JERICKO UKO SAHIHI ASILIMIA ZOTE MFIKISHIE MAULIDI KITENGE UJUMBE KUWA KAMA NINGEKUWA MIMI KITENDO CHA KUNIGUSA NIKIWA NA SILAHA SASA HIVI ANGEPUMZIKA KWA AMANI NA PIA NI KWELI ASKARI YULE SIJUI ALIPANIC NINI WAKATI ANA SILAHA ANGEMWONYESHA KITAMBULISHO KISHA KWA UPOLE AKAMWAMBIA RUDI ALIKOTAKATA AENDE HAPO KAMA ANGEKATAA BADO HAKUWA NA SABABU YA KUTOA SILAHA ANGEITA ASKARI WENGINE AKABEBWA KWA NGUVU NA KUTUPWA KWENYE GARI SASA BAADA YA HAPO KAMA UPINZANI UNGETOKEA NDIYO SILAHA ITOKE SIYO KUTISHIA BALI KUPIGA KILICHOKUSUDIWA KUPIGWA KIHEREHERE CHA MAULIDI SIKU NYINGINE ATAJUTA KUZALIWA NA DHARAU ZAKE MJINGA HUYO.Tukio la kuzuiwa Mkutano wa Mh Nape kuzungumza na wanahabari ni jambo mtambuka, mimi leo nataka nilichambue tukio la askari kumtishia bunduki bwana Nape Nnauye. Naliangalia katika mtazamo wa kitaalamu zaidi.
Kwanza tujifunze mambo machache,
Polisi nini? Hili watu wamekuwa wakilichanganya, Kuwasaidia maana ya neno POLICE ni People's Oorder, Law, lnvestigation and Criminal Enforcements kwamjibu wa Wagiriki, lakini Wazungu wanasema ni Law enforcement and criminal investigation..not vice Verser. Kisha tujifunze utendaji kazi wa huyu mtu aitwaye polisi upoje hapa Tanzania na duniani kote, kwakuwa sheria ni moja japo zinaweza kutofautia kidogo tu kimaumbile na kiutekelezaji lakini msingi wake ni mmoja.
Criminal investigation procedure kupitia criminal investigation Act inamruhusu askari kutumia nguvu pale tu mtuhumiwa anapoonesha ubishi wa kutotii.
Pia sheria hiyohiyo inamtaka, hii ni lazima sio ombi, askari kujitambulisha ikiwa ni Pamoja na kuonesha kitambulisho kabla "hajaanza" utekelezaji wa majukumu yake.
Kwa dhana na uhalisia wa video hii ninayoitumia kama msingi wa uchambuzi, Mh Nape alikuwa sahihi kumuuliza yeye ni nani na akaomba kitambulisho. Kwa hatua hiyo tu, yule askari ana makosa hata kama ni askari uliyevaa sare au umevaa kiraia kama huyu, ukitaka kumkamata mtu lazima ujitambulishe wewe nani na unatokea kituo gani kisha ufanye yako kwa raia sio kwa kwa utaratibu ule hata kwa mazingira gani, Nape pia ana haki yakujua huyo polisi ni nani.
Suala la kutoa silaha lina mambo mengi ya kitaalamu, Kisheria askari popote ulipo unatakiwa kuwa armed muda wote, lakini kuwa armed si kumpoint mtu gun ambaye ni unarmed wala hajaonesha dalili ya madhara kwako. Hili ni kosa kubwa kwa askari huyu.
Polisi yule anaweza kuwa na utetezi wenye hoja na usipokuwa makini unakubaliana naye kwamba aliona Nape yupo peke yake ndio lakini alikuwa amezungukwa na watu anaoamini ni wafuasi wake. Katika mazingira kama yale ambayo watu wengi wamejaa ambao kwa tafsiri ya kawaida ni watu wanaomuunga mkono nape, unategemea silaha itoke baada ya vurugu kuanza? Hii ni hoja nzito na inamruhusu askari kutoa silaha, lakini hoja hiyo inakufa kwenye kitendo cha kumuelekeza silaha mtu aliyesimama na hana silaha yoyote,
Askari huyu anaweza kujitetea tena kwamba alipomuona mtuhumiwa huyu kasimama alikuwa ameweka mikono mfukoni mwa suruali yake hali iliyomfanya yeye askari afikiri huyu mtu ana silaha,hivyo akamuwahi kwakunyooshea silaha.
