VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Sasa ni dhahiri kuwa CHADEMA ni chama kikuu cha upinzani nchini na tishio kwa CCM yetu kama chama tawala Tanzania tangu uhuru. Sasa pia,watanzania wanabadilika kwa kasi mno. Wanajiandaa kubadili siasa za Tanzania hapo 2014 na 2015 katika Chaguzi za Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu. Wananchi wa Tanzania wanajiandaa kuwachagua watu na si vyama. Watachagua wachapakazi na si waharibu demokrasia na maamuzi ya wananchi.Wananchi wako tayari.
Sasa siasa za CHADEMA na CCM ni zile za halali mtu hadi kukuche.Hatua njema sana. Hatua vutizi za kidemokrasia.Yanayotokea Bungeni pia ni kiashiria cha mabadiliko ya kifikra na kimapambano hasa ya kisiasa. Jambo jema linaweza kushadidiwa hata na vijimambo vibayavibaya. Kikubwa ni kuwa demokrasia,kama jambo kubwa na jema, inaimarika. Na wale wanaojaribu kuzuia makuzi ya demokrasia nchini,watakiona cha mtema kuni!
CHADEMA,katika harakati zake za kujitangaza na kujiaminisha kwa watanzania,wanafanya kosa moja kubwa. Wanajiegemeza hasa kwenye mikoa michache nchini. Mikoa mingine inatengwa.Inatembelewa kwa nadra sana. Mikoa inayosahaulika itatumiwa na chama chetu cha CCM isivyo halali kwenye chaguzi. Itatangazwa kuwa CCM imeshinda kwa mbali katika mikoa husika. Hatari kidemokrasia!
CHADEMA wangejielekeza katika hasa mikoa ambayo hata hawana Mbunge hata mmoja. Mikoa kama Mtwara,Pwani,Lindi,Kusini Magharibi,Kaskazini Magharibi na mingineyo ya aina hiyo yaweza kukodolewa macho zaidi. Hakuna haja kila mara kupitia (namaanisha viongozi waandamizi wa chama na makada mahiri) katika mikoa ambayo tayari wameijua na kuikubali CHADEMA. Mikoa hiyo ni kama Mbeya,Arusha,Kilimanjaro,Mara,Manyara,Iringa,Mwanza na Shinyanga,
CHADEMA iliwahi kufanya Operesheni Sangara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. Operesheni hii ikatoa matunda matamu sana kwa CHADEMA. Kanda ya Ziwa ndiyo inayoongoza kutoa Wabunge wengi kwa CHADEMA. Kwanini Operesheni kama hii isifanywe kwingineko? Kanda za kichama hazitoshi. Lazima zaidi kifanyike. Demokrasia ikiimarika,watanzania tutachagua watu bora zaidi.Tutaendelea. CHADEMA fanyeni jambo.
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam