Makosa ya hayati Rais Magufuli ambayo Rais Samia lazima ayaepuke kama ukoma

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,502
51,098
Ni ukweli usio na chembe ya shaka Rais Magufuli hatunaye tena, amerudi mavumbini alipotoka ambayo ni safari yetu sote.
Rais Magufuli alikuwa ni mtawala tofauti sana na watangulizi wake na kiukweli kwa mtizamo wangu alifanya makosa makubwa sana kuliko Watangulizi wake ambayo kama Taifa tunapaswa kuyarekebisha kabisa ili kurudisha nchi katika "Utaifa" na maendeleo ya kweli ya wananchi.

Kwa hiyo katika utawala wake, Rais Samia Suluhu Hassan hana budi kuhakikisha hafanyi makosa haya yafuatayo ambayo yalikuwa ni hatari kwa ustawi wa Taifa:

1. Rais Magufuli hakuwa Mtenda haki na aligawa watu
Yeye alikuwa na double standard kwenye kufanya maamuzi ya jambo linaloshabihiana kwa mfano:
a) Aliwavunjia wananchi wa Kimara Mbezi nyumba kwa hoja za kujenga kwenye hifadhi ya barabara kinyume cha sheria, lakini wakati huohuo akaagiza watu wa Mwanza waliojenga kwenye hifadhi ya barabara wasivunjiwe kwa hoja kuwa eti hao walimpa kura—Huu ni ubaguzi na siyo kutenda haki kwa usawa kwa raia wako wa nchi ileile

b) Rais Magufuli aliendesha zoezi la kubaini vyeti feki kwa waajiriwa wa serikali lakini hakufanya hivyo kwa wateule wake wa kisiasa—Licha ya kuwa teuzi zilikuwa zinategemea tu matashi ya anayeteua, lakini kufoji elimu ni ishara ya ukosefu wa uaminifu na ni jinai, tulitegemea Rais Magufuli awe fair kwa wote, yaani watumishi wa umma na wateule wake, lakini yeye aliamua kusulubu watumishi wa umma tu wakati watumishi hao na wateule wake wote wanalipwa kwa kodi za wananchi

2. Rais Magufuli hakuheshimu katiba na sheria
a) Alitoa agizo la kuzuia vyama vya siasa kufanya siasa hadi mwaka 2020 kinyume cha takwa la katiba ya nchi na sheria ya vyama vya siasa iliyotoa uhuru kwa vyama kufanya mikutano ya hadhara, na kutafuta wanachama wapya

b) Rais Magufuli aliunga mkono kitendo cha wanachama 19 wa CHADEMA waliopoka mamlaka ya kamati kuu ya chama chao, na kwenda kuapishwa bungeni kinyume cha sheria za nchi—Yeye kama sehemu mojawapo ya bunge alipaswa akemee uhuni huu badala ya kuunga mkono au kusaidia "kuuwezesha"

c) Rais Magufuli alifanya manunuzi ya baadhi ya vitu vyenye thamani ya mabilioni ya pesa za wananchi bila kufuata sheria ya manunuzi ya umma na bila kupitia kwanza bungeni ili bunge lijadili kwa kina miradi hiyo na kuipitisha au la —Mradi wa ununuzi wa ndege zile bombadia za mwanzo kabisa ni mfano mzuri wa hilo

3. Rais Magufuli alikuwa na viashiria vya wazi vya Udini
Ukiangalia teuzi ambazo Rais Magufuli alifanya, hasa zenye kuivolve watu wengi kwa wakati mmoja, Utaona wazi zililalia sana kwa Wakiristo. Tazama teuzi za maRAS, maDAS, Wenyeviti wa bodi ya mashirika ya umma, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, mabalozi, Tazama Mawaziri kwenye baraza lake mawaziri la mwanzo na hili la sasa (Tena hili la sasa ndo funga kazi, kuna Mawaziri Waislamu watatu/wanne tu katika baraza zima la mawaziri lenye watu zaidi ya 18)—Ni wazi kabisa Rais Magufuli hakuwa mtenda haki kwenye kutoa nafasi kwenye utumishi wa nchi kwa kuangalia demographia ya watu wa Taifa hili. Maana Waislamu wenye elimu, wazalendo wa kutosha, na waadilifu na wachapakazi walikuwepo na wapo, sasa inayumkinika vipi teuzi zilalie upande mmoja kivile?

4. Rais Magufuli aliendesha nchi kupitia style ya "populism" inayoambatana na "uongo" mkubwa na mwingi.

Nchi hii haijawahi kushuhudi kiwango cha propaganda kusifu na kuimba Mapambio tangu enzi za mwalimu kama awamu hii ya Magufuli, Magazeti kila siku ni vichwa vya Magazeti vilivyoandikwa kwa propaganda Kubwa, TBC ndiyo usiseme kabisa, kila siku ni kumpamba Magufuli utadhani ni nabii.
a) Alizindua miradi ambayo tayari ilishazinduliwa na mtangulizi wake
b) Hakutimiza ahadi alizoahidi kwenye ilani ya uchaguzi ya 2015, tena nyingine alizikana waziwazi mfano katiba mpya

5)Magufuli alijali sana vitu, hakujali hisia za watu na hali zao, na mustakbali wa maisha yao
a) Kupora korosho za wananchi kibabe kulitia watu umasikini
b) kuvunja nyumba za wananchi wakati kuna zuio la mahakama ni mfano mwingine
c) kutolipa nyongeza na stahiki za mishahara zilizopo kwa mujibu wa sheria ni mfano mwingine

6)Rais Magufuli alivunja misingi yote ya utawala bora na demokrasia
a) alitumia bunge kupitisha sheria kandamizi za kuminya uhuru wa wananchi, mfano mmojawapo ni sheria ya habari, na sheria ya kuwapa kinga spika na naibu wake wasishtakiwe
b) Alitumia mahakama kunyanyasa wapinzani wake. Akina Lema, Sugu, Mbowe, Msigwan. k wote washatiwa ndani na Magufuli kwa sababu za kisiasa
c) Alitumia vyombo vya dola kuvuruga wapinzani wake wasifanye siasa kipindi cha uchaguzi mkuu, alikamatakamata wagombea wa upinzani, Aliengua wagombea wa upinzani kinguvu na kiuonevu etc
d) Alivuruga chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu na kuwanyima haki wananchi uhuru na haki ya kuchagua viongozi wao etc
e) Alipeleka majeshi Zanzibar na kwa kweli tuliona uchaguzi namna ulivyofanyika kwa viini macho
f) Tulishuhudia akizima bunge lisiwe Live kwa hoja za watu eti wafanye kazi, wakati yeye alijiweka LIVE alipofanya mambo yake
g) Alifungiafungia vyombo vya habari vinavyocriticize aina yake ya utawala etc

Kiufupi Rais Samia Suluhu Hassan ana kazi kubwa ya kurekebisha makosa makubwa kabisa ya kiuongozi ya rais Magufuli. Makosa yale ni very serious kwa mustakbali wa Taifa, Mama Samia ana jukumu kubwa lifuatalo

1. Kutupatia katiba mpya iliyobora, lakini na yeye atawale kwa mujibu wa katiba na kuheshimu haki za watu

2. Kuupiga vita ufisadi siyo kwa Camera na maneno bali kwa vitendo

3. Kutupa maendeleo ya kweli
 
1.kutopandisha mishahara Kwa watumishi..


2.Kuongeza deni la Taifa Kwa kukopa Sana Hadi Kwa bank za biashara huku uongo WA kuwa tunatumia pesa za ndani ukienezwa..


3.kulazimisha miradi isiyo na kichwa wala miguu ...iishe Kwa haraka huku hali hairuhusu....mfano ni Stieggler
Hasara za mradi huo ni kubwa kuliko faida..

4.Uchaguzi uwe huru na haki japo Kwa wabunge ,madiwani na serikali za mitaa
Kama kuiba waibe za Urais Tu kama tulivyozoea..
 
Mwisho wa safari ya kuliongoza taifa hili kwa John Pombe Joseph Magufuli ndio mwanzo wa safari ya Samia Suluhu Hassan

Mussa aliyagawa maji ya bahari ya shamu taifa la Mungu likavuke na wakavuka, Joshua alikausha maji ya mto Jordan

Rais John Pombe Joseph Magufuli alifanya yaliyompasa kufanya na Mungu amemchukua sasa Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea na safari harudi nyuma na atafanya yanayompasa kadri ya safari ilivyo

Mungu ibariki Tanzania
 
1.kutopandisha mishahara Kwa watumishi..


2.Kuongeza deni la Taifa Kwa kukopa Sana Hadi Kwa bank za biashara huku uongo WA kuwa tunatumia pesa za ndani ukienezwa..


3.kulazimisha miradi isiyo na kichwa wala miguu ...iishe Kwa haraka huku hali hairuhusu....mfano ni Stieggler
Hasara za mradi huo ni kubwa kuliko faida..

4.Uchaguzi uwe huru na haki japo Kwa wabunge ,madiwani na serikali za mitaa
Kama kuiba waibe za Urais Tu kama tulivyozoea..
"Stinglers Haina kichwa wala Miguu"!!!
Nimeamini Watanzania hata akija kutawala Nabii Musa mtamwona Hafai. Hakuna kizuri kisichokuwa na kasoro ndugu zangu, Lakini pia Falsafa za Uongozi zinasema huwezi kumfurahisha kila Mtu au Umma wote ukiwa Madarakani, ukitaka kumfurahisha kila mtu kazi ikufaayo ni kuuuza ICE CREAM ZA AZAM!
Tumwache mwendazake apumzike mahala pake. Over
 

Hoja ya udini ni ya kipumbavu na inaonyesha ni namna gani haupo smart upstairs. Hivi ni lini Serikali imewatenga ndugu waislam?

Juzi wakati wa mazishi Mufti Mkuu Sheikh Aboubakhar Zuberi alisema kuwa Magufuli amewajengea msikiti Dar es salaam na msikiti huo unaitwa Mohamed II na pia aliingoza harambee ya ujenzi wa msikiti wa Chamwino. Vipi kuna suala lingine kubwa kwa muislam zaidi ya kumjengea msikiti?

Kwenye vyeo napo upo shalow sana mbali na Rais kuwa mkiristo huoni kuwa huyohyo unayemuita mdini aliteua Jaji mkuuu muislamu? Vipi kuhusu PM majaliwa? Vice president vipi ni mpagani?
 
Kweli akutukanye hakuchagulii tusi! Acheni lawama zisizo na msingi, fanyeni kazi. RIP Magufuli

Ndio walimwengu hao Bayyo,

Hata wakati JK akiwa rais alitukanwa sana na John Pombe Magufuli akiwa waziri alimtia moyo




Juzi kwenye msiba JK amesema watu husemewa yaliyo mabaya wakiwa hai na mazuri wakiwa wamekufa, ila JPM alibahatika kusemwa kwa mazuri akiwa hai

Mama D nilimsemea mazuri, nitaendelea kuyaenzi na kumshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai wake kwa taifa letu, aendelee kupumzika kwa amani kipenzi chetu John Pombe Magufuli 🙏

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake🇹🇿♥️
 
"Stinglers Haina kichwa wala Miguu"!!!
Nimeamini Watanzania hata akija kutawala Nabii Musa mtamwona Hafai. Hakuna kizuri kisichokuwa na kasoro ndugu zangu, Lakini pia Falsafa za Uongozi zinasema huwezi kumfurahisha kila Mtu au Umma wote ukiwa Madarakani, ukitaka kumfurahisha kila mtu kazi ikufaayo ni kuuuza ICE CREAM ZA AZAM!
Tumwache mwendazake apumzike mahala pake. Over

Stieggler ni mgawatt ngapi?
Megawatts elfu mbili ndo uondoe msitu wa wa ekari zaidi ya milioni moja??

Megawatts 2000 si Bora kutumia uranium Tu ambayo ipo Tele ruvuma kuzalisha hata megawatts elfu 10???
 
Hapo hata haujagusia upande wa Ben Sanane, Azory na risasi mmiminiko kwa Mh Tundu, maana kitendo tu hata cha kutokuundwa kamati kuchunguza hizi jinai hakuna

Mama inabidi aanzishe uchunguzi wa hayo ukijumlisha na vile viroba vya binaadam vilivyokuwa vinapatikana ufukweni , mustakabali wa masheikh wa uamsho na zoezi zima la Kibiti, Mkiru inabidi uchunguzi na taarifa zitoke za wazi

Bila kusahau ni maamuzi yapi labda au ni ilani ipi ya kujenga uwanja mkubwa wa ndege kijijini na manunuzi ya hizo ndege

Na mwisho namshauri mama nae aanze tu kuweka watu wa kutaka kumuongezea muda wa kukaa madarakani na pia aanze kujenga mavitu makubwa makubwa huko nyumbani kwao ili kuondoa hizi double standard na akiulizwa aseme mtangulizi wake alionyesha njia na bila kusahau kuteua wateule wengi kwa misingi ya imani zao /yake na maeneo ya anapotoka yeye (Pwani na Kisiwani)
 
Umewaumiza sana vibaraka wa Jiwe ambao hawataki mabaya ya Jiwe yatajwe utafikiri yeye alikuwa malaika , pamoja na kuwa hujataja mauaji , utekaji , ufungaji watu kwenye viroba , ubambikiaji watu kesi za uonezi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha , Jiwe was a human by physical feature but heart wise was a 😈 himself
Screenshot_20210327-201144.png
 

Hoja ya udini ni ya kipumbavu na inaonyesha ni namna gani haupo smart upstairs. Hivi ni lini Serikali imewatenga ndugu waislam? Juzi wakati wa mazishi Mufti Mkuu Sheikh Aboubakhar Zuberi alisema kuwa Magufuli amewajengea msikiti Dar es salaam na msikiti huo unaitwa Mohamed II na pia aliingoza harambee ya ujenzi wa msikiti wa Chamwino. Vipi kuna suala lingine kubwa kwa muislam zaidi ya kumjengea msikiti? Kwenye vyeo napo upo shalow sana mbali na Rais kuwa mkiristo huoni kuwa huyohyo unayemuita mdini aliteua Jaji mkuuu muislamu? Vipi kuhusu PM majaliwa? Vice president vipi ni mpagani?
Kwani umeambiea waislamu wanataka kujengewa misikiti? Mtoa hoja katoa ulinganifu Katika Baraza la mawaziri, we unakuja na hoja ya kujenga misikiti! Kuhusu ma Samia makamu lzm atoke upande mwingine. Je znz utapata mkristo?
 
Back
Top Bottom