji kwa kijiji na anakusudia kwenda hadi kitongoji kwa kitongoji na hatimaye kila kaya! Huyu ni Mbowe, mwenyekiti. Anafanya jambo jema kwa jimbo lake ingawa ilikuwa inatakiwa kuwa iwe hivyo katika kila jimbo la uchaguzi hasa kule ambako CDM hawana wabunge!. Chadema wasipofanya hivyo sasa, matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani unaweza kuwapa matokeo ya kuwakatisha tamaa!!Mzee Tupatupa umenena kweli na ninakuunga mkono kabisa..mm natokea shinyanga..ni moja ya mikoa ambayo chadema imejiimarisha sana hasa hasa maeneo ya mjini lakini bado chadema wakitaka kuja wanakuja shinyanga mjini tu eneo ambalo kwa sasa hata liwekwe gogo kwa upande wa chadema kitashinda..
wanasahau kujiimarisha vijijini wanakuwa wanaishia mijini tuki kitu ambacho kinaweza kuwagarimu kwenye chaguzi zijazo maeneo ya vijijini..simaanishi kuwa chadema haipo vjjn no ipo tena sana ila tatizo linakuja watu hawa wanakuwa wanaipenda chadema kwa sababu tu wamechoshwa na maisha magumu wanayokumbana nayo ila si kwa influence ya viongozi wa chama..Hii inasababisha baadhi ya watu waliopo vijijini wakati mwingine kukata tamaa na mageuzi kwa sababu ya kukosa msukumo wa viongozi wa chama mwisho kuamiua kukipigia kura ccm.
tatizo jingine ni hilo la viongozi wakuu wa chama kuzuru mikoa kama mbeya tu na kuacha mikoa ambayo
hawajajiimarisha zaidi. hii inasababisha chama kutokukaa mioyoni mwa watu wa mikoa hiyo na mwisho wa siku inakuwa ni rahis kwao kurudi kwenye ccm...bt all in all ni ushaur mzuri ambao viongozi hasa hasa wa ngazi za juu za chama inatakiwa waufanyie kazi
Ni kweli mzee Tupatupa, mi nashauri waanze haraka,tena sio mijini tu,wajikite vijijini ambako ccm inatumia ujinga wa wananchi kuwahadaa na viberiti,chumvi na tshirts...watanzania sasa ni wepesi wa kung'amua vitu na kufanyia kazi