Lakini tuna kina Raila Tanzania? Mazingira ya kisiasa yanatoa fursa ya kujenga kina Raila?
Unawezaje kupewa dola ilhali vyombo vya dola havikuamini? Maana taifa haliongozwi na siasa tu. Idara za usalama na majeshi zina nafasi kubwa sana katika kuamua mustakabali wa nchi. Wanasiasa wa Tanzania ni mara ngapi tunajenga rappour na watu wa usalama ili angalau kujua wanawaza nini. Hakuna.
"These opposition victories should be regarded not simply as the
product of a finally freed-up, democratically expressed public will, but
as the outcome of a lengthy process of unraveling of single-party domination,
first unleashed long before by the decision to allow "limited elections"
and then given a critical boost by the perhaps necessary result of
those elections, a split in the ruling party."
Lakini upinzani priority zao ziko wapi? Program zao za voter education ziko wapi? Network zao ziko extensive kiasi gani? Policies zao ziko intuitive kiasi gani? Wanaonyeshaje tofauti za dhahiri kati yao na CCM? Wanaonyeshaje kwamba wamekomaa na wanaweza kuendesha nchi vyema zaidi ya CCM? Watatuhakikishiaje kwamba CCM hawawezi kutumia machinery ya dola kuiba kura hata kama tukiwapigia upinzani, tume ya uchaguzi ni ya CCM!
Samahani kwa kuuliza maswali mengi kuliko majibu kwa sababu na mimi sijaona majibu ya maswali haya, majibu ambayo yanaweza kuwafanya watu waweke imani katika upinzani na kuamua kuwatoa CCM.
CCM wanayo yote hayo uliyoyauliza?
duh, umetupiga sana. Hata hivyo unfairly. Unapoangalia makosa ya kambi ya upinzani ni vema uangalie 'factors' za ndani na za nje. Katika swot analysis hizi ni fursa na vitisho. Hapo utaweza kutoa hukumu sahihi kabisa.
Vilevile ni muhimu sana kuangalia historia ya vyama hivi katika muktadha wa historia ya tanzania na utamaduni wa kisiasa wa watanzania. Vyama katika nyakati tofauti - kuanzia kina marando na bagenda, mtei na makani, fundikira na kasanga tumbo na mapalala na seif walipoamua kujitoa mhanga na kuanzisha vyama - kumekuwa na hatu kadhaa zimepigwa katika kujenga dmeokrasia ya kweli katika nchi yetu.
Watu wanaiweka tanzania katika mizania ya nchi nyingine jambo ambalo ni kosa kubwa maana tanzania inapaswa kupimwa kutokana na historia yake. Zoezi la ujenzi wa taifa na kuwa na taifa moja chini ya uongozi mahiri wa mwalimu lilifanywa katika misingi ya udikteta mkubwa sana na chini ya amri moja ya 'zidumu fikra za mwenyekiti'. Tanzania ikajenga jamii ya watu wanaoheshimu mamlaka bila kuhoji na hata vyama vingi vilipoanzishwa vilionekana ni vya wasaliti. Ni mtu mmoja tu mpaka sasa ambaye alikonga nyoyo za watanzania na kuaminiwa - augustino lyatonga mrema - lakini naye akavurugwa sana na dola, kuitwa pandikizi na kuondoa kabisa credibility yake katika jamii. Jamii imefanywa kuamini kuwa mrema ni 'kichaa' na hana sifa ya uongozi. Hii ni kazi iliyopangwa na kutekelezwa kwa ustadi mkubwa kiasi kwamba leo ni watanzania wachache sana ambao wanakumbuka sacrifice ya mrema katika ujenzi wa demokrasia nchini.
Tusipojifunza na kuelewa historia hii ya vuguvugu la demokrasia tanzania tutaishia kulaumu watu kila kukicha bila kwenda mbele. Ccm itaendelea kutawala na kila baada ya miaka mitano kutakuwa kinatokea chama kina nguvu na baadae kuangushwa, wabunge wenye nguvu na baadae kuangushwa na hata wanasiasa wenye mvuto na baadae kupakwa matope na kunuka.
Demokrasia hulindwa. Viongozi hulindwa zaidi ili kubakia kama alama ya harakati. Raila odinga aliongoza harakati za mapinduzi kenya mwaka 1982, akaswekwa lupango kwa miaka zaidi ya tisa na kuishi uhamishoni nchini norway kwa miaka mingi. Akajiunga na chama cha baba yake mwaka 1992 ford, kikavunjika na kuwa na ford-k na ford-a. Baba yake mzee jaramogi alipokufa raila akataka kunyakua uongozi wa chama, akashindwa na michael kijana wamalwa na raila akaenda kuanzisha chama chake ndp. Akaivunja ndp na kuingia kanu kuwa katibu mkuu na akaipasua kanu vipande 2 na kuanzisha ldp. Akaingiza ldp katika muungano wa narc na kumpa kibaki urais (literally alimpa urais maana kibaki alikuwa armchair leader of opposition). Akatoka narc na kuanzisha odm-k, akagombana na kalonzo na kuanzisha odm na leo ni waziri mkuu mwenye nguvu kenya.