Lakini utetezi huu unafutwa na kitendo cha yeye awali kwenda moja kwa moja kwa mtuhumiwa na kumshika na kumsukuma arudi kwenye gari, sauti ya video inasikika mtuhumiwa akimtaka mtu huyu anayedhaniwa ni askari ajitambulishe kwa kuonyesha kitambulisho jambo ambalo lilikuwa rahisi tu lakini ghafla akachomoa silaha na kumnyooshea mtuhumiwa.
Lakini nikitumia video hii namuona askari huyu anatumia silaha kizembe sana huyo angekutana na wenye mafunzo angekuwa chini silaha ingenyang'anywa,.
Kwaasili ukimtazama anaonekana akiihamisha silaha mkono wa kulia baada ya kuitoa kwa mkono wa kushoto,hii inamaana anatumia mkono wa kulia, lakini silaha aliweke kiunoni upande wa kushoto, hali inayomfanya achelewe kuichomoa kiunoni, silaha inatolewa zaidi ya sekunde 60 mpaka anapigwa picha nyingi, tazama hiyo picha Nape angekuwa mtaalamu wa mapigano ya kujihami kijasusi alikuwa anaweza kupiga teke au kifuti na kushika mkono wenye silaha na kumpora.
Kosa la pili ni la polisi waliomzunguka huyu aliyetoa silaha mpaka wakaacha raia Maulidi Kitenge kumvaa yule askari.
Tena Maulid Kitenge japo huenda hajui sheria lakini kafanya kosa kubwa sana kuwaingia wakati wakitimiza kazi zao. Kwa askari makini huyu Kitenge tungeimba iyena iyena leo. Ni kwa kosa la baadhi ya Wanausalama kuwa Wabaridi kumwacha Maulid amsukume Afisa active katika situations ile. Ukweli Maulid kawaponza askari walio Dormant hadi akaingilia mission kiasi cha kuhatarisha Usalama wa mwenzao ambae Silaha yake tayari alikwisha weka kwenye chamber
Kwa minajiri hii, Askari waliokuaa kwenye opaesheni hii wanatakiwa kuwajibishwa kwa ukiukwaji kwa sheria kanuni na taratibu za kazi ya uaskari wao,
Lakini askari aliyetishia kwa silaha atakiwa kuadhibiwa kwa uzembe, suala lake ninadhani huwezi kulipeleka kwenye mahakama ya kiraia labda ya kijeshi, kwa mtazamo wangu, yale ni makosa katika oparesheni za kiusalama ambapo anaweza kushitakiwa katika mahakama ya kijeshi. Msingi wa kesi ya kiraia unaweza kuita ni kvamiwa na mtu mwenye silaha anayedhaniwa ni jambazi. Wataalamu wa sheria za kiraia kina Tundu Lissu, Peter Kibatala, John Mallya, Ben Alex Ishabakaki, Jebra Kambole Sr. Na wengine mnaweza kulifafanua vizuri hili...
Na Yericko Nyerere
Hivi kwani ungecomment bila quote asingeona?Hivi Nape ni Mtuhumiwa wa nini ?
Tukio la kuzuiwa Mkutano wa Mh Nape kuzungumza na wanahabari ni jambo mtambuka, mimi leo nataka nilichambue tukio la askari kumtishia bunduki bwana Nape Nnauye. Naliangalia katika mtazamo wa kitaalamu zaidi.

Hatujasoma hbr ya CID au amefuta na au amerekebisha?Sujui kama ni kwa kukusudia auni uelewa wako ila nadhani hilo hitimisho lako kwamba yule bwana anatoka idara ya CID kwenye jeshi la polisi linaweza kuwa na walakini bwana Yericko. Wanausalama wasiovaa sare wapo wa aina nyingi sana.
Rejea kauli ya Waziri Mwigulu leo!
Hivi Nape ni Mtuhumiwa wa nini ?
Aliombwa ajitambulishe ila hakutii ombi hilo, kwahiyo ni vigumu kumtambua kuwa ni polisi na ndio maana maulidi kitenge alimwambia unaharibu kwa kuwa alijua ni msela fulani hivi!Binafsi nilimuona alievaa shati jeupe kama mtu alie composed and professional...
Kuna wanaompongeza Kitenge. Lakini kwa sheria zetu amezuia askari kufanya kazi yao....kitu ambacho kinaweza kumsumbua, hata kama walikuwa hawajajitambulisha, gari aliloamriwa aingie ni lake na dereva ni wake
Kuhusu makosa ya askari, nadhani kulikuwa na pressure kubwa sana kwa pande zote mbili...it happens.. Ndio mambo ya kazi
Wenye makosa zaid ni waliotuma askari na kutaka kumzuia Nappe kuzungumza, dont twist the thing around...
Aliewatuma wale askari kumzuia Nappe ndio source ya yote hayo...
Kwamba Nappe ni X Min. Anaweza pigiwa tu simu kawaida na yeye akaamua cha kufanya...
But you dont have the right to kill freedom of speech from our countrt, no one....unlikely and un acceptable in any democratic state
Shukrani sana kwa maelezo mazuri mkuuMkuu Yericko,
Hao ni makachero wa polisi na walitumwa kwenda kuzuia huo mkutano wa Nape na waandishi wa habari.
Ukimwangalia huyo mwenye jinsi ya blue na fulana nyeupe na kofia unagundua kuwa yeye ndiye kiongozi (team leader) na pia ukiangalia mifuko ya nyuma ya suruali yake mmojawapo una pingu ndani yake na inaonekana wazi.
Kwa kuwa tayari hoteli ilikwishaagizwa kwamba hakuna kuandaa mkutano basi Nape na akina Kitenge wakaamua kuufanyia nje.
Nakubaliana kabisa na wewe kwamba hilo lilikuwa ni kosa la kiufundi kwa hao askari kanzu.
Kwanza, hawakuwa na uhakika kwa asilimia 100 kwamba wanamkabili mtu ambae masaa machache yalopita alikuwa ni waziri hivyo kupelekea kutahayari.
Hiyo inategemea na aina ya mtu waliemkuta ingawa waliweza kumzaba makofi Profesa Lipumba na akaingia kwenye karandika mwaka mmoja ulopita.
Pili, alipaswa kujitambulisha na pia kuamuru wenzie wasambaze watu ili apate nafasi nzuri ya kuzungumza na Nape.
Kwa kifupi hiyo ni technical blunder na kama mimio ningekuwa commanding officer ningwaita training room kwa breefing na ningewaonyesha hiyo video ili wajifunze makosa yao.
Ila uko sawa wanapaswa kuadhibiwa na jeshi na sio mahakama ya kiraia kulingana na hali ilivyokuwa mahali pale kwamba hata Maulidi wa Kitenge nae aligeuka kuwa mlinzi wa Nape.
Lakini cha msingi ni kwamba wao walitumwa na RPC kumzuia Nape kuzungumza na siyo kumkamata hivyo hakukuwa na haja ya kutoa silaha kwani makosa ni yao (polisi kwa kushindwa kufika mahala pale mapema asubuhi kwa ajili ya kufanya "sweeping".
Mkuu asante sana mkuu wanguAsante lakini point of correction,"...silaha yake tayari alikwisha weka kwenye chamber".Hapa ilibidi useme "risasi ilikua kwenye chamber" ingawa kwa mujibu wa taaluma ya ballistics kwa video ilivyo ni ngumu kujua hata kana ile handfun(pistol) ilikua na risasi maana video haijaonyesha bali nimeona jamaa ameshika silaha tu.10 cimmandments of firearms miongoni mwazo
-Treat every firearm as if it were loaded.
-Do not put a finger on a trigger until targert is ready to be fired. Etc;
Sasa silaha inamfumo wa Internal na external.Kwa hapa niongelee internal ballistics,risasi inapokua ndani ya magazine na ikachomekwa tayari internal ballistic processes inaanza kuapply na risasi ikishatoka na catriage kutika ndipo tunaita external ballistics.
Sasa ukiangalia video ili risasi iweze kupelekwa kwenye chamber ni lazima kuklcock breech ili risasi iwe tayari kutega primer kupigwa na firing pin lakini video inaonyesha jamaa kachomoa na kaonyesha bila kucock.Lakini yawezekana risasi ilikua kwa chamber ila alifunga usalama yaani safety catch kwa maana ukifunga risasi iliyo kwa chamber haiwezi toka hata ukisqeez triger.
Anyway msingi wa neno langu ni kwamba ilitakiwa useme "... Risasi ikiwa chamber" na sio silaha ilikua chamber.
Asante sana.
We ni mwana sheria au mjuaji wa mjini tuu?Maulidi kitenge hawezi kuwa na hatia kumsaidia raia ambaye amekidwa na watu wasiojulikana!. Laiti wangejitambulisha kuwa ni Maaskari hapo sawa, lakini hawakujitambilisha!
Nisamehe mkuu , natumia Tecno ya tochi , viwango vyake ni vidogo .Hivi kwani ungecomment bila quote asingeona?
Ngoja nimchunguze .Yaonyesha maulidi na yule mtoa silaha wanafahamiana kwa sababu nyingi tu mfano ni pale maudi alipogoma yule Bashite no 2'alionyesha kusikia na kupoa