Makosa ya kitaalamu Oparesheni Nape

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,997
20,329
Tukio la kuzuiwa Mkutano wa Mh Nape kuzungumza na wanahabari ni jambo mtambuka, mimi leo nataka nilichambue tukio la askari kumtishia bunduki bwana Nape Nnauye. Naliangalia katika mtazamo wa kitaalamu zaidi.

Kwanza tujifunze mambo machache,
Polisi nini? Hili watu wamekuwa wakilichanganya, Kuwasaidia maana ya neno POLICE ni People's Oorder, Law, lnvestigation and Criminal Enforcements kwamjibu wa Wagiriki, lakini Wazungu wanasema ni Law enforcement and criminal investigation..not vice Verser. Kisha tujifunze utendaji kazi wa huyu mtu aitwaye polisi upoje hapa Tanzania na duniani kote, kwakuwa sheria ni moja japo zinaweza kutofautia kidogo tu kimaumbile na kiutekelezaji lakini msingi wake ni mmoja.

Criminal investigation procedure kupitia criminal investigation Act inamruhusu askari kutumia nguvu pale tu mtuhumiwa anapoonesha ubishi wa kutotii.

Pia sheria hiyohiyo inamtaka, hii ni lazima sio ombi, askari kujitambulisha ikiwa ni Pamoja na kuonesha kitambulisho kabla "hajaanza" utekelezaji wa majukumu yake.

Kwa dhana na uhalisia wa video hii ninayoitumia kama msingi wa uchambuzi, Mh Nape alikuwa sahihi kumuuliza yeye ni nani na akaomba kitambulisho. Kwa hatua hiyo tu, yule askari ana makosa hata kama ni askari uliyevaa sare au umevaa kiraia kama huyu, ukitaka kumkamata mtu lazima ujitambulishe wewe nani na unatokea kituo gani kisha ufanye yako kwa raia sio kwa kwa utaratibu ule hata kwa mazingira gani, Nape pia ana haki yakujua huyo polisi ni nani.

Suala la kutoa silaha lina mambo mengi ya kitaalamu, Kisheria askari popote ulipo katika misheni yoyote unatakiwa kuwa armed muda wote, lakini kuwa armed si kumpoint mtu gun ambaye ni unarmed wala hajaonesha dalili ya madhara kwako. Hili ni kosa kubwa kwa askari huyu.

Polisi yule anaweza kuwa na utetezi wenye hoja na usipokuwa makini unakubaliana naye kwamba aliona Nape yupo peke yake ndio lakini alikuwa amezungukwa na watu anaoamini ni wafuasi wake. Katika mazingira kama yale ambayo watu wengi wamejaa ambao kwa tafsiri ya kawaida ni watu wanaomuunga mkono nape, unategemea silaha itoke baada ya vurugu kuanza? Hii ni hoja nzito na inamruhusu askari kutoa silaha, lakini hoja hiyo inakufa kwenye kitendo cha kumuelekeza silaha mtu aliyesimama na hana silaha yoyote,

Askari huyu anaweza kujitetea tena kwamba alipomuona mtuhumiwa huyu kasimama alikuwa ameweka mikono mfukoni mwa suruali yake hali iliyomfanya yeye askari afikiri huyu mtu ana silaha,hivyo akamuwahi kwakunyooshea silaha.

Lakini utetezi huu unafutwa na kitendo cha yeye awali kwenda moja kwa moja kwa mtuhumiwa na kumshika na kumsukuma arudi kwenye gari, sauti ya video inasikika mtuhumiwa akimtaka mtu huyu anayedhaniwa ni askari ajitambulishe kwa kuonyesha kitambulisho jambo ambalo lilikuwa rahisi tu lakini ghafla akachomoa silaha na kumnyooshea mtuhumiwa.

Lakini nikitumia video hii namuona askari huyu anatumia silaha kizembe sana huyo angekutana na wenye mafunzo angekuwa chini silaha ingenyang'anywa,.

Kwaasili ukimtazama anaonekana akiihamisha silaha mkono wa kulia baada ya kuitoa kwa mkono wa kushoto,hii inamaana anatumia mkono wa kulia, lakini silaha aliweke kiunoni upande wa kushoto, hali inayomfanya achelewe kuichomoa kiunoni, silaha inatolewa zaidi ya sekunde 60 mpaka anapigwa picha nyingi, tazama hiyo picha Nape angekuwa mtaalamu wa mapigano ya kujihami kijasusi alikuwa anaweza kupiga teke au kifuti na kushika mkono wenye silaha na kumpora.

Kosa la pili ni la polisi waliomzunguka huyu aliyetoa silaha mpaka wakaacha raia Maulidi Kitenge kumvaa yule askari.
Tena Maulid Kitenge japo huenda hajui sheria lakini kafanya kosa kubwa sana kuwaingia wakati wakitimiza kazi zao. Kwa askari makini huyu Kitenge tungeimba iyena iyena leo. Ni kwa kosa la baadhi ya Wanausalama kuwa Wabaridi kumwacha Maulid amsukume Afisa active katika situations ile. Ukweli Maulid kawaponza askari walio Dormant hadi akaingilia mission kiasi cha kuhatarisha Usalama wa mwenzao ambae Silaha yake tayari alikwisha weka kwenye chamber

Kwa minajiri hii, Askari waliokuaa kwenye opaesheni hii wanatakiwa kuwajibishwa kwa ukiukwaji kwa sheria kanuni na taratibu za kazi ya uaskari wao,

Lakini askari aliyetishia kwa silaha atakiwa kuadhibiwa kwa uzembe, suala lake ninadhani huwezi kulipeleka kwenye mahakama ya kiraia labda ya kijeshi, kwa mtazamo wangu, yale ni makosa katika oparesheni za kiusalama ambapo anaweza kushitakiwa katika mahakama ya kijeshi. Msingi wa kesi ya kiraia unaweza kuita ni kvamiwa na mtu mwenye silaha anayedhaniwa ni jambazi. Wataalamu wa sheria za kiraia kina Tundu Lissu, Peter Kibatala, John Mallya, Ben Alex Ishabakaki, Jebra Kambole Sr. Na wengine mnaweza kulifafanua vizuri hili...

Na Yericko Nyerere
 
Attachments

  • VID-20170323-WA0854.mp4
    1.1 MB · Views: 63
Nnape ni mvumilivu sn kuliko mimi. NAOGOPA KUFA KIZEMBE... huyo mwana usalama angelamba HEAD nzur mno sidhan km angeinuka akaiona siraha yake...(hata nchi yenyewe haina uwezo wa compasate kifo changu) sasa kwanini nisimuadhibu anaetaka kuniua haraka kadri mungu atakavyo nijalia?. Pia vyombo vya USALAMA kuna haja ya kuamin kuwa kuna wenye tekniks nzur kumumaliza adui kwa wered zaid kuliko huyo anaeamin ni proffesional..! Watu wabajua kungfu,boxing,taikwando,acrobatic, na kutumia siraha kwa wepes zaid ya wanausalama ...hivyo tueshim kila raia...kwa mazingira yake. Kila taaluma ina tabia zake..ila kwa jana taaluma ya uandishi wa habari jukaaa mbele ya camera kuchukua video kwa wtu wanaopigana tena mmoja ana siraha....kuna taaluma nyingine zinaelekeza kila kitu ni siraha ya kujiham..hapo camera ndo ingekuwa fimbo ,jiwe na siraha kali..kuliko kilichofanyika.
 
Sujui kama ni kwa kukusudia auni uelewa wako ila nadhani hilo hitimisho lako kwamba yule bwana anatoka idara ya CID kwenye jeshi la polisi linaweza kuwa na walakini bwana Yericko. Wanausalama wasiovaa sare wapo wa aina nyingi sana.

Rejea kauli ya Waziri Mwigulu leo!
 
Tukio la kuzuiwa Mkutano wa Mh Nape kuzungumza na wanahabari ni jambo mtambuka, mimi leo nataka nilichambue tukio la askari kumtishia bunduki bwana Nape Nnauye. Naliangalia katika mtazamo wa kitaalamu zaidi.

Kwanza tujifunze mambo machache,
Polisi nini? Hili watu wamekuwa wakilichanganya, Kuwasaidia maana ya neno POLICE ni People's Oorder, Law, lnvestigation and Criminal Enforcements kwamjibu wa Wagiriki, lakini Wazungu wanasema ni Law enforcement and criminal investigation..not vice Verser. Kisha tujifunze utendaji kazi wa huyu mtu aitwaye polisi upoje hapa Tanzania na duniani kote, kwakuwa sheria ni moja japo zinaweza kutofautia kidogo tu kimaumbile na kiutekelezaji lakini msingi wake ni mmoja.

Criminal investigation procedure kupitia criminal investigation Act inamruhusu askari kutumia nguvu pale tu mtuhumiwa anapoonesha ubishi wa kutotii.

Pia sheria hiyohiyo inamtaka, hii ni lazima sio ombi, askari kujitambulisha ikiwa ni Pamoja na kuonesha kitambulisho kabla "hajaanza" utekelezaji wa majukumu yake.

Kwa dhana na uhalisia wa video hii ninayoitumia kama msingi wa uchambuzi, Mh Nape alikuwa sahihi kumuuliza yeye ni nani na akaomba kitambulisho. Kwa hatua hiyo tu, yule askari ana makosa hata kama ni askari uliyevaa sare au umevaa kiraia kama huyu, ukitaka kumkamata mtu lazima ujitambulishe wewe nani na unatokea kituo gani kisha ufanye yako kwa raia sio kwa kwa utaratibu ule hata kwa mazingira gani, Nape pia ana haki yakujua huyo polisi ni nani.

Suala la kutoa silaha lina mambo mengi ya kitaalamu, Kisheria askari popote ulipo unatakiwa kuwa armed muda wote, lakini kuwa armed si kumpoint mtu gun ambaye ni unarmed wala hajaonesha dalili ya madhara kwako. Hili ni kosa kubwa kwa askari huyu.

Polisi yule anaweza kuwa na utetezi wenye hoja na usipokuwa makini unakubaliana naye kwamba aliona Nape yupo peke yake ndio lakini alikuwa amezungukwa na watu anaoamini ni wafuasi wake. Katika mazingira kama yale ambayo watu wengi wamejaa ambao kwa tafsiri ya kawaida ni watu wanaomuunga mkono nape, unategemea silaha itoke baada ya vurugu kuanza? Hii ni hoja nzito na inamruhusu askari kutoa silaha, lakini hoja hiyo inakufa kwenye kitendo cha kumuelekeza silaha mtu aliyesimama na hana silaha yoyote,

Askari huyu anaweza kujitetea tena kwamba alipomuona mtuhumiwa huyu kasimama alikuwa ameweka mikono mfukoni mwa suruali yake hali iliyomfanya yeye askari afikiri huyu mtu ana silaha,hivyo akamuwahi kwakunyooshea silaha.

Lakini utetezi huu unafutwa na kitendo cha yeye awali kwenda moja kwa moja kwa mtuhumiwa na kumshika na kumsukuma arudi kwenye gari, sauti ya video inasikika mtuhumiwa akimtaka mtu huyu anayedhaniwa ni askari ajitambulishe kwa kuonyesha kitambulisho jambo ambalo lilikuwa rahisi tu lakini ghafla akachomoa silaha na kumnyooshea mtuhumiwa.

Lakini nikitumia video hii namuona askari huyu anatumia silaha kizembe sana huyo angekutana na wenye mafunzo angekuwa chini silaha ingenyang'anywa,.

Kwaasili ukimtazama anaonekana akiihamisha silaha mkono wa kulia baada ya kuitoa kwa mkono wa kushoto,hii inamaana anatumia mkono wa kulia, lakini silaha aliweke kiunoni upande wa kushoto, hali inayomfanya achelewe kuichomoa kiunoni, silaha inatolewa zaidi ya sekunde 60 mpaka anapigwa picha nyingi, tazama hiyo picha Nape angekuwa mtaalamu wa mapigano ya kujihami kijasusi alikuwa anaweza kupiga teke au kifuti na kushika mkono wenye silaha na kumpora.

Kosa la pili ni la polisi waliomzunguka huyu aliyetoa silaha mpaka wakaacha raia Maulidi Kitenge kumvaa yule askari.
Tena Maulid Kitenge japo huenda hajui sheria lakini kafanya kosa kubwa sana kuwaingia wakati wakitimiza kazi zao. Kwa askari makini huyu Kitenge tungeimba iyena iyena leo. Ni kwa kosa la baadhi ya Wanausalama kuwa Wabaridi kumwacha Maulid amsukume Afisa active katika situations ile. Ukweli Maulid kawaponza askari walio Dormant hadi akaingilia mission kiasi cha kuhatarisha Usalama wa mwenzao ambae Silaha yake tayari alikwisha weka kwenye chamber

Kwa minajiri hii, Askari waliokuaa kwenye opaesheni hii wanatakiwa kuwajibishwa kwa ukiukwaji kwa sheria kanuni na taratibu za kazi ya uaskari wao,

