Makosa ya mwanaume yanayosababisha mke amsaliti

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
MAKOSA YA MWANAUME YANAYOSABABISHA MKE AMSALITI



Kuna sababu anuai zinazomfanya mwanamke amsaliti mumewe. Ni muhimu kutambua kuwa mwanamke ni kiumbe mwenye hisia kali na daima ahisi raha na amani. Baadhi ya nyakati hufanya usaliti ili kuziba pengo la upungufu unaotokea katika maisha yake. Zifuatazo ni sababu kubwa ambazo zinamfanya amsaliti mumewe:

1. KUTOMPA KIPAUMBELE NA KUTOMTHAMINI

Tunatambua kuwa mke anafanya kazi kubwa sana ambayo lau kama ingekuwa ni kampuni basi pangehitajika watu zaidi ya 10 kuzifanya. Atamtunza mume, watoto, nyumba na familia kwa ujumla.

Wakati fulani mume anaweza akampuuza na asimthamini, licha ya kujitoa kwa moyo wote kumtunza na kuihudumia familia. Hivyo, kutotoa kipaumble kwa mke ni kosa kubwa ambalo linaweza likamgharimu mume, mke akipata mtu anayempa kipaumbele na kumuonesha thamani hakika hataacha kuitumia hiyo fursa.

2. UKOSEFU WA MAHABA

Kwa asili mwanamke ana silika ya hitajio la kupendwa, mwanamke anahitaji kupendwa, mwanaume yeye ana silika ya kupenda ngono, ukimpa ngono tu basi anaridhika.

Mwanamke anahitaji kupetiwapetiwa, anahitaji kudekezwa, anahitaji aambiwe maneno yenye ladha adimu yaliyochanganywa na vionjo vya ndimu, mwanamke anataka hivyo, anataka aone kama anapendwa, anataka aone mtu anamwambia vile alivyo, alivyo maridhawa, amueleze hisia zake, ampe lugha ya kimajnun, mwanamke anamtaka Majnun. Sasa akimpata mtu wa aina hiyo, tofauti na mumewe, huwa ni balaa tupu, mnanipata hapo?

3. USALITI WA MUME

Miongoni mwa mambo ambayo huibadilisha roho ya mwanamke ni pale anapogundua kuwa mumewe kipenzi anamsaliti. Hapo mwanamke anaweza akabadilika kabisa. Wapo wanaosamehe, lakini wapo wanaolipiza kisasi.

4. KUTOJIAMINI

Mwanamke anahitaji mwanaume anayemfanya ajiamini iwapo mumewe hatekelezi jukumu hilo, akimpata mtu anayemfanya ajiamini, yanaweza kutokea mengine kabisa. Hivyo, nasaha zangu kwa kaka zangu kuyaangalia kwa makini mambo haya.
 
Asante kwa mada hii.
Ukweli unabaki kuwa unaweza ukaandika unavyoweza kuandika ILA hakuna sababu za kumfanya mwanandoa kuisaliti ndoa yake Kama ambavyo hakuna sababu ya kumfanya mwanandoa kutosaliti ndoa yake zaidi ya " UAMINIFU" .
Hatupaswi kuwatendea vibaya wale tunaowapenda Na ambao tuna ahadi za uaminifu. Mwanaume anapaswa kuishi Na mkewe kwa namna inavyopasa, vivyo hivyo
Mke naye anapaswa kuishi sawa sawa Na kiapo chake.
Sababu zote ulizoweka Ni " subjective" kwa mazingira Na namba ambavyo watu wanatafsiri.
Kwa mke wangu kujali unaweza kuwa kumpeleka shopping kila mwezi, kwa mwingine unaweza kuwa kuwahi kurudi nyumbani na kutumia muda mwingi pamoja naye.
Asante kwa tafakuri
 
Ndoa ni eneo pana sana linalohitaji uelewa mpana kabla ya kuliendea....wanandoa wengi wanaingia kwenye ndoa bila ya kuwa na uelewa mpana kwenye ndoa zaidi ya hisia za kimapenzi zilitawala kwenye nyoyo zao....

Hisia hizo kali za mapenzi zinawafanya wawe vipofu na wasiuone ulimwengu halisi wa maisha....
Matatizo mengi yanayozikumba ndoa za nyakati hizi ni ishara ya kuwa wanandoa wengi hawajui maana ya ndoa na hata hawajui hata kwanini wameoana....
Tukisimama katika misingi ya ndoa na kwa kuzingatia maana halisi ya ndoa huwezi kukuta mtu anathubutu au anafikiria kumsaliti mpenzi wake...kwa kuwa yule aliyemchagua ndiye ambaye anaishi ndani ya nafsi yake...

Tukisimama katika misingi ya ndoa haiwezekani mume asimjali mke wake...haiwezekani mke asimvumilie mume wake wakati wa kipindi kigumu cha hali ya maisha....
Katika misingi ya ndoa haiwezekani kwa mume anayejitambua kumkwaza mkewe ambaye ndiye malikia wa moyo wake bali atamfanya kuwa chanzo cha furaha yake maishani mwake...
Katika misingi ya ndoa huwezi kukuta mwanandoa akitoa siri za ndani kwani wao wote ni mwili mmoja....

Vijana kabla ya kuingia kwenye ndoa wanatakiwa wapate mafundisho yanayohusu ndoa kupitia imani zao....kwani kuna neema na baraka tele kwenye kumshirikisha muumba kwenye jambo lenye kheri kama hilo kwani daima Mungu kupitia mafunzo yake hutupa miongozo sahihi....
 
human beings are never the same, kilicho muhim kwa mmoja kwa mwingine ni useless, huko kupetiwa kuna mwingine anataka pesa tu. Kuna mwingine anataka muonekano wa mumewe n so on. Kuna wadada hua wanacheat for no reason kwa io hakuna 7 maalum
 
Back
Top Bottom