Mchakato wote huu raila alionekana msaliti, mpenda vyeo na mtu wa vita. Lakini leo huna tena kanu na raila alipata kuniambia, demokrasia afrika itaimarika tu iwapo vyama vilivyoleta uhuru vitapasukapasuka na kuondoa ile claim yao ya sisi tulileta uhuru - hii ni claim ya ccm na hata kumkumbatia mwalimu kama wao.
Lakini tuna kina raila tanzania? Mazingira ya kisiasa yanatoa fursa ya kujenga kina raila?
Unawezaje kupewa dola ilhali vyombo vya dola havikuamini? Maana taifa haliongozwi na siasa tu. Idara za usalama na majeshi zina nafasi kubwa sana katika kuamua mustakabali wa nchi. Wanasiasa wa tanzania ni mara ngapi tunajenga rappour na watu wa usalama ili angalau kujua wanawaza nini. Hakuna.
Mwanakijiji utaandika mpaka utachoka na kutulaumu mpaka utakasirika. Demokrasia ya tanzania itajengwa kwa sober approach ya kutazama historia yetu na kujua 'political culture' ya watanzania. Unatutaka tuchukue fursa inapotokea. Wazo murua kabisa. Lakini capacity ipo wapi? Wapo wap wanaofikiri na kuziona fursa? Wapo wapi watu wanaojenga scenerios na kujiuliza what if?
Tulianza vizuri zoezi la kujenga imani kwa wananchi kupitia bunge. Tulifanikiwa kupata sizable number ya wabunge wa ccm na kujenga coalition nzuri na kupashana habari. Tukamezwa. Tukajikuta tumewauzia ajenda tukijua kabisa hawatafika nayo mbali.
Ndani ya ccm hivi sana wanachowaza ni nani atakuwa rais ajaye kati ya membe na lowasa. Hakuna ajenda ya taifa, hakuna vision pale. Lakini wanasiasa wa upinzani tunaimba nyimbo zao hawa mabwana na hata 'opinion makers' kama wewe mwanakijiji mnaimba nyimbo zao.
Juzi nilisema hapa jf, lets be sober and scan the political situation objectively. Kinachoniumiza kichwa ni kwamba, kuna vijana wachache katika vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wamechoka na bickerings za wanasiasa. Watataka ku restore order! Mzee sarakikya aliiwahi kuniasa kuwa tusiruhusu hali hiyo itokee kwani ikitokea hawatarudi makambini! Ili isitokee kuna haja ya kufikiri vizuri - ignore ccm
kama ambavyo wewe mheshimiwa zito ambavyo umekuwa ukitungiwa uongo,fitna na majungu na wapambe wa mbowe wanaohisi amani ya wao kutawala inahatarishwa na wewe.
Nimesikitika sana kusikia kuwa mbowe bado ana bifu la uchaguzi.umemuachia nafasi na kashinda kwa asilimia 96 bado analia kuwa anawafukuza wanachama wengine. Kweli tuna safari ndefu sana.kwenye demokrasia ya vyama mimi naona cuf wako juu kuliko utumbo anaoufanya mbowe na wenzake.
WildCard,Na ndio maana niliwahi kutoa maoni yangu humu kwamba kuna makundi mawili hapa nchini hatujayatumia vizuri.
Moja ni wafanyakazi wa Nchi hii. Tangu walipoondoka CCM ambako ilikuwa ni Jumuia kama UWT wamebaki yatima. Matokeo yake kila mfanyakazi na lwake. Baadhi wamejiunga na mafisadi wa CCM kuambulia angalau makombo.
Kundi la pili ni wanafunzi na wanavyuo mbalimbali. Nadhani wewe Zitto ulijiunga na CHADEMA ungali chuoni. Sasa hivi tumewakatisha tamaa wanavyuo wetu. CCM bado wana CHIPUKIZI wao. Watoto wadogo kabisa wanaiimbia CCM, wanazima Mwenge, wanacheza halaiki. Upinzani hamlikemei hili. Watoto wetu wanazaliwa na vyama kama wanavyozaliwa na KABILA na DINI za wazazi wao.
You are the living proof,kama sample wamekuchukua wewe, median,standard variation n.k zimeangukia kwenye point inayoitwa Mwafrika.Umezisikia wapi hizi habari?