Lakini askari aliyetishia kwa silaha atakiwa kuadhibiwa kwa uzembe, suala lake ninadhani huwezi kulipeleka kwenye mahakama ya kiraia labda ya kijeshi, kwa mtazamo wangu, yale ni makosa katika oparesheni za kiusalama ambapo anaweza kushitakiwa katika mahakama ya kijeshi. Msingi wa kesi ya kiraia unaweza kuita ni kvamiwa na mtu mwenye silaha anayedhaniwa ni jambazi. Wataalamu wa sheria za kiraia kina Tundu Lissu, Peter Kibatala, John Mallya, Ben Alex Ishabakaki, Jebra Kambole Sr. Na wengine mnaweza kulifafanua vizuri hili...

Na Yericko Nyerere
Hivi Nape ni Mtuhumiwa wa nini ?
 
Ni kweli Kitenge kaingilia mission ya watu wakiwa kazini ni kosa ila detector kutoa pistol kwa unarmed person ni kosa kubwa zaidi na udhalilishaji wa jeshi la policcm.
 
Binafsi nilimuona alievaa shati jeupe kama mtu alie composed and professional...
Kuna wanaompongeza Kitenge. Lakini kwa sheria zetu amezuia askari kufanya kazi yao....kitu ambacho kinaweza kumsumbua, hata kama walikuwa hawajajitambulisha, gari aliloamriwa aingie ni lake na dereva ni wake

Kuhusu makosa ya askari, nadhani kulikuwa na pressure kubwa sana kwa pande zote mbili...it happens.. Ndio mambo ya kazi

Wenye makosa zaid ni waliotuma askari na kutaka kumzuia Nappe kuzungumza, dont twist the thing around...

Aliewatuma wale askari kumzuia Nappe ndio source ya yote hayo...
Kwamba Nappe ni X Min. Anaweza pigiwa tu simu kawaida na yeye akaamua cha kufanya...
But you dont have the right to kill freedom of speech from our countrt, no one....unlikely and un acceptable in any democratic state
 
Mr KGB kwanza hakuna inshara yeyote inayomtambulisha yule kama ni askari askari wanatambulika kwa vitu 3 si kuwa tu na silaha kwani silaha ata raia wa kawaida anaweza kuwa nayo vitu vinavyomtambulisha askari ni

1 Mavazi rasmi au sare
2 Kitambulisho
3Vifaa vya usalama au ulinzi au lugha za kiusalama mfano Name ,rank na serial number (unapozungumzia silaha si kifaa )

Katika vitu vyote nilivyovitaja ambavyo vinamtambulisha askari ktk tukio la jana havikuwapo so kwa maana hyo ni ngumu sana kusema jamaa alikuwa ni askari au alikuwa ni mmoja wa waigizaji ktk tamthilia ya Nape jana

So kwa vitu hyo bdo zitabaki ni hisia tu kuwa yule alikuwa askari au alikuwa muhuni aliyetumwa kucheza kipande chake kama jambazi kuu
 
Kama sio askari, je wale askari waliotumwa na kamanda wa kinondoni kwa ajili ya kwenda kulinda usalama, walichukua hatua gani baada ya yule mvamizi kutoa silaha!
Wachukue hatua gani wakati aliowatuma mmoja?
 
Binafsi nilimuona alievaa shati jeupe kama mtu alie composed and professional...
Kuna wanaompongeza Kitenge. Lakini kwa sheria zetu amezuia askari kufanya kazi yao....kitu ambacho kinaweza kumsumbua, hata kama walikuwa hawajajitambulisha, gari aliloamriwa aingie ni lake na dereva ni wake

Kuhusu makosa ya askari, nadhani kulikuwa na pressure kubwa sana kwa pande zote mbili...it happens.. Ndio mambo ya kazi

Wenye makosa zaid ni waliotuma askari na kutaka kumzuia Nappe kuzungumza, dont twist the thing around...

Aliewatuma wale askari kumzuia Nappe ndio source ya yote hayo...
Kwamba Nappe ni X Min. Anaweza pigiwa tu simu kawaida na yeye akaamua cha kufanya...
But you dont have the right to kill freedom of speech from our countrt, no one....unlikely and un acceptable in any democratic state
Yule jamaa kwanini unahisi ni Askari.
Inawezekana ni Kibaka tu na ile bastola ni Toy.
Kashikwa na Kitene aka Freeze kabisa
 
Back
Top Bottom